< תהילים 21 >
למנצח מזמור לדוד יהוה בעזך ישמח מלך ובישועתך מה יגיל מאד׃ | 1 |
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa!
תאות לבו נתתה לו וארשת שפתיו בל מנעת סלה׃ | 2 |
Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake.
כי תקדמנו ברכות טוב תשית לראשו עטרת פז׃ | 3 |
Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
חיים שאל ממך נתתה לו ארך ימים עולם ועד׃ | 4 |
Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele.
גדול כבודו בישועתך הוד והדר תשוה עליו׃ | 5 |
Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu.
כי תשיתהו ברכות לעד תחדהו בשמחה את פניך׃ | 6 |
Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako.
כי המלך בטח ביהוה ובחסד עליון בל ימוט׃ | 7 |
Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.
תמצא ידך לכל איביך ימינך תמצא שנאיך׃ | 8 |
Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.
תשיתמו כתנור אש לעת פניך יהוה באפו יבלעם ותאכלם אש׃ | 9 |
Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza.
פרימו מארץ תאבד וזרעם מבני אדם׃ | 10 |
Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu.
כי נטו עליך רעה חשבו מזמה בל יוכלו׃ | 11 |
Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,
כי תשיתמו שכם במיתריך תכונן על פניהם׃ | 12 |
kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.
רומה יהוה בעזך נשירה ונזמרה גבורתך׃ | 13 |
Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako.