< Zsoltárok 149 >
1 Hallelúja! Énekeljetek az Örökkévalónak új éneket, dicsérete hangozzék a jámborok gyülekezetében!
Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu.
2 Örüljön Izraél a teremtőjében, Czión fiai vigadjanak királyukban!
Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao.
3 Dicsérjék nevét körtáncz mellett, dobbal és hárfával zengjenek neki.
Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi.
4 Mert az Örökkévalónak kedve telik népében, megdicsőíti az alázatosakat segítséggel.
Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu.
5 Vígadjanak a jámborok dicsőségben, ujjongjanak fekvőkelyeiken;
Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao.
6 Isten magasztalása torkukban, és két élü kard kezükben
Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao
7 hogy bosszút végezzenek a nemzeteken, fenyítéseket a népeken;
kutekeleza kisasi juu ya mataifa na matendo ya adhabu juu ya watu.
8 hogy megkössék királyaikat bilincsekkel, s előkelőiket vasbéklyókkal;
Nao watawafunga wafalme wao kwa minyororo na wakuu wao kwa pingu za chuma. Watatekeleza hukumu ambayo imeandikwa.
9 hogy végezzék rajtuk a megirott törvényt. Dísze az mind az ő jámborainak. Hallelúja!
Hii itakuwa ni heshima kwa ajili ya watakatifu wake wote. Msifuni Yahwe.