< ויקרא 18 >
וידבר יהוה אל משה לאמר׃ | 1 |
Bwana akamwambia Mose,
דבר אל בני ישראל ואמרת אלהם אני יהוה אלהיכם׃ | 2 |
“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
כמעשה ארץ מצרים אשר ישבתם בה לא תעשו וכמעשה ארץ כנען אשר אני מביא אתכם שמה לא תעשו ובחקתיהם לא תלכו׃ | 3 |
Msifanye kama wafanyavyo huko Misri, mahali mlipokuwa mnaishi, wala msifanye kama wanavyofanya katika nchi ya Kanaani, mahali ninapowapeleka. Msifuate matendo yao.
את משפטי תעשו ואת חקתי תשמרו ללכת בהם אני יהוה אלהיכם׃ | 4 |
Ni lazima mzitii sheria zangu, na mwe waangalifu kuzifuata amri zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
ושמרתם את חקתי ואת משפטי אשר יעשה אתם האדם וחי בהם אני יהוה׃ | 5 |
Zishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi Bwana.
איש איש אל כל שאר בשרו לא תקרבו לגלות ערוה אני יהוה׃ | 6 |
“‘Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Bwana.
ערות אביך וערות אמך לא תגלה אמך הוא לא תגלה ערותה׃ | 7 |
“‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye.
ערות אשת אביך לא תגלה ערות אביך הוא׃ | 8 |
“‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako.
ערות אחותך בת אביך או בת אמך מולדת בית או מולדת חוץ לא תגלה ערותן׃ | 9 |
“‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.
ערות בת בנך או בת בתך לא תגלה ערותן כי ערותך הנה׃ | 10 |
“‘Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako; utajivunjia heshima.
ערות בת אשת אביך מולדת אביך אחותך הוא לא תגלה ערותה׃ | 11 |
“‘Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako.
ערות אחות אביך לא תגלה שאר אביך הוא׃ | 12 |
“‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako.
ערות אחות אמך לא תגלה כי שאר אמך הוא׃ | 13 |
“‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu.
ערות אחי אביך לא תגלה אל אשתו לא תקרב דדתך הוא׃ | 14 |
“‘Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako.
ערות כלתך לא תגלה אשת בנך הוא לא תגלה ערותה׃ | 15 |
“‘Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye.
ערות אשת אחיך לא תגלה ערות אחיך הוא׃ | 16 |
“‘Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako.
ערות אשה ובתה לא תגלה את בת בנה ואת בת בתה לא תקח לגלות ערותה שארה הנה זמה הוא׃ | 17 |
“‘Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti wa mwanawe au binti wa binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu.
ואשה אל אחתה לא תקח לצרר לגלות ערותה עליה בחייה׃ | 18 |
“‘Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza, na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi.
ואל אשה בנדת טמאתה לא תקרב לגלות ערותה׃ | 19 |
“‘Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi.
ואל אשת עמיתך לא תתן שכבתך לזרע לטמאה בה׃ | 20 |
“‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.
ומזרעך לא תתן להעביר למלך ולא תחלל את שם אלהיך אני יהוה׃ | 21 |
“‘Usimtoe mtoto wako yeyote awe kafara kwa mungu Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.
ואת זכר לא תשכב משכבי אשה תועבה הוא׃ | 22 |
“‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo.
ובכל בהמה לא תתן שכבתך לטמאה בה ואשה לא תעמד לפני בהמה לרבעה תבל הוא׃ | 23 |
“‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.
אל תטמאו בכל אלה כי בכל אלה נטמאו הגוים אשר אני משלח מפניכם׃ | 24 |
“‘Msijitie unajisi kwa njia yoyote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi.
ותטמא הארץ ואפקד עונה עליה ותקא הארץ את ישביה׃ | 25 |
Hata nchi ilitiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake, nayo nchi ikawatapika wakazi wake.
ושמרתם אתם את חקתי ואת משפטי ולא תעשו מכל התועבת האלה האזרח והגר הגר בתוככם׃ | 26 |
Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzawa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya,
כי את כל התועבת האל עשו אנשי הארץ אשר לפניכם ותטמא הארץ׃ | 27 |
kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu, na nchi ikawa najisi.
ולא תקיא הארץ אתכם בטמאכם אתה כאשר קאה את הגוי אשר לפניכם׃ | 28 |
Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia.
כי כל אשר יעשה מכל התועבות האלה ונכרתו הנפשות העשת מקרב עמם׃ | 29 |
“‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao.
ושמרתם את משמרתי לבלתי עשות מחקות התועבת אשר נעשו לפניכם ולא תטמאו בהם אני יהוה אלהיכם׃ | 30 |
Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.’”