< תהילים 107 >

הדו ליהוה כי טוב כי לעולם חסדו׃ 1
Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele.
יאמרו גאולי יהוה אשר גאלם מיד צר׃ 2
Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui,
ומארצות קבצם ממזרח וממערב מצפון ומים׃ 3
wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini.
תעו במדבר בישימון דרך עיר מושב לא מצאו׃ 4
Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi.
רעבים גם צמאים נפשם בהם תתעטף׃ 5
Walikuwa na njaa na kiu, nafsi zao zikadhoofika.
ויצעקו אל יהוה בצר להם ממצוקותיהם יצילם׃ 6
Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.
וידריכם בדרך ישרה ללכת אל עיר מושב׃ 7
Akawaongoza kwa njia iliyo sawa hadi mji ambao wangeweza kuishi.
יודו ליהוה חסדו ונפלאותיו לבני אדם׃ 8
Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,
כי השביע נפש שקקה ונפש רעבה מלא טוב׃ 9
kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.
ישבי חשך וצלמות אסירי עני וברזל׃ 10
Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, wafungwa wakiteseka katika minyororo,
כי המרו אמרי אל ועצת עליון נאצו׃ 11
kwa sababu walikuwa wameasi dhidi ya maneno ya Mungu na kudharau shauri la Aliye Juu Sana.
ויכנע בעמל לבם כשלו ואין עזר׃ 12
Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.
ויזעקו אל יהוה בצר להם ממצקותיהם יושיעם׃ 13
Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.
יוציאם מחשך וצלמות ומוסרותיהם ינתק׃ 14
Akawatoa katika giza na huzuni kuu na akavunja minyororo yao.
יודו ליהוה חסדו ונפלאותיו לבני אדם׃ 15
Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,
כי שבר דלתות נחשת ובריחי ברזל גדע׃ 16
kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma.
אולים מדרך פשעם ומעונתיהם יתענו׃ 17
Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao, wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao.
כל אכל תתעב נפשם ויגיעו עד שערי מות׃ 18
Wakachukia kabisa vyakula vyote, wakakaribia malango ya mauti.
ויזעקו אל יהוה בצר להם ממצקותיהם יושיעם׃ 19
Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.
ישלח דברו וירפאם וימלט משחיתותם׃ 20
Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo yao.
יודו ליהוה חסדו ונפלאותיו לבני אדם׃ 21
Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.
ויזבחו זבחי תודה ויספרו מעשיו ברנה׃ 22
Na watoe dhabihu za kushukuru, na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.
יורדי הים באניות עשי מלאכה במים רבים׃ 23
Wengine walisafiri baharini kwa meli, walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.
המה ראו מעשי יהוה ונפלאותיו במצולה׃ 24
Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini.
ויאמר ויעמד רוח סערה ותרומם גליו׃ 25
Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu.
יעלו שמים ירדו תהומות נפשם ברעה תתמוגג׃ 26
Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.
יחוגו וינועו כשכור וכל חכמתם תתבלע׃ 27
Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo.
ויצעקו אל יהוה בצר להם וממצוקתיהם יוציאם׃ 28
Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao.
יקם סערה לדממה ויחשו גליהם׃ 29
Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia.
וישמחו כי ישתקו וינחם אל מחוז חפצם׃ 30
Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.
יודו ליהוה חסדו ונפלאותיו לבני אדם׃ 31
Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.
וירממוהו בקהל עם ובמושב זקנים יהללוהו׃ 32
Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee.
ישם נהרות למדבר ומצאי מים לצמאון׃ 33
Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu,
ארץ פרי למלחה מרעת ישבי בה׃ 34
nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa, kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo.
ישם מדבר לאגם מים וארץ ציה למצאי מים׃ 35
Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji, nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo;
ויושב שם רעבים ויכוננו עיר מושב׃ 36
aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, nao wakajenga mji wangeweza kuishi.
ויזרעו שדות ויטעו כרמים ויעשו פרי תבואה׃ 37
Walilima mashamba na kupanda mizabibu, nayo ikazaa matunda mengi,
ויברכם וירבו מאד ובהמתם לא ימעיט׃ 38
Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana, wala hakuruhusu mifugo yao kupungua.
וימעטו וישחו מעצר רעה ויגון׃ 39
Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa kwa kuonewa, maafa na huzuni.
שפך בוז על נדיבים ויתעם בתהו לא דרך׃ 40
Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu, aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia.
וישגב אביון מעוני וישם כצאן משפחות׃ 41
Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao, na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo.
יראו ישרים וישמחו וכל עולה קפצה פיה׃ 42
Wanyofu wataona na kufurahi, lakini waovu wote watafunga vinywa vyao.
מי חכם וישמר אלה ויתבוננו חסדי יהוה׃ 43
Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya, na atafakari upendo mkuu wa Bwana.

< תהילים 107 >