< תהילים 48 >
שיר מזמור לבני קרח גדול יהוה ומהלל מאד בעיר אלהינו הר קדשו׃ | 1 |
Yahwe ndiye aliye mkuu na mwenyekusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu kwenye mlima wake mtakatifu.
יפה נוף משוש כל הארץ הר ציון ירכתי צפון קרית מלך רב׃ | 2 |
Ni mzuri katika mwinuko wake, furaha ya nchi yote, ni mlima Sayuni, kwenye upande wa kaskazini, mji wa Mfalme mkuu.
אלהים בארמנותיה נודע למשגב׃ | 3 |
Mungu amejifunua mwenyewe katika jumba lake la kifahari kama kimbilio la usalama.
כי הנה המלכים נועדו עברו יחדו׃ | 4 |
Maana, tazama, wafalme walikusanyika wenyewe; wote pamoja walipita.
המה ראו כן תמהו נבהלו נחפזו׃ | 5 |
Nao waliuona, wakashangaa; walifadhaika, na wakaharakisha kuondoka.
רעדה אחזתם שם חיל כיולדה׃ | 6 |
Pale pale tetemeko liliwashikilia, maumivu makali kama mwanamke anaye zaa.
ברוח קדים תשבר אניות תרשיש׃ | 7 |
Kwa upepo wa mashariki wewe huivunja meli ya Tarshishi.
כאשר שמענו כן ראינו בעיר יהוה צבאות בעיר אלהינו אלהים יכוננה עד עולם סלה׃ | 8 |
Kama tulivyo sikia, vivyo hivyo tumeona katika mji wa Yahwe wa majeshi, katika mji wa Mungu wetu; Mungu atautunza milele. (Selah)
דמינו אלהים חסדך בקרב היכלך׃ | 9 |
Tumeutafakari uaminifu wa agano lako, Mungu, katikati ya hekalu lako.
כשמך אלהים כן תהלתך על קצוי ארץ צדק מלאה ימינך׃ | 10 |
Kama lilivyo jina lako, Mungu, hivyo ndivyo zilivyo sifa zako mpaka miisho ya dunia; mkono wako wa kuume umejaa haki.
ישמח הר ציון תגלנה בנות יהודה למען משפטיך׃ | 11 |
Milma Sayuni na ufurahi, nao wana wa Yuda washangilie kwa sababu ya amri ya haki yako.
סבו ציון והקיפוה ספרו מגדליה׃ | 12 |
Tembeeni katika Mlima Sayuni, muuzungukie mji,
שיתו לבכם לחילה פסגו ארמנותיה למען תספרו לדור אחרון׃ | 13 |
mzitazame kwa makini nguzo zake, na mtazame majumba yake ya kifahari ili kwamba muweze kuwasimulia kizazi kijacho.
כי זה אלהים אלהינו עולם ועד הוא ינהגנו על מות׃ | 14 |
Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; naye atakuwa kiongozi wetu mpaka kufa.