< תהילים 87 >

לבני קרח מזמור שיר יסודתו בהררי קדש׃ 1
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
אהב יהוה שערי ציון מכל משכנות יעקב׃ 2
Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.
נכבדות מדבר בך עיר האלהים סלה׃ 3
Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:
אזכיר רהב ובבל לידעי הנה פלשת וצור עם כוש זה ילד שם׃ 4
“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’”
ולציון יאמר איש ואיש ילד בה והוא יכוננה עליון׃ 5
Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”
יהוה יספר בכתוב עמים זה ילד שם סלה׃ 6
Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”
ושרים כחללים כל מעיני בך׃ 7
Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

< תהילים 87 >