< 1 Korintho 10 >
1 Ndoilwe unye mulenge akak niadada ane, kina iatata itu aeakole pihe ilunde hange ehi aeakiie mubahali.
Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari.
2 Ehi ekabadisigwa kutula ang'wa Musa mulunda mukati numukati mubahali,
Wote walibatizwa katika umoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari.
3 hange ehi ikalya indya zizo zizoo niakinkolo.
Wote walikula chakula kilekile cha kiroho,
4 Ehi ekang'wa ekeng'wi kiko kikoo nikakinkolo. Ndogoilyo aeang'ee kupuma migwe lakinkolo naeliatyatile, nigwe nilanso aeKilisto.
wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.
5 Kuite Itunda singaaeuloeigwe kukila nawa niang'wao nemeimbaao ikasapatiligwa mumbuga.
Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
6 Inge imakani aya ehi aekilengasiilyo kitu, nsoko usese kuleke kutula antu ansula niembi anga nianso naeitu.
Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.
7 Muleke kukulya iadudu, anga niang'wi ao naeile. Eye anga niandekile, “Iantu aeikie pihe akalya nukung'wa, hange ikauka kiginsa kunsula yaukosi.
Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.”
8 Kuleke kituma ukosi anga niidu ao naetumile. Ikasasha luhiku lung'wi antu makumi ambiili nuu tata elfu kunsoko yiyo.
Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Hange kuleke kumugema Ukilisto, anga niidu ao naeitumile ikabepigwa ninzoka.
Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.
10 Hange gwa muleke kisusumya, anga niidu ao naeisusumilye nukubepigwa numalaeka waashi.
Wala msinung'unike kama baadhi yao walivyonung'unika, wakaangamizwa na Mwangamizi!
11 Inge imakani aya aeatendekile anga ilengasiilyo yitu. Akaandekwa nsoko akukenela usese - nekupikewe nempelo nakali. (aiōn )
Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwisho wa nyakati unatukabili. (aiōn )
12 Kuite kela nukiona wemekile nuatule nukilangaila waleke kugwa.
Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.
13 Kutile geng'wa nelemupatile unye nesinga kawaeda aantu. Inge Itunda watai. Singa ukumuleka mugeng'we kukila muukumi wanyu. Palung'wi nigeng'wa nuanso ukumupa mumulango nuakupumile nsoko muhume kudula.
Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
14 Kuite gwa, alowa ane, lemanki ikulyo nelaadudu.
Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu.
15 Kutambula nunyenye anga antu neakete imahala, nsoko mulamule kuaya nekumatambula.
Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo.
16 Ikekombe nikakukembeta nikukikembetile, singa upalung'wi nuasakami ang'wa Kilisto? Umukate uo nekuuega, singa upalung'wi nuamuili wang'wa Kilisto?
Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
17 Kunsoko umukate ung'wi, usese nikiidu kiamuili ung'wi. Usese kehi kuusingiilya umukate ung'wi kupalung'wi.
Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.
18 Agozi iantu akuisilaeli. Itee awa ehi neeliza izabihu singa ipalung'wine pakizindaalo?
Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe: kwao, wenye kula vilivyotambikiwa madhabahuni waliungana na hiyo madhabahu.
19 Kulunga ulegwa? Kina ududu kentunee? Ang'wi kina uludya nulupumigwe isongeelyo kududu kentune?
Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya sanamu?
20 Kuite kutunga kumaintu nanso niapumilye isongeelyo iantu anyakilungu niamihe, kina akupumya imaintu aya kuahing'wi hange singa kung'wi Tunda. Nunee singantakile unyenye kutula mepalung'wi niaking'wi!
Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe na ushirika na pepo.
21 Shanga mukung'wela ikekombe ka Mukulu nikekombe kaahing'wi. Shanga mukutula palung'wi mumeza a Mukulu nemeza nahung'wi.
Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya pepo.
22 Ang'wi kuumupa Umukulu wetu? Kukete ngulune kukilanuanso?
Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu zaidi kuliko yeye?
23 Imaintu ehi anonee, “kuite singa ehe agombigwe. Maintu ehi anonee” kuite singa ehi neeakulya eantu.
Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga.
24 Kutile anga nung'wi nukuduma nimaza nakweudu. kuleka gwa ite, kukela ung'wiao azuzeeduma nimaza namiakwe.
Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake.
25 Muhumile kulya kela kintu nekikuguligwa kinsoko muleke kukolyakolya kunsoko amasigo.
Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu;
26 Ndogoilyo, Uunkumbigulu nsao a Mukulu, hange ehi nuuizue.
maana Maandiko yasema: “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.”
27 Numuntu nushuhuie anga wanutanga kulya hange malowa kulongola, mulye kehi nukumupe muleke kukolya imakolyo namasigo.
Kama mtu ambaye si muumini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
28 Kuite umuntu anga wamuile, “Uludya ulu lupumigwe isongeelyo nianyakilungu,” leki kulya. Eye kunsoko akwe numuiya, hange kunsoko amasigo.
Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
29 Nunee singa nimaie anga masigo anyu, inge masigo amungiza. Kundogoilyo kuniki uwidesi wane ulamulwe nimasigo amuntu mungiza?
Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: “Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?
30 Angeze unene kutumela indya kilumbi, kuneke tukilwe kukentu nensongeeye kukenso?
Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?”
31 Kuite gwa kehi nemukulya ang'wi mukung'wa, ang'wi kehi nemukituma, itumi ehi kunsoko aukulu wang'wi Tunda.
Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
32 Leki kuakoseshi Iayahudi ang'wi Iayunani, ang'w Itekeelo lang'wi Tunda.
Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu.
33 Gemi anga unene nenegema kualoelya iantu ehi kumakani ehi. Shanga kuduma anga nsailo ane unene, inge naangiza. Nunee kituma ite nsoko alije uguneki.
Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.