< サムエル記Ⅰ 30 >
1 ダビデと其從者第三日にチクラグにいたるにアマレク人すでに南の地とチクラグを侵したりかれらチクラグを撃ち火をもて之を燬き
Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Ziklagi siku ya tatu, Waamaleki walifanya mashambulizi katika Negevu na Ziklagi. Waliupiga Ziklagi, wakauchoma moto mji,
2 其中に居りし婦女を擄にし老たるをも若きをも一人も殺さずして之をひきて其途におもむけり
na kuwachukua mateka wanawake na kila mmoja aliyekuwa ndani yake, mkubwa kwa mdogo. Wao hawakuua hata mmoja, lakini waliwachukua watu na kuondoka nao.
3 ダビデと其從者邑にいたりて視に邑は火に燬けその妻と男子女子は擄にせられたり
Daudi na watu wake walipofika kwenye mji, ulikuwa umechomwa moto - na wake zao, watoto wao wakiume na wakike walichukuliwa mateka.
4 ダビデおよびこれとともにある民聲をあげて哭き終に哭く力もなきにいたれり
Ndipo Daudi na watu aliokuwa nao wakapaza sauti zao na kulia hadi walipokuwa hawana nguvu zaidi za kulia.
5 ダビデのふたりの妻すなはちヱズレル人アヒノアムとカルメル人ナバルの妻なりしアビガルも虜にせられたり
Wake wawili wa Daudi walichukuliwa mateka, yaani Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili aliyekuwa mke wa Nabali Mkarmeli.
6 時にダビデ大に心を苦めたり其は民おのおの其男子女子のために氣をいらだてダビデを石にて撃んといひたればなりされどダビデ其神ヱホバによりておのれをはげませり
Daudi aliguswa sana, maana watu walikuwa wanaongea kuhusu kumpiga mawe, kwa sababu roho za watu wote walihuzunika, kila mtu kwa ajili ya mtoto wake wakiume na wakike, lakini Daudi alijiimarisha katika BWANA, Mungu wake.
7 ダビデ、アヒメレクの子祭司アビヤタルにいひけるは請ふエポデを我にもちきたれとアビヤタル、エポデをダビデにもちきたる
Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, “Tafadhali, niletee hapa ile naivera.”Abiathari akaileta hiyo naivera kwa Daudi.
8 ダビデ、ヱホバに問ていひけるは我此軍の後を追ふべきや我これに追つくことをえんかとヱホバかれにこたへたまはく追ふべし爾かならず追つきてたしかに取もどすことをえん
Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya mwongozo, akisema, “Je, kama nikiliandama jeshi hili, nitalipata?” BWANA akamjibu, “Wafuate, maana kweli utawapata, na kwa hakika utarudisha kila kitu.”
9 ダビデおよびこれとともなる六百人の者ゆきてベソル川にいたれり後にのこれる者はここにとどまる
Kwa hiyo Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye; nao wakafika katika kijito cha Bethori, mahali walipokaa wale walioachwa nyuma.
10 即ちダビデ四百人をひきゐて追ゆきしが憊れてベソル川をわたることあたはざる者二百人はとどまれり
Lakini Daudi aliendelea kuwafuata, yeye na watu mia nne; maana wale mia mbili walibaki nyuma, wakiwa wamechoka kiasi cha kutoweza kuvuka kijito cha Besori.
11 衆人野にて一人のエジプト人を見これをダビデにひききたりてこれに食物をあたへければ食へりまたこれに水をのませたり
Nao walimkuta Mmisri shambani na wakamleta kwa Daudi; wakampatia mkate, na akala; wakampa maji ya kunywa;
12 すなはち一段の乾無花果と二球の乾葡萄をこれにあたへたり彼くらひて其氣ふたたび爽かになれりかれは三日三夜物をもくはず水をものまざりしなり
kisha walimpa kipande cha keki ya tini na vishada viwili vya zabibu. Alipomaliza kula, akapata nguvu tena, kwa kuwa alikuwa hajala mkate wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku.
13 ダビデかれにいひけるは爾は誰の人なる爾はいづくの者なるやかれいひけるは我はエジプトの少者にて一人のアマレク人の僕なり三日まへに我疾にかかりしゆゑにわが主人我をすてたり
Ndipo Daudi akamuuliza, “Wewe ni mtu wa nani? Je, unatoka wapi?” Naye akajibu, “Mimi ni kijana wa Misri, mtumishi wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu siku tatu zilizopita nilikuwa mgonjwa.
14 我らケレテ人の南とユダの地とカレブの南ををかしまた火をもてチクラグをやけり
Tulifanya mashambulizi dhidi ya Negevu ya Wakerethi, na iliyochini ya Yuda, na ile Negevu ya Kalebu, na kuichoma moto Ziklagi.”
15 ダビデかれにいひけるは爾我を此軍にみちびきくだるやかれいひけるは爾我をころさずまた我をわが主人の手にわたさざるを神をさして我に誓へ我爾を此軍にみちびきくだらん
Daudi akamwambia, “Je, utanipeleka hadi kwa jeshi lililofanya mashabulizi?” Huyo Mmisri akasema, “Uniapie kwa Mungu kwamba hautaniua au kunisaliti na kuniweka katika mikono ya bwana wangu, nami nitakupeleka liliko hilo jeshi.”
