< 歴代誌Ⅰ 4 >
1 ユダの子等はペレヅ、ヘヅロン、カルミ、ホル、シヨバル
Uzao wa Yuda ulikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri, na Shobali.
2 シヨバルの子レアヤ、ヤハテを生みヤハテ、アホマイおよびラハデを生り是等はザレア人の宗族なり
Shobali alikuwa baba wa Reaya. Reaya alikuwa baba wa Yahathi. Yahathi alikuwa baba wa Ahumai na Lahadi. Hawa walikuwa mababu wa koo za Wasorathi.
3 エタムの父の生る者は左のごとしヱズレル、イシマおよびイデバシその姉妹の名はハゼレルポニといふ
Hawa walikuwa mababu wa ukoo katika mji wa Etamu: Yezreeli, Ishma, na Idbashi. Babu yao alikuwa Haselelponi.
4 ゲドルの父ペヌエル、ホシヤの父エゼル是等はベテレヘムの父エフラタの長子ホルの子等なり
Penueli alikuwa babu wa koo katika mji wa Gedori. Ezeri alikuwa muanzilishi wa koo katika Husha. Hawa walikuwa uzao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi na muanzilishi wa Bethelehemu.
5 テコアの父アシユルは二人の妻を有り即ちヘラとナアラ
Ashuri baba wa Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
6 ナアラ、アシユルによりてアホザム、へペル、テメニおよびアハシタリを產り是等はナアラの產る子なり
Naara alimzalia Ahuzamu, Heferi, Temeni na Ahashtari. Hawa walikua wana wa Naara.
Wana wa Hela walikua Serethi, Ishari, Ethnani,
8 ハツコヅはアヌブおよびゾベバを產り ハルムの子アハルヘルの宗族も彼より出づ
na Kozi, alikua baba wa Anubu na Sobeba, na koo zilizotoka kwa Aharheli mwana wa Harumu.
9 ヤベヅはその兄弟の中にて最も尊ばれたる者なりきその母我くるしみてこれを產たればといひてその名をヤベヅ(くるしみ)と名けたり
Yabesi aliheshimika zaidi ya kaka zake. Mama yake alimuita Yabesi. Alisema, “Kwasababu nimemzaa katika huzuni.”
10 ヤベヅ、イスラエルの神に龥はり我を祝福に祝福て我境を擴め御手をもて我を助け我をして災難に罹りてくるしむこと無らしめたまへと言り神その求むる所を允したまふ
Yabesi akamuita Mungu wa Israeli na kusema, “Kama tu utanibariki mimi, ongeza mipaka yangu, na mkono wako ukuwa juu yangu. Ukifanya hivi utaninusuru na mabaya, ili kwamba niwe huru na huzuni!” Kwa hivyo Mungu akamjalia maombi yake.
11 シユワの兄弟ケルブはメヒルを生りメヒルはエシトンの父なり
Kelubu kaka wa Shuha akawa baba wa Mehiri, aliyekuwa baba wa Eshtoni.
12 エシトンはベテラパ、パセアおよびイルハナシの父テヒンナを生り是等はレカの人なり
Eshtoni akawa baba wa Beth-Rafa, Pasea, na Tehina, ambaye alianzisha mji wa Nahashi. Hawa ni wanaume walioishi Reka.
13 ケナズの子等はオテニエルおよびセラヤ、オテニエルの子はハタテ
Wana wa Kenazi walikua Othinieli na Seraia. Wana wa Othinieli walikuwa Hathathi na Meonothai.
14 メオノタイはオフラを生みセラヤはヨアブを生りヨアブはカラシム(工匠)谷の人々の父なり彼處のものは工匠なればかくいふ
Meonothai akawa baba wa Ofara, na Seraia akawa baba wa Yohabu, mwanzilishi wa Ge Harashimu, ambao watu wake walikua wahunzi.
15 ヱフンネの子カレブの子等はイル、エラおよびナアム、エラの子等およびケナズ
Wana wa Kalebu mwana wa Yefune walikua Iru, Ele na Namu. Wana wa Ela alikua Kenazi.
16 ヱハレレルの子等はジフ、ジバ、テリア、アサレル
Wana wa Yehaleli walikua Zifi, Zifa, Tiriya, na Azareli.
17 エズラの子等はヱテル、メレデ、エペル、ヤロン、メレデの妻はミリアム、シヤンマイおよびイシバを產り イシバはエシテモアの父なり
Wana wa Ezra walikua Yetheri, Meredi, Eferi, na Yaloni.
18 そのユダヤ人なる妻はゲドルの父ヱレデとシヨコの父へベルとザノアの父ヱクテエルを產り是等はメレデが娶りたるパロの女ビテヤの生る子なり
Mke wake Meredi wa Kimisri alimzalia Miriamu, Shamai, na Ishibahi, aliyekua baba wa Eshitemoa. Hawa walikua wana wa Bithia, binti wa Farao, ambaye Meredi alimuoa. Mke wa Kiyahudi wa Meredi alimzalia Yeredi, ambaye alikua baba wa Gedore; Heberi, aliyekua baba wa Soko; na Yekuthieli aliyekua baba wa Zanoa.
19 ナハムの姉妹なるホデヤの妻の生める子等はガルミ人ケイラの父およびマアカ人エシテモアなり
Kati ya watoto wawili wa mke wa Hodia, dada wa Nahamu, mmoja wao kawa baba wa Keila Mgarimite. Mwingine alikua Eshitemoa Mmakathite.
