< תהילים 132 >

שיר המעלות זכור יהוה לדוד את כל ענותו׃ 1
Wimbo wa kwenda juu. Ee Bwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili.
אשר נשבע ליהוה נדר לאביר יעקב׃ 2
Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:
אם אבא באהל ביתי אם אעלה על ערש יצועי׃ 3
“Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu:
אם אתן שנת לעיני לעפעפי תנומה׃ 4
sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia,
עד אמצא מקום ליהוה משכנות לאביר יעקב׃ 5
mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
הנה שמענוה באפרתה מצאנוה בשדי יער׃ 6
Tulisikia habari hii huko Efrathi, tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara:
נבואה למשכנותיו נשתחוה להדם רגליו׃ 7
“Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;
קומה יהוה למנוחתך אתה וארון עזך׃ 8
inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako.
כהניך ילבשו צדק וחסידיך ירננו׃ 9
Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”
בעבור דוד עבדך אל תשב פני משיחך׃ 10
Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako.
נשבע יהוה לדוד אמת לא ישוב ממנה מפרי בטנך אשית לכסא לך׃ 11
Bwana alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe katika kiti chako cha enzi,
אם ישמרו בניך בריתי ועדתי זו אלמדם גם בניהם עדי עד ישבו לכסא לך׃ 12
kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.”
כי בחר יהוה בציון אוה למושב לו׃ 13
Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake:
זאת מנוחתי עדי עד פה אשב כי אותיה׃ 14
“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku:
צידה ברך אברך אביוניה אשביע לחם׃ 15
Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula.
וכהניה אלביש ישע וחסידיה רנן ירננו׃ 16
Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.
שם אצמיח קרן לדוד ערכתי נר למשיחי׃ 17
“Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu.
אויביו אלביש בשת ועליו יציץ נזרו׃ 18
Adui zake nitawavika aibu, bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”

< תהילים 132 >