< מִשְׁלֵי 16 >

לאדם מערכי לב ומיהוה מענה לשון׃ 1
Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.
כל דרכי איש זך בעיניו ותכן רוחות יהוה׃ 2
Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na Bwana.
גל אל יהוה מעשיך ויכנו מחשבתיך׃ 3
Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa.
כל פעל יהוה למענהו וגם רשע ליום רעה׃ 4
Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi.
תועבת יהוה כל גבה לב יד ליד לא ינקה׃ 5
Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.
בחסד ואמת יכפר עון וביראת יהוה סור מרע׃ 6
Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.
ברצות יהוה דרכי איש גם אויביו ישלם אתו׃ 7
Njia za mtu zinapompendeza Bwana, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.
טוב מעט בצדקה מרב תבואות בלא משפט׃ 8
Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
לב אדם יחשב דרכו ויהוה יכין צעדו׃ 9
Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.
קסם על שפתי מלך במשפט לא ימעל פיו׃ 10
Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, wala kinywa chake hakipotoshi haki.
פלס ומאזני משפט ליהוה מעשהו כל אבני כיס׃ 11
Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.
תועבת מלכים עשות רשע כי בצדקה יכון כסא׃ 12
Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki.
רצון מלכים שפתי צדק ודבר ישרים יאהב׃ 13
Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu; humthamini mtu asemaye kweli.
חמת מלך מלאכי מות ואיש חכם יכפרנה׃ 14
Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti, bali mtu mwenye hekima ataituliza.
באור פני מלך חיים ורצונו כעב מלקוש׃ 15
Uso wa mfalme ungʼaapo, inamaanisha uhai; upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli.
קנה חכמה מה טוב מחרוץ וקנות בינה נבחר מכסף׃ 16
Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha!
מסלת ישרים סור מרע שמר נפשו נצר דרכו׃ 17
Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.
לפני שבר גאון ולפני כשלון גבה רוח׃ 18
Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko.
טוב שפל רוח את עניים מחלק שלל את גאים׃ 19
Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho miongoni mwa walioonewa kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.
משכיל על דבר ימצא טוב ובוטח ביהוה אשריו׃ 20
Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana.
לחכם לב יקרא נבון ומתק שפתים יסיף לקח׃ 21
Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu, na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho.
מקור חיים שכל בעליו ומוסר אולים אולת׃ 22
Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao, bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu.
לב חכם ישכיל פיהו ועל שפתיו יסיף לקח׃ 23
Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho.
צוף דבש אמרי נעם מתוק לנפש ומרפא לעצם׃ 24
Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.
יש דרך ישר לפני איש ואחריתה דרכי מות׃ 25
Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.
נפש עמל עמלה לו כי אכף עליו פיהו׃ 26
Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi; njaa yake humsukuma aendelee.
איש בליעל כרה רעה ועל שפתיו כאש צרבת׃ 27
Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya, maneno yake ni kama moto uunguzao.
איש תהפכות ישלח מדון ונרגן מפריד אלוף׃ 28
Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.
איש חמס יפתה רעהו והוליכו בדרך לא טוב׃ 29
Mtu mkali humvuta jirani yake na kumwongoza katika mapito yale mabaya.
עצה עיניו לחשב תהפכות קרץ שפתיו כלה רעה׃ 30
Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu; naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.
עטרת תפארת שיבה בדרך צדקה תמצא׃ 31
Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu.
טוב ארך אפים מגבור ומשל ברוחו מלכד עיר׃ 32
Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.
בחיק יוטל את הגורל ומיהוה כל משפטו׃ 33
Kura hupigwa kwa siri, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.

< מִשְׁלֵי 16 >