< תהילים 89 >
משכיל לאיתן האזרחי חסדי יהוה עולם אשירה לדר ודר אודיע אמונתך בפי׃ | 1 |
Utenzi wa Ethani Mwezrahi. Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.
כי אמרתי עולם חסד יבנה שמים תכן אמונתך בהם׃ | 2 |
Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.
כרתי ברית לבחירי נשבעתי לדוד עבדי׃ | 3 |
Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi,
עד עולם אכין זרעך ובניתי לדר ודור כסאך סלה׃ | 4 |
‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’”
ויודו שמים פלאך יהוה אף אמונתך בקהל קדשים׃ | 5 |
Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.
כי מי בשחק יערך ליהוה ידמה ליהוה בבני אלים׃ | 6 |
Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana?
אל נערץ בסוד קדשים רבה ונורא על כל סביביו׃ | 7 |
Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
יהוה אלהי צבאות מי כמוך חסין יה ואמונתך סביבותיך׃ | 8 |
Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, ni nani aliye kama wewe? Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka.
אתה מושל בגאות הים בשוא גליו אתה תשבחם׃ | 9 |
Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.
אתה דכאת כחלל רהב בזרוע עזך פזרת אויביך׃ | 10 |
Wewe ulimponda Rahabu kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako.
לך שמים אף לך ארץ תבל ומלאה אתה יסדתם׃ | 11 |
Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo.
צפון וימין אתה בראתם תבור וחרמון בשמך ירננו׃ | 12 |
Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.
לך זרוע עם גבורה תעז ידך תרום ימינך׃ | 13 |
Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa.
צדק ומשפט מכון כסאך חסד ואמת יקדמו פניך׃ | 14 |
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.
אשרי העם יודעי תרועה יהוה באור פניך יהלכון׃ | 15 |
Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana.
בשמך יגילון כל היום ובצדקתך ירומו׃ | 16 |
Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako.
כי תפארת עזמו אתה וברצנך תרים קרננו׃ | 17 |
Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu.
כי ליהוה מגננו ולקדוש ישראל מלכנו׃ | 18 |
Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
אז דברת בחזון לחסידיך ותאמר שויתי עזר על גבור הרימותי בחור מעם׃ | 19 |
Ulizungumza wakati fulani katika maono, kwa watu wako waaminifu, ukasema: “Nimeweka nguvu kwa shujaa, nimemwinua kijana miongoni mwa watu.
מצאתי דוד עבדי בשמן קדשי משחתיו׃ | 20 |
Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimemtia mafuta yangu matakatifu.
אשר ידי תכון עמו אף זרועי תאמצנו׃ | 21 |
Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu.
לא ישא אויב בו ובן עולה לא יעננו׃ | 22 |
Hakuna adui atakayemtoza ushuru, hakuna mtu mwovu atakayemwonea.
וכתותי מפניו צריו ומשנאיו אגוף׃ | 23 |
Nitawaponda adui zake mbele zake na kuwaangamiza watesi wake.
ואמונתי וחסדי עמו ובשמי תרום קרנו׃ | 24 |
Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.
ושמתי בים ידו ובנהרות ימינו׃ | 25 |
Nitauweka mkono wake juu ya bahari, mkono wake wa kuume juu ya mito.
הוא יקראני אבי אתה אלי וצור ישועתי׃ | 26 |
Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’
אף אני בכור אתנהו עליון למלכי ארץ׃ | 27 |
Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.
לעולם אשמור לו חסדי ובריתי נאמנת לו׃ | 28 |
Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara.
ושמתי לעד זרעו וכסאו כימי שמים׃ | 29 |
Nitaudumisha uzao wake milele, kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.
אם יעזבו בניו תורתי ובמשפטי לא ילכון׃ | 30 |
“Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu,
אם חקתי יחללו ומצותי לא ישמרו׃ | 31 |
kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu,
ופקדתי בשבט פשעם ובנגעים עונם׃ | 32 |
nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga,
וחסדי לא אפיר מעמו ולא אשקר באמונתי׃ | 33 |
lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
לא אחלל בריתי ומוצא שפתי לא אשנה׃ | 34 |
Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
אחת נשבעתי בקדשי אם לדוד אכזב׃ | 35 |
Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi:
זרעו לעולם יהיה וכסאו כשמש נגדי׃ | 36 |
kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
כירח יכון עולם ועד בשחק נאמן סלה׃ | 37 |
kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.”
ואתה זנחת ותמאס התעברת עם משיחך׃ | 38 |
Lakini wewe umemkataa, umemdharau, umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.
נארתה ברית עבדך חללת לארץ נזרו׃ | 39 |
Umelikana agano lako na mtumishi wako, na umeinajisi taji yake mavumbini.
פרצת כל גדרתיו שמת מבצריו מחתה׃ | 40 |
Umebomoa kuta zake zote, na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.
שסהו כל עברי דרך היה חרפה לשכניו׃ | 41 |
Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; amekuwa dharau kwa jirani zake.
הרימות ימין צריו השמחת כל אויביו׃ | 42 |
Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, umewafanya watesi wake wote washangilie.
אף תשיב צור חרבו ולא הקימתו במלחמה׃ | 43 |
Umegeuza makali ya upanga wake, na hukumpa msaada katika vita.
השבת מטהרו וכסאו לארץ מגרתה׃ | 44 |
Umeikomesha fahari yake, na kukiangusha kiti chake cha enzi.
הקצרת ימי עלומיו העטית עליו בושה סלה׃ | 45 |
Umezifupisha siku za ujana wake, umemfunika kwa vazi la aibu.
עד מה יהוה תסתר לנצח תבער כמו אש חמתך׃ | 46 |
Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?
זכר אני מה חלד על מה שוא בראת כל בני אדם׃ | 47 |
Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!
מי גבר יחיה ולא יראה מות ימלט נפשו מיד שאול סלה׃ (Sheol ) | 48 |
Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? (Sheol )
איה חסדיך הראשנים אדני נשבעת לדוד באמונתך׃ | 49 |
Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni, ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?
זכר אדני חרפת עבדיך שאתי בחיקי כל רבים עמים׃ | 50 |
Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,
אשר חרפו אויביך יהוה אשר חרפו עקבות משיחך׃ | 51 |
dhihaka ambazo kwazo adui zako wamenisimanga, Ee Bwana, ambazo kwazo wamesimanga kila hatua ya mpakwa mafuta wako.
ברוך יהוה לעולם אמן ואמן׃ | 52 |
Msifuni Bwana milele!