< תהילים 55 >

למנצח בנגינת משכיל לדוד האזינה אלהים תפלתי ואל תתעלם מתחנתי׃ 1
Uyategee sikio maombi yangu, Mungu; nawe usijifiche mbali na kusihi kwangu.
הקשיבה לי וענני אריד בשיחי ואהימה׃ 2
Unitazame kwa makini na unijibu; Sina pumziko katika shida zangu
מקול אויב מפני עקת רשע כי ימיטו עלי און ובאף ישטמוני׃ 3
kwa sababu ya sauti ya adui zangu, kwa sababu ya ukandamizaji wa waovu; maana wananiletea matatizo na kunitesa wakiwa na hasira.
לבי יחיל בקרבי ואימות מות נפלו עלי׃ 4
Moyo wangu wasumbuka ndani yangu, na hofu ya kifo imeniangukia.
יראה ורעד יבא בי ותכסני פלצות׃ 5
Uwoga na kutetemeka kumenijia, nayo hofu imenielemea.
ואמר מי יתן לי אבר כיונה אעופה ואשכנה׃ 6
Nikasema, “Oh, kama tu ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningelipaa mbali na kupata pumziko.
הנה ארחיק נדד אלין במדבר סלה׃ 7
Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. (Selah)
אחישה מפלט לי מרוח סעה מסער׃ 8
Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani.”
בלע אדני פלג לשונם כי ראיתי חמס וריב בעיר׃ 9
Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
יומם ולילה יסובבה על חומתיה ואון ועמל בקרבה׃ 10
Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.
הוות בקרבה ולא ימיש מרחבה תך ומרמה׃ 11
Uovu uko katikati yake; ukandamizaji na uongo hauiachi mitaa yake.
כי לא אויב יחרפני ואשא לא משנאי עלי הגדיל ואסתר ממנו׃ 12
Kwa maana hakuwa adui aliye nikemea, hivyo ningevumilia; wala ingekuwa ni yule aliye nichukia aliyejiinua mwenyewe dhidi yagu, hivyo ningejificha asinione.
ואתה אנוש כערכי אלופי ומידעי׃ 13
Lakini ulikuwa wewe, mtu sawa na mimi, mwenzangu na rafiki yangu.
אשר יחדו נמתיק סוד בבית אלהים נהלך ברגש׃ 14
Tulikuwa na ushirika mtamu pamoja; tuliingia katika nyumba ya Mungu tukiwa na umati mkubwa.
ישימות עלימו ירדו שאול חיים כי רעות במגורם בקרבם׃ (Sheol h7585) 15
Kifo na kiwapate ghafla; na washuke wakiwa hai kuzimuni, maana ndiko waishiko waovu, hapo hapo kati yao. (Sheol h7585)
אני אל אלהים אקרא ויהוה יושיעני׃ 16
Lakini kwangu mimi, nitamwita Mungu, na Yahwe ataniokoa.
ערב ובקר וצהרים אשיחה ואהמה וישמע קולי׃ 17
Wakati wa jioni, asubuhi na mchana ninalalamika na kuomboleza; yeye atasikia sauti yangu.
פדה בשלום נפשי מקרב לי כי ברבים היו עמדי׃ 18
Kwa usalama kabisa atayaokoa maisha yangu na vita dhidi yangu, kwa maana wale waliopigana nami walikuwa ni wengi.
ישמע אל ויענם וישב קדם סלה אשר אין חליפות למו ולא יראו אלהים׃ 19
Mungu, yule unayetawala milele, atawasikia na kuwaaibisha wao. (Selah) Hawabadiliki, na hawamhofu Mungu.
שלח ידיו בשלמיו חלל בריתו׃ 20
Rafiki yangu ameinua mikono yake dhidi ya wale waliokuwa na amani naye; Hakuheshimu agano alilokuwa nalo.
חלקו מחמאת פיו וקרב לבו רכו דבריו משמן והמה פתחות׃ 21
Mdomo wake ulikuwa laini kama siagi, lakini moyo wake ulikuwa adui; maneno yake yalikuwa laini kuliko mafuta, lakini yalikuwa ni panga zilizochomolewa.
השלך על יהוה יהבך והוא יכלכלך לא יתן לעולם מוט לצדיק׃ 22
Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.
ואתה אלהים תורדם לבאר שחת אנשי דמים ומרמה לא יחצו ימיהם ואני אבטח בך׃ 23
Bali wewe, Mungu, utawaleta waovu chini kwenye shimo la uharibifu; watu wenye kiu ya kumwaga damu na waongo hawataishi hata nusu ya maisha kama wengine, lakini mimi nitakuamini wewe.

< תהילים 55 >