< ירמיה 30 >
הדבר אשר היה אל ירמיהו מאת יהוה לאמר׃ | 1 |
Neno lilokuja kwa Yeremia kutoka kwa Yahwe likisema,
כה אמר יהוה אלהי ישראל לאמר כתב לך את כל הדברים אשר דברתי אליך אל ספר׃ | 2 |
“Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema, 'Jiandikie mwenyewe katika baraua maneno yote niliyotangaza kwako katika barua.
כי הנה ימים באים נאם יהוה ושבתי את שבות עמי ישראל ויהודה אמר יהוה והשבתים אל הארץ אשר נתתי לאבותם וירשוה׃ | 3 |
Maana ona, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapowarudisha mateka wa watu wangu Israeli na Yuda. Mimi, Yahwe, nimesema hili. Kwa maana nitawarudisha kwenye nchi ambayo niliwapa babu zao, na wataimiliki.”'
ואלה הדברים אשר דבר יהוה אל ישראל ואל יהודה׃ | 4 |
Haya ni maneno ambayo Yahwe anatangaza kuhusu Israeli na Yuda,
כי כה אמר יהוה קול חרדה שמענו פחד ואין שלום׃ | 5 |
“Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Tumesikia sauti ya kutetemesha ya hofu na wala siyo ya amani.
שאלו נא וראו אם ילד זכר מדוע ראיתי כל גבר ידיו על חלציו כיולדה ונהפכו כל פנים לירקון׃ | 6 |
Ulizeni na muone kama mwanaume anamwogopa mtoto. Mbona ninamwona kila mwanaume kijana ameshika mikono yake juu ya kiuno chake kama mwanamke anayejifungua mtoto? Kwa nini nyuso zao wote zimegeuka rangi?
הוי כי גדול היום ההוא מאין כמהו ועת צרה היא ליעקב וממנה יושע׃ | 7 |
Ole! Kwa maana siku hiyo itakuwa kuu, isiyofanana na yoyote. Utakuwa wakati wa huzuni kwa Yakobo, lakini ataokolewa.
והיה ביום ההוא נאם יהוה צבאות אשבר עלו מעל צוארך ומוסרותיך אנתק ולא יעבדו בו עוד זרים׃ | 8 |
Kwa maana itakuwa katika siku hiyo—hili ni tangazo la Yahwe wa majeshi—kwamba nitaivunja nira ya shingo zenu, na nitaisambaza minyororo yenu, kwa hiyo wageni hawatawafanya watumwa tena.
ועבדו את יהוה אלהיהם ואת דוד מלכם אשר אקים להם׃ | 9 |
Bali watamwabudu Yahwe Mungu wao na kumtumikia Daudi mfalme wao, ambaye nitamfanya mfalme juu yao.
ואתה אל תירא עבדי יעקב נאם יהוה ואל תחת ישראל כי הנני מושיעך מרחוק ואת זרעך מארץ שבים ושב יעקב ושקט ושאנן ואין מחריד׃ | 10 |
Kwa hiyo wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope—hili ni tangazo la Yahwe—na usikate tamaa, Israeli. Maana ona, niko karibu kukurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya utumwa, Yakobo atarudi na kuwa katika amani; ataokolewa, na hapatakuwa na hofu zaidi.
כי אתך אני נאם יהוה להושיעך כי אעשה כלה בכל הגוים אשר הפצותיך שם אך אתך לא אעשה כלה ויסרתיך למשפט ונקה לא אנקך׃ | 11 |
Kwa maana niko pamoja nawe—hili ni tangazo la Yahwe—ili kukuokoa. Kisha nitaleta mwisho kamili kwa mataifa yote ambako nimewatawanya. Bali sitaweka mwisho kwako, ingawa ninakuadhibu kwa haki na kwa hakika sitakuacha bila kukuadhibu.'
כי כה אמר יהוה אנוש לשברך נחלה מכתך׃ | 12 |
Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Jeraha lako si la kupona; kidonda chako kimeenea.
