< ירמיה 27 >

בראשית ממלכת יהויקם בן יאושיהו מלך יהודה היה הדבר הזה אל ירמיה מאת יהוה לאמר׃ 1
Katika mwanzo wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hil lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahwe. (Ingawa nakala nyingi za Kiebrania zinasema “Yehoyakimu, matoleo mengi ya kisasa yanasema “Sedekia”, kwa sababu tukio katika sura hii lilitokea katika kipindi cha utawala wake).
כה אמר יהוה אלי עשה לך מוסרות ומטות ונתתם על צוארך׃ 2
Hiki ndicho Yahwe alisema kwangu, “Tengeneza vifungo na nira kwa ajili yako mwenyewe. Ziweke shingoni mwako.
ושלחתם אל מלך אדום ואל מלך מואב ואל מלך בני עמון ואל מלך צר ואל מלך צידון ביד מלאכים הבאים ירושלם אל צדקיהו מלך יהודה׃ 3
Kisha akawatuma kwenda kw mfalme wa Edomu, mfalme wa Moabu, mfalme wa watu wa amoni, mfalme wa Tiro, na kwa mfalme wa Sidoni. Watume kwa mkono wa wajumbe hao wa wafalme ambao walikuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.
וצוית אתם אל אדניהם לאמר כה אמר יהוה צבאות אלהי ישראל כה תאמרו אל אדניכם׃ 4
Toa amri kwao kwa ajili ya mabwana zao na sema, ' Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Hivyo ndivyo utakavyosema kwa mabwana zenu,
אנכי עשיתי את הארץ את האדם ואת הבהמה אשר על פני הארץ בכחי הגדול ובזרועי הנטויה ונתתיה לאשר ישר בעיני׃ 5
Mimi mwenyewe niliiumba dunia kwa nguvu zangu kuu na mkono wangu ulioinuka. Pia niliwaumba watu na wanyama juu ya dunia, na nikawatoa kwa yeyote aliyesahihi katika macho yangu.
ועתה אנכי נתתי את כל הארצות האלה ביד נבוכדנאצר מלך בבל עבדי וגם את חית השדה נתתי לו לעבדו׃ 6
Kwa hiyo sasa, Mimi mwenyewe naziweka nchi hizi zote kwenye mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu. Pia, ninavikabidhi kwake viumbe hai vyote katika mashamba ili vimtumikie.
ועבדו אתו כל הגוים ואת בנו ואת בן בנו עד בא עת ארצו גם הוא ועבדו בו גוים רבים ומלכים גדלים׃ 7
Kwa maana mataifa yote watamtumikia yeye, wanaye, na wajukuu zake hadi muda wa nchi yake ufike. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamtiisha.
והיה הגוי והממלכה אשר לא יעבדו אתו את נבוכדנאצר מלך בבל ואת אשר לא יתן את צוארו בעל מלך בבל בחרב וברעב ובדבר אפקד על הגוי ההוא נאם יהוה עד תמי אתם בידו׃ 8
Kwa hiyo taifa na ufalme ambo haumtumikii Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na ule usioweka shingo yake chini ya nira ya Nebukadreza mfalme wa Babeli—nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa, na pigo—hili ni tangazo la Yahwe—hadi nitakapokuwa nimewateketeza kwa mkono wake.
ואתם אל תשמעו אל נביאיכם ואל קסמיכם ואל חלמתיכם ואל ענניכם ואל כשפיכם אשר הם אמרים אליכם לאמר לא תעבדו את מלך בבל׃ 9
Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, wabashiri wenu, waonaji wenu, ndoto zenu, watambuzi wenu, ambao wamekuw wakisema kwenu na kusema, ' Msimtumikie mfalme wa Babeli.'
כי שקר הם נבאים לכם למען הרחיק אתכם מעל אדמתכם והדחתי אתכם ואבדתם׃ 10
Kwa maana wanatabiri uongo kwenu ili kuwapeleka mbali na nchi zenu, kwa maana nitawapeleka mbali, na mtakufa.
