< איוב 13 >

הן כל ראתה עיני שמעה אזני ותבן לה׃ 1
“Macho yangu yameona hili lote, masikio yangu yamesikia na kulielewa.
כדעתכם ידעתי גם אני לא נפל אנכי מכם׃ 2
Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; mimi si mtu duni kuliko ninyi.
אולם אני אל שדי אדבר והוכח אל אל אחפץ׃ 3
Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.
ואולם אתם טפלי שקר רפאי אלל כלכם׃ 4
Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!
מי יתן החרש תחרישון ותהי לכם לחכמה׃ 5
Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.
שמעו נא תוכחתי ורבות שפתי הקשיבו׃ 6
Sikieni sasa hoja yangu; sikilizeni kusihi kwangu.
הלאל תדברו עולה ולו תדברו רמיה׃ 7
Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?
הפניו תשאון אם לאל תריבון׃ 8
Mtamwonyesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?
הטוב כי יחקר אתכם אם כהתל באנוש תהתלו בו׃ 9
Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?
הוכח יוכיח אתכם אם בסתר פנים תשאון׃ 10
Hakika angewakemea kama mkiwapendelea watu kwa siri.
הלא שאתו תבעת אתכם ופחדו יפל עליכם׃ 11
Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?
זכרניכם משלי אפר לגבי חמר גביכם׃ 12
Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.
החרישו ממני ואדברה אני ויעבר עלי מה׃ 13
“Nyamazeni kimya nipate kusema; kisha na yanipate yatakayonipata.
על מה אשא בשרי בשני ונפשי אשים בכפי׃ 14
Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?
הן יקטלני לא איחל אך דרכי אל פניו אוכיח׃ 15
Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.
גם הוא לי לישועה כי לא לפניו חנף יבוא׃ 16
Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu atakayethubutu kuja mbele yake!
שמעו שמוע מלתי ואחותי באזניכם׃ 17
Sikilizeni maneno yangu kwa makini; nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.
הנה נא ערכתי משפט ידעתי כי אני אצדק׃ 18
Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.
מי הוא יריב עמדי כי עתה אחריש ואגוע׃ 19
Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.
אך שתים אל תעש עמדי אז מפניך לא אסתר׃ 20
“Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, nami sitajificha uso wako:
כפך מעלי הרחק ואמתך אל תבעתני׃ 21
Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.
וקרא ואנכי אענה או אדבר והשיבני׃ 22
Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu.
כמה לי עונות וחטאות פשעי וחטאתי הדיעני׃ 23
Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.
למה פניך תסתיר ותחשבני לאויב לך׃ 24
Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako?
העלה נדף תערוץ ואת קש יבש תרדף׃ 25
Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?
כי תכתב עלי מררות ותורישני עונות נעורי׃ 26
Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.
ותשם בסד רגלי ותשמור כל ארחותי על שרשי רגלי תתחקה׃ 27
Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.
והוא כרקב יבלה כבגד אכלו עש׃ 28
“Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, kama vazi lililoliwa na nondo.

< איוב 13 >