< איוב 30 >
ועתה שחקו עלי צעירים ממני לימים אשר מאסתי אבותם לשית עם כלבי צאני׃ | 1 |
“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.
גם כח ידיהם למה לי עלימו אבד כלח׃ | 2 |
Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
בחסר ובכפן גלמוד הערקים ציה אמש שואה ומשאה׃ | 3 |
Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa.
הקטפים מלוח עלי שיח ושרש רתמים לחמם׃ | 4 |
Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi, nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio.
מן גו יגרשו יריעו עלימו כגנב׃ | 5 |
Walifukuzwa mbali na watu wao, wakipigiwa kelele kama wevi.
בערוץ נחלים לשכן חרי עפר וכפים׃ | 6 |
Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka, kwenye majabali na mahandaki.
בין שיחים ינהקו תחת חרול יספחו׃ | 7 |
Kwenye vichaka walilia kama punda, na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka.
בני נבל גם בני בלי שם נכאו מן הארץ׃ | 8 |
Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya, waliofukuzwa watoke katika nchi.
ועתה נגינתם הייתי ואהי להם למלה׃ | 9 |
“Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo; nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.
תעבוני רחקו מני ומפני לא חשכו רק׃ | 10 |
Wananichukia sana na kujitenga nami, wala hawasiti kunitemea mate usoni.
כי יתרו פתח ויענני ורסן מפני שלחו׃ | 11 |
Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa, wamekuwa huru kunitendea waonavyo.
על ימין פרחח יקומו רגלי שלחו ויסלו עלי ארחות אידם׃ | 12 |
Kuume kwangu kundi linashambulia; wao huitegea miguu yangu tanzi, na kunizingira.
נתסו נתיבתי להותי יעילו לא עזר למו׃ | 13 |
Huizuia njia yangu, nao hufanikiwa katika kuniletea maafa, nami sina yeyote wa kunisaidia.
כפרץ רחב יאתיו תחת שאה התגלגלו׃ | 14 |
Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana; katikati ya magofu huja na kunishambulia.
ההפך עלי בלהות תרדף כרוח נדבתי וכעב עברה ישעתי׃ | 15 |
Vitisho vimenifunika; heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo, salama yangu imetoweka kama wingu.
ועתה עלי תשתפך נפשי יאחזוני ימי עני׃ | 16 |
“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; siku za mateso zimenikamata.
לילה עצמי נקר מעלי וערקי לא ישכבון׃ | 17 |
Usiku mifupa yangu inachoma; maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe.
ברב כח יתחפש לבושי כפי כתנתי יאזרני׃ | 18 |
Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu.
הרני לחמר ואתמשל כעפר ואפר׃ | 19 |
Yeye amenitupa kwenye matope, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
אשוע אליך ולא תענני עמדתי ותתבנן בי׃ | 20 |
“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu.
תהפך לאכזר לי בעצם ידך תשטמני׃ | 21 |
Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.
תשאני אל רוח תרכיבני ותמגגני תשוה׃ | 22 |
Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali.
כי ידעתי מות תשיבני ובית מועד לכל חי׃ | 23 |
Ninajua utanileta mpaka kifoni, mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa.
אך לא בעי ישלח יד אם בפידו להן שוע׃ | 24 |
“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, anapoomba msaada katika shida yake.
אם לא בכיתי לקשה יום עגמה נפשי לאביון׃ | 25 |
Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini?
כי טוב קויתי ויבא רע ואיחלה לאור ויבא אפל׃ | 26 |
Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.
מעי רתחו ולא דמו קדמני ימי עני׃ | 27 |
Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili.
קדר הלכתי בלא חמה קמתי בקהל אשוע׃ | 28 |
Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.
אח הייתי לתנים ורע לבנות יענה׃ | 29 |
Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.
עורי שחר מעלי ועצמי חרה מני חרב׃ | 30 |
Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; mifupa yangu inaungua kwa homa.
ויהי לאבל כנרי ועגבי לקול בכים׃ | 31 |
Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo, nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.