16 かれダビデをみちびきくだりしが視よ彼等はペリシテ人の地とユダの地より奪ひたる諸の大なる掠取物のためによろこびて飮食し踊りつつ地にあまねく散ひろがりて居る
Yule Mmisri alipompeleka huko Daudi, hao wateka nyara walikuwa wametawanyika kila sehemu, wakila na kunywa, na wakicheza, kwa sababu ya nyara zote walizokuwa wamezitwaa kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka nchi ya Yuda.
17 ダビデ暮あひより次日の晩にいたるまでかれらを撃しかば駱駝にのりて逃げたる四百人の少者の外は一人ものがれたるもの无りき
Daudi akawashambulia tangu jua lilipozama hadi jioni ya siku ya pili. Hakuna mtu aliyeponyoka isipokuwa vijana mia nne, waliopanda ngamia na kukimbia.
18 ダビデはすべてアマレク人の奪ひたる物を取りもどせり其二人の妻もダビデとりもどせり
Daudi akarudisha vyote ambavyo Waamaleki walikuwa wamevichukua; na Daudi akawaokoa wake zake wawili.
19 小きも大なるも男子も女子も掠取物もすべてアマレク人の奪さりし物は一も失はずダビデことごとく取かへせり
Hakuna kilichopotea, si kidogo wala kikubwa, si watoto wa kiume wala wa kike, si mali iliyotekwa, wala chochote ambacho wavamizi alikichukuwa kwa ajili yao. Daudi akawa amerejesha kila kitu.
20 ダビデまた凡の羊と牛をとれり人々この家畜をそのまへに驅きたり是はダビデの掠取物なりといへり
Akachukua makundi yote ya kondoo na ng'ombe, ambayo watu waliyatanguliza mbele ya ng'ombe wengine. Wakisema, “Hizi ni nyara za Daudi.”
21 かくてダビデかの憊れてダビデにしたがひ得ずしてベソル川のほとりに止まりし二百人の者のところにいたるに彼らダビデをいでむかへまたダビデとともなる民をいでむかふダビデかの民にちかづきてその安否をたづぬ
Daudi akafika kwa wale watu mia mbili waliokuwa wamechoka kufuatana naye, wale walioachwa wakae katika kijito cha Besori. Watu hawa wakajitokeza kumlaki na watu waliokuwa naye.
22 ダビデとともにゆきし人々の中の惡く邪なる者みなこたへていひけるは彼等は我らとともにゆかざりければ我らこれに取りもどしたる掠取物をわけあたふべからず唯おのおのにその妻子をあたへてこれをみちびきさらしめん
Ndipo watu wote waovu na wasiofaa miongoni mwa waliokwenda na Daudi wakasema, “Kwa sababu watu hawa hawakwenda nasi, hatutawapa chochote kutoka katika nyara tulizorudisha. Isipokuwa kila mtu aweza kuchukuwa mke na watoto wake, wawatoe na kwenda zao.”
23 ダビデ言けるはわが兄弟よヱホバ我らをまもり我らにせめきたりし軍を我らの手にわたしたまひたれば爾らヱホバのわれらにたまひし物をしかするは宜からず
Ndipo Daudi akasema, “Ndugu zangu, msifanye hivyo, kwa vitu ambavyo BWANA ametupatia. Ametuhifadhi na kuwaweka mkononi mwetu wavamizi waliotuinukia.
24 誰か爾らにかかることをゆるさんや戰ひにくだりし者の取る分のごとく輜重のかたはらに止まりし者の取る分もまた然あるべし共にひとしく取るべし
Ni nani atawasikiliza kuhusu jambo hili? Kwa maana mgawo ni kwa yeyote aendae vitani, basi pia mgawo ni kwa yeyote aliyelinda mizigo; Nao watapata tena kilicho sawa.”
25 この日よりのちダビデこれをイスラエルの法となし例となせり其事今日にいたる
Ilikuwa hivyo tangu siku hiyo hadi leo, maana Daudi aliamua iwe sheria na amri kwa Israeli.
26 ダビデ、チクラグにいたりて其掠取物をユダの長老なる其朋友にわかちおくりて曰しめけるは是はヱホバの敵よりとりて爾らにおくる饋物なり
Daudi alipofika Ziklagi, alituma sehemu ya nyara kwa wazee wa Yuda, kwa rafiki zake, akisema, “Tazama, hii ni zawadi yenu kutokana na nyara za adui wa BWANA.”
27 ベテルにをるもの南のラモテにをるものヤツテルにをる者
Zawadi zilienda kwa wazee waliokuwa Bethueli, na kwa hao waliokuwa Ramothi iliyoko kusini, na kwa hao waliokuwa Yatiri,
28 アロエルにをる者シフモテにをるものエシテモにをるもの
na kwa hao waliokuwa Aroeri, na kwa hao waliokuwa Sifmothi, na kwa hao waliokuwa Eshtemoa
29 ラカルにをるものヱラメル人の邑にをるものケニ人の邑にをるもの
Pia kwa wazee waliokuwa Rakali, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wayerameeli, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wakeni,
30 ホルマにをるものコラシヤンにをるものアタクにをるもの
na kwa hao waliokuwa Horma, na kwa hao waliokuwa Borashani, na kwa hao waliokuwa Athaki,
31 ヘブロンにをるものおよびすべてダビデが其從者とともに毎にゆきし所にこれをわかちおくれり
na kwa hao waliokuwa Hebroni, na kwa sehemu zote ambazo Daudi mwenyewe na watu wake walizoea kwenda.