< מִשְׁלֵי 12 >
אהב מוסר אהב דעת ושנא תוכחת בער׃ | 1 |
Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa, bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.
טוב יפיק רצון מיהוה ואיש מזמות ירשיע׃ | 2 |
Mtu mwema hupata kibali kutoka kwa Bwana, bali Bwana humhukumu mwenye hila.
לא יכון אדם ברשע ושרש צדיקים בל ימוט׃ | 3 |
Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa.
אשת חיל עטרת בעלה וכרקב בעצמותיו מבישה׃ | 4 |
Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.
מחשבות צדיקים משפט תחבלות רשעים מרמה׃ | 5 |
Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.
דברי רשעים ארב דם ופי ישרים יצילם׃ | 6 |
Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa.
הפוך רשעים ואינם ובית צדיקים יעמד׃ | 7 |
Watu waovu huondolewa na kutoweka, bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.
לפי שכלו יהלל איש ונעוה לב יהיה לבוז׃ | 8 |
Mtu husifiwa kulingana na hekima yake, bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa.
טוב נקלה ועבד לו ממתכבד וחסר לחם׃ | 9 |
Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi, kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.
יודע צדיק נפש בהמתו ורחמי רשעים אכזרי׃ | 10 |
Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake, bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili.
עבד אדמתו ישבע לחם ומרדף ריקים חסר לב׃ | 11 |
Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.
חמד רשע מצוד רעים ושרש צדיקים יתן׃ | 12 |
Waovu hutamani mateka ya watu wabaya, bali shina la mwenye haki hustawi.
בפשע שפתים מוקש רע ויצא מצרה צדיק׃ | 13 |
Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi, bali mwenye haki huepuka taabu.
מפרי פי איש ישבע טוב וגמול ידי אדם ישוב לו׃ | 14 |
Kutokana na tunda la midomo yake mtu hujazwa na mambo mema, hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza.
דרך אויל ישר בעיניו ושמע לעצה חכם׃ | 15 |
Njia ya mpumbavu huonekana sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri.
אויל ביום יודע כעסו וכסה קלון ערום׃ | 16 |
Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja, bali mtu wa busara hupuuza matukano.
יפיח אמונה יגיד צדק ועד שקרים מרמה׃ | 17 |
Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika, bali shahidi wa uongo husema uongo.
יש בוטה כמדקרות חרב ולשון חכמים מרפא׃ | 18 |
Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.
שפת אמת תכון לעד ועד ארגיעה לשון שקר׃ | 19 |
Midomo isemayo kweli hudumu milele, bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.
מרמה בלב חרשי רע וליעצי שלום שמחה׃ | 20 |
Upo udanganyifu katika mioyo ya wale ambao hupanga mabaya, bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.
לא יאנה לצדיק כל און ורשעים מלאו רע׃ | 21 |
Hakuna dhara linalompata mwenye haki, bali waovu wana taabu nyingi.
תועבת יהוה שפתי שקר ועשי אמונה רצונו׃ | 22 |
Bwana anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
אדם ערום כסה דעת ולב כסילים יקרא אולת׃ | 23 |
Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe, bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.
יד חרוצים תמשול ורמיה תהיה למס׃ | 24 |
Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.
דאגה בלב איש ישחנה ודבר טוב ישמחנה׃ | 25 |
Moyo wa wasiwasi humlemea mtu, bali neno la huruma humfurahisha.
יתר מרעהו צדיק ודרך רשעים תתעם׃ | 26 |
Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki, bali njia ya waovu huwapotosha.
לא יחרך רמיה צידו והון אדם יקר חרוץ׃ | 27 |
Mtu mvivu haoki mawindo yake, bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.
בארח צדקה חיים ודרך נתיבה אל מות׃ | 28 |
Katika njia ya haki kuna uzima; katika mapito hayo kuna maisha ya milele.