< תהילים 2 >

למה רגשו גוים ולאמים יהגו ריק׃ 1
Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure?
יתיצבו מלכי ארץ ורוזנים נוסדו יחד על יהוה ועל משיחו׃ 2
Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
ננתקה את מוסרותימו ונשליכה ממנו עבתימו׃ 3
Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
יושב בשמים ישחק אדני ילעג למו׃ 4
Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
אז ידבר אלימו באפו ובחרונו יבהלמו׃ 5
Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
ואני נסכתי מלכי על ציון הר קדשי׃ 6
“Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
אספרה אל חק יהוה אמר אלי בני אתה אני היום ילדתיך׃ 7
Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa.
שאל ממני ואתנה גוים נחלתך ואחזתך אפסי ארץ׃ 8
Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako.
תרעם בשבט ברזל ככלי יוצר תנפצם׃ 9
Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”
ועתה מלכים השכילו הוסרו שפטי ארץ׃ 10
Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia.
עבדו את יהוה ביראה וגילו ברעדה׃ 11
Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka.
נשקו בר פן יאנף ותאבדו דרך כי יבער כמעט אפו אשרי כל חוסי בו׃ 12
Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.

< תהילים 2 >