והגוי אשר יביא את צוארו בעל מלך בבל ועבדו והנחתיו על אדמתו נאם יהוה ועבדה וישב בה׃ 11
Lakini taifa ambalo wataweka shingo zao chini ya nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitawaruhusu kupumzika katika nchi yao—hili ni tangazo la Yahwe—na watailima na kufanya nyumba zao humo.””
ואל צדקיה מלך יהודה דברתי ככל הדברים האלה לאמר הביאו את צואריכם בעל מלך בבל ועבדו אתו ועמו וחיו׃ 12
Kwa hiyo nilisema kwa Sedekia mfalme wa Yuda na kumpa ujumbe huu, “Ziwekeni shingo zenu chini ya nira ya mfalme wa Babeli na mtumikieni yeye na watu wake, na mtaishi.
למה תמותו אתה ועמך בחרב ברעב ובדבר כאשר דבר יהוה אל הגוי אשר לא יעבד את מלך בבל׃ 13
Kwa nini mfe—wewe na watu wako—kwa upanga, njaa, na pigo, kama vile nilivyotangaza kuhusu taifa ambalo watapuuza kumtumikia mfalme wa Babeli?
ואל תשמעו אל דברי הנבאים האמרים אליכם לאמר לא תעבדו את מלך בבל כי שקר הם נבאים לכם׃ 14
Msisikilize maneno ya manabii wanaozungumza kwenu na kusema, 'Msimtumikie mfalme wa Babeli', kwa maana wanatabiri uongo kwenu.
כי לא שלחתים נאם יהוה והם נבאים בשמי לשקר למען הדיחי אתכם ואבדתם אתם והנבאים הנבאים לכם׃ 15
'Kwa maana mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana wanatabiri uongo katika jina langu ili kwamba niwafukeze inje na muangamie, ninyi nyote na manabii wanaotabiri kwenu.”'
ואל הכהנים ואל כל העם הזה דברתי לאמר כה אמר יהוה אל תשמעו אל דברי נביאיכם הנבאים לכם לאמר הנה כלי בית יהוה מושבים מבבלה עתה מהרה כי שקר המה נבאים לכם׃ 16
Nilitangaza hili kwa makuhani na watu wote na kusema, “Yahwe anasema hivi: Msisikilize maneno ya manabii wanaotabiri kwenu na kusema, 'Angalia! Vyombo vya nyumba ya Yahwe vinarudishwa kutoka Babeli sasa hivi!' Wanatabiri uongo kwenu.
אל תשמעו אליהם עבדו את מלך בבל וחיו למה תהיה העיר הזאת חרבה׃ 17
Msiwasikilize. Mtamtumikia mfalme wa Babeli na mtaishi. Kwa nini mji huu uangamizwe?
ואם נבאים הם ואם יש דבר יהוה אתם יפגעו נא ביהוה צבאות לבלתי באו הכלים הנותרים בבית יהוה ובית מלך יהודה ובירושלם בבלה׃ 18
Kama ni manabii, na kama neno la Mungu limekuja kwao kweli, basi wamwombe Yahwe wa majeshi asivipeleke Babeli vyombo vilivyosalia katika nyumba, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu.
כי כה אמר יהוה צבאות אל העמדים ועל הים ועל המכנות ועל יתר הכלים הנותרים בעיר הזאת׃ 19
Yahwe wa majeshi anasema hivi kuhusu zile nguzo, bahari, na kitako, na vyombo vyote vilivyosalia katika mji huu—
אשר לא לקחם נבוכדנאצר מלך בבל בגלותו את יכוניה בן יהויקים מלך יהודה מירושלם בבלה ואת כל חרי יהודה וירושלם׃ 20
vyombo ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika utumwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.
כי כה אמר יהוה צבאות אלהי ישראל על הכלים הנותרים בית יהוה ובית מלך יהודה וירושלם׃ 21
Yahwe wa majeshsi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu vyombo vilivyosalia katika nyumba ya Yahwe, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu,
בבלה יובאו ושמה יהיו עד יום פקדי אתם נאם יהוה והעליתים והשיבתים אל המקום הזה׃ 22
'Vitaletwa Babeli, na vitabaki huko hadi siku niyovipangia kutimia—hili ni tangazo la Yahwe—kisha nitavileta na kuvirudisha kataika sehemu hii.”

< ירמיה 27 >