< תהילים 6 >

למנצח בנגינות על השמינית מזמור לדוד יהוה אל באפך תוכיחני ואל בחמתך תיסרני׃ 1
Yahweh, usinikemee ukiwa na hasira au usiniadhibu katika gadhabu yako.
חנני יהוה כי אמלל אני רפאני יהוה כי נבהלו עצמי׃ 2
Unihurumie, Yahwe, kwa maana ni dhaifu; uniponye, Yahweh, kwa kuwa mifupa yangu ina tikisika.
ונפשי נבהלה מאד ואת יהוה עד מתי׃ 3
Moyo wangu pia umesumbuka sana. Lakini wewe, Yahweh, mpaka lini hali hii itaendelea?
שובה יהוה חלצה נפשי הושיעני למען חסדך׃ 4
Rudi, Yahweh! uniokoe. Uniokoe kwa sababu ya uaminifu wa agano lako!
כי אין במות זכרך בשאול מי יודה לך׃ (Sheol h7585) 5
kwa kuwa kifoni hakuna kumbukumbu lako. Kuzimuni ni nani atakaye kushukuru? (Sheol h7585)
יגעתי באנחתי אשחה בכל לילה מטתי בדמעתי ערשי אמסה׃ 6
Nimechoshwa na kuugua kwangu. Ninalowanisha kitanda changu kwa machozi usiku kucha; ninaosha kiti changu kwa machozi.
עששה מכעס עיני עתקה בכל צוררי׃ 7
Macho yangu yanafifia kwa kulia sana; yanazidi kuwa dhaifu kwa sababu ya adaui zangu.
סורו ממני כל פעלי און כי שמע יהוה קול בכיי׃ 8
Ondokeni kwangu, nyote mtendao maovu; kwa kuwa Yahweh amesikia sauti ya kilio changu.
שמע יהוה תחנתי יהוה תפלתי יקח׃ 9
Yahweh amesikia malalamiko yangu kwa ajili ya huruma; Yahweh ameyapokea maombi yangu.
יבשו ויבהלו מאד כל איבי ישבו יבשו רגע׃ 10
Maadui zangu wote wataaibishwa na kuteswa sana. Watarudi nyuma na ghafra kufedheheshwa.

< תהילים 6 >