< תהילים 126 >
שיר המעלות בשוב יהוה את שיבת ציון היינו כחלמים׃ | 1 |
Bwana alipowarejesha mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto.
אז ימלא שחוק פינו ולשוננו רנה אז יאמרו בגוים הגדיל יהוה לעשות עם אלה׃ | 2 |
Vinywa vyetu vilijawa na vicheko na ndimi zetu zilijawa na kuimba. Kisha wakasema kati ya mataifa, “Yahwe amewatendea mambo makuu.”
הגדיל יהוה לעשות עמנו היינו שמחים׃ | 3 |
Yahwe alitufanyia mambo makuu; ni furaha gani tuliyokuwa nayo!
שובה יהוה את שבותנו כאפיקים בנגב׃ | 4 |
Ee Yahwe, uwarejeshe mateka wetu, kama vijito vya kusini.
הזרעים בדמעה ברנה יקצרו׃ | 5 |
Wale wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.
הלוך ילך ובכה נשא משך הזרע בא יבוא ברנה נשא אלמתיו׃ | 6 |
Yeye aendaye akilia, akibeba mbegu kwa ajili a kupanda, atarudi tena kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.