< ויקרא 2 >
ונפש כי תקריב קרבן מנחה ליהוה סלת יהיה קרבנו ויצק עליה שמן ונתן עליה לבנה׃ | 1 |
Yeyote akitoa sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake lazima iwe unga safi, na atamwaga mafuta juu yake na kuweka ubani juu yake.
והביאה אל בני אהרן הכהנים וקמץ משם מלא קמצו מסלתה ומשמנה על כל לבנתה והקטיר הכהן את אזכרתה המזבחה אשה ריח ניחח ליהוה׃ | 2 |
Atachukua sadaka kwa wana wa Haruni, makuhani na pale kuhani atachukua konzi moja ya unga safi pamoja na mafuta na ubani. Kisha kuhani atateketeza hiyo sadaka juu ya madhabahu kuwa shukrani kwa uzuri wa Bwana. Italeta harufu nzuri sana kwa Bwana, itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
והנותרת מן המנחה לאהרן ולבניו קדש קדשים מאשי יהוה׃ | 3 |
Unga wowote uliobaki utakuwa ni wa Haruni na watoto wake. Ni takatifu sana kwa Bwana iliyotolewa sadaka kwa Bwana kwa moto.
וכי תקרב קרבן מנחה מאפה תנור סלת חלות מצת בלולת בשמן ורקיקי מצות משחים בשמן׃ | 4 |
Kisha utakapotoa sadaka ya unga bila chachu iliyookwa kweye kiokeo, itakuwa mkate lainiya unga safi uliochanganywa na mafuta, au mkate mgumu usiokuwa na chachu, ambao umesambazwa na mafuta.
ואם מנחה על המחבת קרבנך סלת בלולה בשמן מצה תהיה׃ | 5 |
Kama matoleo yako ya nafaka yameokwa na kikaango cha chuma ni lazima iwe unga safi bila chachu uliochanganywa na mafuta.
פתות אתה פתים ויצקת עליה שמן מנחה הוא׃ | 6 |
Utagawanya katika vipande na kumwaga mafuta juu yake. Hii ni sadaka ya nafaka.
ואם מנחת מרחשת קרבנך סלת בשמן תעשה׃ | 7 |
Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa katika kikaango, ni lazima iwe imetengenezwa kwa unga safi na mafuta.
והבאת את המנחה אשר יעשה מאלה ליהוה והקריבה אל הכהן והגישה אל המזבח׃ | 8 |
Utaleta matoleo ya nafaka yaliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana, italeta kwa kuhani, ambaye ataleta mbele ya madhabahu.
והרים הכהן מן המנחה את אזכרתה והקטיר המזבחה אשה ריח ניחח ליהוה׃ | 9 |
Ndipo kuhani atachukua baadhi ya sadaka ya nafaka ya shukrani ya Bwana, ataitekeza katika madhabahu. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, italeta harufu nzuri kwa Bwana.
והנותרת מן המנחה לאהרן ולבניו קדש קדשים מאשי יהוה׃ | 10 |
Itakayobaki sadaka ya nafaka itakuwa ya Haruni na wanawe. Itakuwa takatifu kamili ya Bwana kutoka matoleo kwa Bwana yatolewayo kwa moto.
כל המנחה אשר תקריבו ליהוה לא תעשה חמץ כי כל שאר וכל דבש לא תקטירו ממנו אשה ליהוה׃ | 11 |
Sadaka ya nafaka itolewayo kwa Bwana isiwe na chachu, hautatekeza chachu wala asali kama matoleo yatakayotekezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana.
קרבן ראשית תקריבו אתם ליהוה ואל המזבח לא יעלו לריח ניחח׃ | 12 |
Utayatoa kwa Bwana kama mazao ya kwanza, lakini hayatatumika kama matoleo ya harufu nzuri ya moto juu ya madhabahu.
וכל קרבן מנחתך במלח תמלח ולא תשבית מלח ברית אלהיך מעל מנחתך על כל קרבנך תקריב מלח׃ | 13 |
Utaweka chumvi katika kila matoleo yako ya nafaka. Usipungukie chumvi ya agano la Bwana katika matoleo yako ya unga. Matoleo yako yote hayatapungukiwa na chumvi.
ואם תקריב מנחת בכורים ליהוה אביב קלוי באש גרש כרמל תקריב את מנחת בכוריך׃ | 14 |
Kama ukitoa matoleo ya nafaka ya mazao ya kwanza kwa Bwana, utatoa nafaka mbichi yaliyookwa kwa moto, na yaliyopondwa.
ונתת עליה שמן ושמת עליה לבנה מנחה הוא׃ | 15 |
Lazima utaweka mafuta na ubani juu yake. Haya ni matoleo ya nafaka.
והקטיר הכהן את אזכרתה מגרשה ומשמנה על כל לבנתה אשה ליהוה׃ | 16 |
Kuhani atatoa sehemu ya nafaka iliyopondwa na mafuta na ubani, kama sadaka ya shukrani itolewayo kwa uzuri wa Bwana. Hii ni sadaka ya Bwana inayotolewa kwa moto.