< Matayo 5 >
1 U Yesu naewaliona iumbi, akahega akalongola Mulugulu, naewikie pihi, iamanyisigwa akwe akaza kitalakwe.
Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,
2 Akaligitya nukuamanyisa, akalunga,
naye akaanza kuwafundisha:
3 “Bahu awa nia kia amunkolo kunsoko utemi wa kigulu wao.
“Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 Bahu niakite ikinyauwai, azizapumbuligwa.
Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
5 Bahu awa niapolo, kunsoko azizamisala ihi.
Heri walio wapole, maana watairithi nchi.
6 Bahu awa niakite inzala ni nyota atai kunsoko azizalisigwa ikute.
Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.
7 Bahu awania hegelya imilanda nienso aziza hegeligwa.
Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.
8 Bahu awa niankolo nza azemuona Itunda.
Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.
9 Bahu awa niakaminkanya, nsoko nianso azezitangwa ana ang'wi Tunda.
Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.
10 Bahu awa neitumigwa usese kunsoko atai, nsoko utemi wa kigulu wao.
Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Bahu unye niantu akumutukila nukumitumya ubi, nukumligitya ubi nuteele kunsoko ane.
“Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
12 Lowi nukulumbiilya kunsoko ikipegwa kanyu kikulu kigulu. Kunsoko inge uu aiaitumilya ubi ianyakidagu nia kali.
Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
13 Unye mi munyu wa unkumbigulu umunyu iga ulimilye umulyo wake, ukutula ne munyu hange? Singa ukutula uza kukintu nikingiza inge ukugung'wa kunzi nukupambatwa nimigulu aantu.
“Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 Unye miwelu wa unkumbigulu. Ihi nizengilwe mulugulu nishalipihile.
“Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
15 Iantu singa akakilya ulumule nukuluika pihi a nkapu, akumiika migulya, ikualika ihi niakoli munyumba.
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
16 Leka uwelu wanyu welye kuntongeela aantu kunsoko aione intendo yanyu ninza hangi amukulye utata wanyu nuakigulu.
Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”
17 Leki kusigiili kina ainzile gazanja uzipiili nia anyakidagu. Singa zegazanja zilekondanilya.
“Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
18 Kutai kumuila unkumbigulu nihi ihi ukile hangi kutile uzipiilya hata nung'wi, mpaka nuzetula wakondigwa.
Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
19 Kululo wihi nuibananga ilagiilyo ninino nilamalagiilyo aya nukuamanyisa kituma niangiza uu ukitangwa munino muutemi wa kigulu. Inge gwa wihi nuiambile nukuimanyisa ukitangwa muutemi wa kigulu.
Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
20 Kunsoko numuie itai anyu igehite kumikelinkela itai a mafarisayo, shanga mukingile mtemi wa kigulu.
Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
21 Amigulu ikali ailambuwe kina leka, “kubulaga” numubulagi wihi ukole mubii wa ulamulya.
“Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.
22 Hangi kumuila wihi ni shumuloilwe muluna akwe ukutula ukole mubii wa ulamulwa. Hangi muntu wihi nukumuila umunyandugu wakwe kina shufaile! ukutula mubii wianza. Nuyu wihi nuilunga uwe wimupungu, ukutula mubii wa moto wamu jehanamu. (Geenna )
Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: Pumbavu atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu. (Geenna )
23 Ang'wi ukupumya isongeelyo kuntongeela ikumbikilo, kunu aza mileile numunyandugu shamiungamie,
Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
24 Lileke isongeelyo pa ntongeela pi kumbikilo, uambi nzila ende miungamile hanza numunyandugu wako, usuke uzupumye gwa isongeelyo.
iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
25 Kayi igombi numilei wako munzila nimukili mulongoe kianza, hakamuhite kigombya umilei wako uhumile akuleke mumikono angwa mlamuli hangi ugung'we kukitungo.
“Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
26 Tai numuie shangaukulekelwa mpaka mulipe impia nimudaigwe.
Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya mwisho.
27 Migule iligitigwe kina leka, “Kugoolya.”
“Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!
28 Numuie kina wihi nukumugoza umusungu nukumulowa wagoolya munkolo akwe.
Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.
29 Ang'wi iliho lako nila mukono wako nua kigoha lenda kutwala muibe, liheje uligume kule nuewe, ikatula bahu muili unino ugung'we unukulu uguneke kugung'wa ku jehanamu. (Geenna )
Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling'oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu. (Geenna )
30 Ang'we umukono wa kigoha inda nsoko akukumpa uteme ugume kuli, sunga umuili nungiza uleke kugung'wa ku jehanamu. (Geenna )
Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu. (Geenna )
31 Itambuwe kina wihi nukumuzunsa umusungu wakwe ampe ikilingisilyo kutai na ulamulwa.
“Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.
32 Une numuie wihi nukumleka umusungu wakwe nsoko a ugoolya, ukutula wituma usambo. Hangi wihi nukumuhugela anga wapegwa ulamulwa wa tai ukutula wituma usambo.
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
33 Hangi migule aitambuue kuantu ao niakali, leki kutambuli uteele, kululo twali itai anyu kumukulu.
“Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
34 Une numuie, leki kutambula hata niniino, ang'wi kigulu, nsoko kung'wanso kung'witunda.
Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu;
35 Ang'wi mihi, nsoko wieka ituntu lakupambatilya impambatilyo yakwe ang'wi Yerusalemu, nsoko ingi kisali ni kamutemi numukulu.
wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.
36 Leka kulapa nitwe lako, kunsoko shukulipeula isingi ling'we litule lyelu ang'wi ilwaalu.
Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Ingi gwa inkani yanyu, tai, tai, singau, singa u, kunsoko ayo nakangeelya ipuma kumulugu.
Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
38 Migule iligitigwe kina, liho na liho ni lino na lino.
“Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino.
39 Une numuie leki inkungumi nu muntu nu mubii, anga wakukua ikunda nilamkono wa kigoha mupiuele nilulya.
Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.
40 Ang'wi wihi nuloilwe kulongola nuewe kianza anga wakuhegelya inkanzu ako, muleke ni joho lao.
Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.
41 Nuyu wihi nukuonyeelya kulongola muhinzo ung'we, longola nung'wenso mihinzo ibiili.
Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
42 Wihi nukulompa mpe, hangi uleke kumuhita uyu nutakile umukopise.
Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopa kitu usimnyime.
43 Migule iligitigwe mlowe umunyakisali wako, na umuhukilwe umubi wako.
“Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.
44 Kululo numuie, alowi iabi anyu, alompeeli awa nimutasha.
Lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyi
45 Ingi gwa mutule miano wang'wa tata wanyu nuakigulu, kunsoko wialikila ilyoa iabi niaza. Hangi wikuisa imbula kuabi niaza.
ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
46 Anga mualowe ao nizamualoilwe nye, mipata kintu kii? Aiahoela mpia shaituma ne itii?
Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi? Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!
47 Anga mulamushe ianyandugu anyu du mipata ntuni kua uya? Ianyakilungu shaituma ne uu?
Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
48 Kululo ihumikile mutule mia tai, anga utata wanyu nuakigulu nukoli mutai.
Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.