20 シモンの子等はアムノン、リンナ、ベネハナン、テロン、イシの子等はゾヘテおよびべネゾヘテ
Wana wa Shimoni walikua Amnoni, Rina, Beni Hanani, na Tilon. Wana wa Ishi walikua Zohethi na Beni Zoheti.
21 ユダの子シラの子等はレカの父エル、マレシヤの父ラダおよび織布者の家の宗族すなはちアシベアの家の者等
Uzao wa Shela mwana wa Yuda, Ulikua ni Eri baba wa Leka, Laada baba wa Maresha na koo za wafanyakazi wa kushona kule Beth Ashbea,
22 ならびにモアブに主たりしヨキム、コゼバの人々ヨアシおよびサラフ等なり またヤシユブ、レハムといふ者ありその記録は古し
Yoakimu, Wanaume wa Kozeba, na Yoashi na Sarafi, waliokua na mali huko Moabu, lakini walirudi Bethlehemu. ( Maelezo haya yametoka kwenye nakala za zamani.)
23 是等の者は陶工にしてネタイムおよびゲデラに住み王の地に居りてその用をなせり
Baadhi ya watu hawa walikuwa ni wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera na wakawa wafanyakazi wa Mfalme.
24 シメオンの子等はネムエル、ヤミン、ヤリブ、ゼラ、シヤウル
Uzao wa Simeoni ulikua Jamini, Jaribu, Zera, na Shauli.
25 シヤウルの子はシヤルム その子はミブサムその子はミシマ
Shalumu alikua mwana wa Shauli, Mibisamu mwana wa Shalumu, na Mishima mwana wa Mibisamu.
26 ミシマの子はハムエル その子はザツクル その子はシメイ
Ukoo wa Mishima ulikua Hamueli mwana wake, Zakuri mjukuu wake, na Shimei kitukuu chake.
27 シメイには男子十六人女子六人ありしがその兄弟等には多の子あらざりきまたその宗族の者は凡てユダの子孫ほどには殖増ざりき
Shimei alikua na wana kumi na sita na mabinti sita. Kaka yake hakua na watoto wengi, Hivyo koo zao hazikuongezeka kwa idadi kubwa kama wato wa Yuda walivyoongezeka.
28 彼らの住る處はベエルシバ、モラダ、ハザルシユアル
Waliishi Beasheba, Molada, na Hazari Shuali.
Pia waliishi Bilha, Ezemu, Toladi,
Bethueli, Horma, Zikilagi,
31 ベテマルカボテ、ハザルスシム、ベテビリ、シヤライム是等の邑はダビデの世にたるまで彼等の有たりき
Bethi Markabothi, Hazari Susimi, Bethi Biri, na Shaaraimu. Hii ilikua miji yao mpaka utawala wa Daudi.
32 その村郷はエタム、アイン、リンモン、トケン、アシヤンの五の邑なり
Vijiji vyao vitano vilikua Etamu, Aini, Tocheni, na Ashani,
33 またこの邑々の周圍に衆多の村ありてバアルにまでおよべり彼らの住處は是のごとくにして彼ら各々系譜あり
pamoja na mipaka ya vijiji kwa umbali wa Baali. Haya yalikua makazi yao, na walitunza kumbukumbu za uzao wao.
Viongozi wa ukoo walikua Meshobabu, Yamileki, Yoshahi mwana wa Amazia,
35 ヨエル、アシエルの曾孫セラヤの孫ヨシビアの子ヱヒウ
Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia mwana wa Seraia mwana wa Asieli,
36 ヱリオエナイ、ヤコバ、ヱシヨハヤ、アサヤ、アデヱル、ヱシミエル、ベナヤ
Elioenai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaia,
37 およびシピの子ジザ、シピはアロンの子 アロンはヱダヤの子 ヱダヤはシムリの子 シムリはシマヤの子なり
na Ziza mwana wa Shifi mwana wa Aloni mwana wa Yedaia mwana wa Shimiri mwana wa Shemaia.
38 此に名を擧げたる者等はその宗族の中の長たる者にしてその宗家は大に蔓延り
Hawa walio orodheshwa kwa majina walikua viongozi wa koo zao, na koo zao ziliongezeka sana.
39 彼等はその群のために牧場を求めんとてゲドルの西におもむき谷の東の方にいたり
Walienda karibu na Gedori, mashariki mwa bonde, kutafuta malisho ya mifugo yao.
40 つひに膏腴なる善き牧場を見いだせしがその地は廣く靜穩にして安寧なりき其は昔より其處に住たりし者はハム人なればなり
Walipata malisho mengi na mazuri. Nchi ilikua tambarare, tulivu na ya amani. Wahamu waliishi hapo awali.
41 即ち上にその名を記したる者等ユダの王ヒゼキヤの代に往て彼らの幕屋を撃やぶり彼らと其處に居しメウニ人を盡く滅ぼし之に代りて其處に住て今日にいたる是はその群を牧べき牧場其處にありたればなり
Hao walio orodheshwa hapo kwa majina walikuja katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda, na wakashambulia makazi ya Wahamu na Wameuni, ambao pia walikua hapo. Waliwaangamiza kabisa na kuishi hapo sababu walipata malisho kwa ajili ya mifugo yao.
42 またシメオンの子孫の者五百人許イシの子等ペラテア、ネアリア、レバヤ、ウジエルを長としてセイル山に攻ゆき
Wanaume mia tano wa kabila la Simeoni walienda katika mlima Seiri, na viongozi wao Pelatia, Nearia, Refaia, na Uzieli, wana wa Ishi.
43 アマレキ人の逃れて遺れる者を撃ほろぼして今日まで其處に住り
Waliwashinda wakimbizi wa Waamaleki waliobakia, na wakaishi hapo hadi siku hii.