< 1 Tessalonicesi 5 >
1 Riguardo poi ai tempi e ai momenti, fratelli, non avete bisogno che ve ne scriva;
Sasa, kwa habari ya muda na nyakati, ndugu, hamna haja kwamba kitu chochote kiandikwe kwenu.
2 infatti voi ben sapete che come un ladro di notte, così verrà il giorno del Signore.
Kwa kuwa ninyi wenyewe mwajua kwa usahihi ya kuwa siku ya Bwana inakuja kama mwizi ajapo usiku.
3 E quando si dirà: «Pace e sicurezza», allora d'improvviso li colpirà la rovina, come le doglie una donna incinta; e nessuno scamperà.
Pale wasemapo kuna “Amani na usalama”, ndipo uharibifu huwajia ghafla. Ni kama utungu umjiavyo mama mwenye mimba. Hawataepuka kwa njia yeyote.
4 Ma voi, fratelli, non siete nelle tenebre, così che quel giorno possa sorprendervi come un ladro:
Lakini ninyi, ndugu hampo kwenye giza hata ile siku iwajie kama mwizi.
5 voi tutti infatti siete figli della luce e figli del giorno; noi non siamo della notte, né delle tenebre.
Kwa maana ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi siyo wana wa usiku au wa gizani.
6 Non dormiamo dunque come gli altri, ma restiamo svegli e siamo sobrii.
Hivyo basi, tusilale kama wengine walalavyo. Bali tukeshe na kuwa makini.
7 Quelli che dormono, infatti, dormono di notte; e quelli che si ubriacano, sono ubriachi di notte.
Kwa kuwa wanaolala hulala usiku na wanao lewa hulewa usiku.
8 Noi invece, che siamo del giorno, dobbiamo essere sobrii, rivestiti con la corazza della fede e della carità e avendo come elmo la speranza della salvezza.
Kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, tuwe makini. Tuvae ngao ya imani na upendo, na, kofia ya chuma, ambayo ni uhakika wa wokovu wa wakati ujao.
9 Poiché Dio non ci ha destinati alla sua collera ma all'acquisto della salvezza per mezzo del Signor nostro Gesù Cristo,
Kwa kuwa Mungu hakutuchagua mwanzo kwa ajili ya gadhabu, bali kwa kupata wokovu kwa njia ya Bwana Yesu Kristo.
10 il quale è morto per noi, perché, sia che vegliamo sia che dormiamo, viviamo insieme con lui.
Yeye ndiye aliyetufia ili kwamba, tukiwa macho au tumelala, tutaishi pamoja naye.
11 Perciò confortatevi a vicenda edificandovi gli uni gli altri, come gia fate.
Kwa hiyo, farijianeni na kujengana ninyi kwa ninyi, kama ambavyo tayari mnafanya.
12 Vi preghiamo poi, fratelli, di aver riguardo per quelli che faticano tra di voi, che vi sono preposti nel Signore e vi ammoniscono;
Ndugu, twawaomba muwatambue wale wanaotumika miongoni mwenu na wale walio juu yenu katika Bwana na wale wanao washauri.
13 trattateli con molto rispetto e carità, a motivo del loro lavoro. Vivete in pace tra voi.
Tunawaomba pia muwatambue na kuwapa heshima katika upendo kwa sababu ya kazi yao. Muwe na amani miongoni mwenu ninyi wenyewe.
14 Vi esortiamo, fratelli: correggete gli indisciplinati, confortate i pusillanimi, sostenete i deboli, siate pazienti con tutti.
Twawasihi, ndugu: muwaonye wasio kwenda kwa utaratibu, watieni moyo walio kata tamaa, Wasaidieni walio wanyonge, na muwe wavumilivu kwa wote.
15 Guardatevi dal rendere male per male ad alcuno; ma cercate sempre il bene tra voi e con tutti.
Angalieni asiwepo mtu yeyote anayelipa baya kwa baya kwa mtu yeyote. Badala yake, fanyeni yaliyo mema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote.
17 pregate incessantemente,
Ombeni bila kukoma.
18 in ogni cosa rendete grazie; questa è infatti la volontà di Dio in Cristo Gesù verso di voi.
Mshukuruni Mungu kwa kila jambo, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo.
19 Non spegnete lo Spirito,
Msimzimishe Roho.
20 non disprezzate le profezie;
Msiudharau unabii.
21 esaminate ogni cosa, tenete ciò che è buono.
Yajaribuni mambo yote. Mlishike lililo jema.
22 Astenetevi da ogni specie di male.
Epukeni kila mwonekano wa uovu.
23 Il Dio della pace vi santifichi fino alla perfezione, e tutto quello che è vostro, spirito, anima e corpo, si conservi irreprensibile per la venuta del Signore nostro Gesù Cristo.
Mungu wa amani awakamilishe katika utakatifu. Roho, nafsi na mwili vitunzwe pasipo mawaa katika kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
24 Colui che vi chiama è fedele e farà tutto questo!
Yeye aliyewaita ni mwaminifu, naye ndiye mwenye kutenda.
25 Fratelli, pregate anche per noi.
Ndugu, tuombeeni pia.
26 Salutate tutti i fratelli con il bacio santo.
Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.
27 Vi scongiuro, per il Signore, che si legga questa lettera a tutti i fratelli.
Nawasihi katika Bwana kwamba barua hii isomwe kwa ndugu wote.
28 La grazia del Signore nostro Gesù Cristo sia con voi.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.