< Isaia 2 >

1 Ciò che Isaia, figlio di Amoz, vide riguardo a Giuda e a Gerusalemme.
Vitu ambavyo Isaya mtoto Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu.
2 Alla fine dei giorni, il monte del tempio del Signore sarà eretto sulla cima dei monti e sarà più alto dei colli; ad esso affluiranno tutte le genti.
Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale.
3 Verranno molti popoli e diranno: «Venite, saliamo sul monte del Signore, al tempio del Dio di Giacobbe, perché ci indichi le sue vie e possiamo camminare per i suoi sentieri». Poiché da Sion uscirà la legge e da Gerusalemme la parola del Signore.
Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu.
4 Egli sarà giudice fra le genti e sarà arbitro fra molti popoli. Forgeranno le loro spade in vomeri, le loro lance in falci; un popolo non alzerà più la spada contro un altro popolo, non si eserciteranno più nell'arte della guerra.
Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena.
5 Casa di Giacobbe, vieni, camminiamo nella luce del Signore.
Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe.
6 Tu hai rigettato il tuo popolo, la casa di Giacobbe, perché rigurgitano di maghi orientali e di indovini come i Filistei; agli stranieri battono le mani.
Kwa maana mmewatekeleza watu wenu, nyumba ya Yakobo, wamejazwa na desturi kutoka mashariki na dalili kutokea kama mfilisti, na watasalimiana kwa mikono na wana wa wageni.
7 Il suo paese è pieno di argento e di oro, senza fine sono i suoi tesori; il suo paese è pieno di cavalli, senza numero sono i suoi carri.
Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, na hakuna mipaka katika utajiri wao; nchi yao pia imejaa farasi, wala hakuna mipika ya magari.
8 Il suo paese è pieno di idoli; adorano l'opera delle proprie mani, ciò che hanno fatto le loro dita.
Nchi yao pia imejaa sanamu; wanaabu utengenezaji wa mikono yao wenyewe, vitu aambavyo vidole vyao vimetengeneza.
9 Perciò l'uomo sarà umiliato, il mortale sarà abbassato; tu non perdonare loro.
Watu watainama chini, na kila mmoja atanguka chini; hivyo basi msiwanyanyue juu.
10 Entra fra le rocce, nasconditi nella polvere, di fronte al terrore che desta il Signore, allo splendore della sua maestà, quando si alzerà a scuotere la terra.
Nendeni maeneo yenye miamba na mjifiche kwenye aridhi kwa hofu ya Yahwe na kwa utukufu wa enzi yake.
11 L'uomo abbasserà gli occhi orgogliosi, l'alterigia umana si piegherà; sarà esaltato il Signore, lui solo in quel giorno.
Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
12 Poiché ci sarà un giorno del Signore degli eserciti contro ogni superbo e altero, contro chiunque si innalza ad abbatterlo;
Maana kutakuwa na siku ya Yahwe wa majeshi juu ya yeyote anayejigamba na kujiinua juu, na dhidi ya yeyote mwenye kiburi na atashushwa chini-
13 contro tutti i cedri del Libano alti ed elevati, contro tutte le querce del Basan,
na dhidi ya mierezi ya Lebanoni iliyo juu na kupandishwa juu, na dhidi ya mialoni ya Bashani.
14 contro tutti gli alti monti, contro tutti i colli elevati,
Siku hiyo ya Yahwe wa majeshi itakuwa dhidi ya milima yote mirefu, na dhidi ya vilima vyote vilivyonyanyuliwa juu,
15 contro ogni torre eccelsa, contro ogni muro inaccessibile,
na dhidi ya minara mirefu, na dhidi ya kila ukutaunaojitokeza,
16 contro tutte le navi di Tarsis e contro tutte le imbarcazioni di lusso.
na dhidi ya merikebu zote za Tarshishi, na dhidi ya vyombo vizuri vya meli.
17 Sarà piegato l'orgoglio degli uomini, sarà abbassata l'alterigia umana; sarà esaltato il Signore, lui solo in quel giorno
Kiburi cha mwanaume kitashushwa chini, na kiburi cha wanaume kitaanguka; Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
18 e gli idoli spariranno del tutto.
Sanamu zote zitaondolewa.
19 Rifugiatevi nelle caverne delle rocce e negli antri sotterranei, di fronte al terrore che desta il Signore e allo splendore della sua maestà, quando si alzerà a scuotere la terra.
Wanaume wataingia kwenye mapango ya miamba na mashimo ya aridhi, kwa hofu ya Yahwe, na kwa utukufu wa enzi yake, atakapo nyanyuka na kuitisha nchi.
20 In quel giorno ognuno getterà gli idoli d'argento e gli idoli d'oro, che si era fatto per adorarli, ai topi e ai pipistrelli,
Siku hiyo watu watatupa sanamu zao za fedha na dhahabu ambazo wametengeneza wenyewe kwa ajili ya kuabudia - watazitupa mbali kwa fuko na popo.
21 per entrare nei crepacci delle rocce e nelle spaccature delle rupi, di fronte al terrore che desta il Signore e allo splendore della sua maestà, quando si alzerà a scuotere la terra.
Watu wataingia kwenye miamba kupitia mwanya itakuwa miamba chakavu, kwa hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake,
22 Guardatevi dunque dall'uomo, nelle cui narici non v'è che un soffio, perché in quale conto si può tenere?
usimwaminia mtu, ambae pumzi yake inatokea katika pua yake, ni kwa kiasi gan?

< Isaia 2 >