אין דן דינך למזור רפאות תעלה אין לך׃ | 13 |
Hakuna mtu wa kukutetea kesi yako; hakuna utetezi kwa ajili ya kidonda chako ili upone.
כל מאהביך שכחוך אותך לא ידרשו כי מכת אויב הכיתיך מוסר אכזרי על רב עונך עצמו חטאתיך׃ | 14 |
Wapenzi wako wote wamekusahau. Hawatakuangalia, kwa maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui na nidhimu ya bwana mkatili kwa sababu ya uovu wako mwingi na dhambi zako zisizohesabika.
מה תזעק על שברך אנוש מכאבך על רב עונך עצמו חטאתיך עשיתי אלה לך׃ | 15 |
Kwa nini unaita msaada kwa ajili ya jeraha lako? Maumivu yako hayaponyeki. kwa sambabu ya uovu wako mwingi, dhambi zako zisizohesabika, nimefanya mambo haya kwako.
לכן כל אכליך יאכלו וכל צריך כלם בשבי ילכו והיו שאסיך למשסה וכל בזזיך אתן לבז׃ | 16 |
Kila mtu akulaye ataliwa, na adui zako wote wataenda utumwani. Kwa maana kila aliyekuteka nyara atatekwa, na nitawafanya wote wanaokuwinda kuwa mawindo.
כי אעלה ארכה לך וממכותיך ארפאך נאם יהוה כי נדחה קראו לך ציון היא דרש אין לה׃ | 17 |
Kwa maana nitaleta uponyaji juu yako; nitakuponya majeraha yako—hili ni tangazo la Yahwe—nitafanya hivyo kwa sababu walikuita: Mwenyekutupwa. Hakuna anayeujali Sayuni.”
כה אמר יהוה הנני שב שבות אהלי יעקוב ומשכנתיו ארחם ונבנתה עיר על תלה וארמון על משפטו ישב׃ | 18 |
Yahwe anasema hivi, “Ona, niko karibu kuwarudisha mateka wa hema za Yakobo na kuwa na huruma juu ya nyumba zake. Kisha mji utajengwa juu ya lundo la magofu, na jumba litakuwepo tena kama ilivyokuwa kawaida.
ויצא מהם תודה וקול משחקים והרבתים ולא ימעטו והכבדתים ולא יצערו׃ | 19 |
Kisha wimbo wa kusifu na sauti ya ya shangwe itasikika kutoka kwao, kwa maana nitawaongeza na wala sitawapunguza; nitawaheshimu ili kwamba wasifanywe wanyonge.
והיו בניו כקדם ועדתו לפני תכון ופקדתי על כל לחציו׃ | 20 |
Kisha watu watakuwa kama ilivyokuwa mwanzo, na kusanyiko lao litaanzishwa mbele yangu wakati nitakapowaadhibu wote wanaowatesa kwa sasa.
והיה אדירו ממנו ומשלו מקרבו יצא והקרבתיו ונגש אלי כי מי הוא זה ערב את לבו לגשת אלי נאם יהוה׃ | 21 |
Kiongozi wao atatoka miongoni mwao. Atatokeza kutoka kati yao nitakapomleta karibu na atakapanikaribia mimi. kama sitafanya hivyo, ni nani atakayethubutu kunisogelea? —hili ni tangazo la Yahwe.
והייתם לי לעם ואנכי אהיה לכם לאלהים׃ | 22 |
Kisha mtakuwa watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu.
הנה סערת יהוה חמה יצאה סער מתגורר על ראש רשעים יחול׃ | 23 |
Ona, tufani ya Yahwe, ghadhabu yake, imekwenda nje. Ni tufani isiyokoma. Itazunguka juu ya vichwa vya watu waovu.
לא ישוב חרון אף יהוה עד עשתו ועד הקימו מזמות לבו באחרית הימים תתבוננו בה׃ | 24 |
Hasira ya Yahwe haitarudi mpaka itoke na kutimiza makusudi ya moyo wake. Katika siku za mwisho mtalielewa hili.”