< מִשְׁלֵי 18 >

לתאוה יבקש נפרד בכל תושיה יתגלע׃ 1
Mtu ajitengaye na wengine hufuata matakwa yake mwenyewe; hupiga vita kila shauri jema.
לא יחפץ כסיל בתבונה כי אם בהתגלות לבו׃ 2
Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe.
בבוא רשע בא גם בוז ועם קלון חרפה׃ 3
Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia, pamoja na aibu huja lawama.
מים עמקים דברי פי איש נחל נבע מקור חכמה׃ 4
Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji, bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.
שאת פני רשע לא טוב להטות צדיק במשפט׃ 5
Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu, au kumnyima haki asiye na hatia.
שפתי כסיל יבאו בריב ופיו למהלמות יקרא׃ 6
Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo.
פי כסיל מחתה לו ושפתיו מוקש נפשו׃ 7
Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.
דברי נרגן כמתלהמים והם ירדו חדרי בטן׃ 8
Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu.
גם מתרפה במלאכתו אח הוא לבעל משחית׃ 9
Mtu aliye mlegevu katika kazi yake ni ndugu na yule anayeharibu.
מגדל עז שם יהוה בו ירוץ צדיק ונשגב׃ 10
Jina la Bwana ni ngome imara, wenye haki huikimbilia na kuwa salama.
הון עשיר קרית עזו וכחומה נשגבה במשכיתו׃ 11
Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.
לפני שבר יגבה לב איש ולפני כבוד ענוה׃ 12
Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.
משיב דבר בטרם ישמע אולת היא לו וכלמה׃ 13
Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza, huo ni upumbavu wake na aibu yake.
רוח איש יכלכל מחלהו ורוח נכאה מי ישאנה׃ 14
Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?
לב נבון יקנה דעת ואזן חכמים תבקש דעת׃ 15
Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.
מתן אדם ירחיב לו ולפני גדלים ינחנו׃ 16
Zawadi humfungulia njia mtoaji, nayo humleta mbele ya wakuu.
צדיק הראשון בריבו יבא רעהו וחקרו׃ 17
Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi, hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali.
מדינים ישבית הגורל ובין עצומים יפריד׃ 18
Kupiga kura hukomesha mashindano na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.
אח נפשע מקרית עז ומדונים כבריח ארמון׃ 19
Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika kuliko mji uliozungushiwa ngome, nayo mabishano ni kama malango ya ngome yenye makomeo.
מפרי פי איש תשבע בטנו תבואת שפתיו ישבע׃ 20
Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake, atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.
מות וחיים ביד לשון ואהביה יאכל פריה׃ 21
Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.
מצא אשה מצא טוב ויפק רצון מיהוה׃ 22
Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa Bwana.
תחנונים ידבר רש ועשיר יענה עזות׃ 23
Mtu maskini huomba kuhurumiwa bali tajiri hujibu kwa ukali.
איש רעים להתרעע ויש אהב דבק מאח׃ 24
Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu, bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.

< מִשְׁלֵי 18 >