< תהילים 9 >

למנצח עלמות לבן מזמור לדוד אודה יהוה בכל לבי אספרה כל נפלאותיך׃ 1
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
אשמחה ואעלצה בך אזמרה שמך עליון׃ 2
Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
בשוב אויבי אחור יכשלו ויאבדו מפניך׃ 3
Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako.
כי עשית משפטי ודיני ישבת לכסא שופט צדק׃ 4
Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki.
גערת גוים אבדת רשע שמם מחית לעולם ועד׃ 5
Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu; umeyafuta majina yao milele na milele.
האויב תמו חרבות לנצח וערים נתשת אבד זכרם המה׃ 6
Uharibifu usiokoma umempata adui, umeingʼoa miji yao; hata kumbukumbu lao limetoweka.
ויהוה לעולם ישב כונן למשפט כסאו׃ 7
Bwana anatawala milele, ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.
והוא ישפט תבל בצדק ידין לאמים במישרים׃ 8
Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki, atatawala mataifa kwa haki.
ויהי יהוה משגב לדך משגב לעתות בצרה׃ 9
Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.
ויבטחו בך יודעי שמך כי לא עזבת דרשיך יהוה׃ 10
Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao.
זמרו ליהוה ישב ציון הגידו בעמים עלילותיו׃ 11
Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.
כי דרש דמים אותם זכר לא שכח צעקת עניים׃ 12
Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa.
חננני יהוה ראה עניי משנאי מרוממי משערי מות׃ 13
Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,
למען אספרה כל תהלתיך בשערי בת ציון אגילה בישועתך׃ 14
ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni na huko niushangilie wokovu wako.
טבעו גוים בשחת עשו ברשת זו טמנו נלכדה רגלם׃ 15
Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.
נודע יהוה משפט עשה בפעל כפיו נוקש רשע הגיון סלה׃ 16
Bwana anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.
ישובו רשעים לשאולה כל גוים שכחי אלהים׃ (Sheol h7585) 17
Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. (Sheol h7585)
כי לא לנצח ישכח אביון תקות ענוים תאבד לעד׃ 18
Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.
קומה יהוה אל יעז אנוש ישפטו גוים על פניך׃ 19
Ee Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde. Mataifa na yahukumiwe mbele zako.
שיתה יהוה מורה להם ידעו גוים אנוש המה סלה׃ 20
Ee Bwana, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.

< תהילים 9 >