< ירמיה 26 >
בראשית ממלכות יהויקים בן יאשיהו מלך יהודה היה הדבר הזה מאת יהוה לאמר׃ | 1 |
Mwanzoni mwa utawala wake Yehoyakimu mwana wa Yosia, neno likaja kutoka kwa Yeremia, likisema,
כה אמר יהוה עמד בחצר בית יהוה ודברת על כל ערי יהודה הבאים להשתחות בית יהוה את כל הדברים אשר צויתיך לדבר אליהם אל תגרע דבר׃ | 2 |
“Yahwe anasema hivi: Simama katika uwanja wa nyumba yangu na sema kuhusu miji yote ya Yuda ambao huja kuabudu katika nyumba yangu. Tangaza maneno yote niliyokuamuru kuyasema kwao. Usipunguze neno lolote!
אולי ישמעו וישבו איש מדרכו הרעה ונחמתי אל הרעה אשר אנכי חשב לעשות להם מפני רע מעלליהם׃ | 3 |
Labda watasikiliza, kwamba kila mtu ataziacha njia zake mbaya, ili nighairi majanga ninayokusudia kuyaleta juu yao kwa sababu ya uovu wa matendo yao.
ואמרת אליהם כה אמר יהוה אם לא תשמעו אלי ללכת בתורתי אשר נתתי לפניכם׃ | 4 |
Kwa hiyo lazima useme kwao, 'Yahwe anasema hivi: Kama hamtanisikiliza ili mtembee katika sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu—
לשמע על דברי עבדי הנבאים אשר אנכי שלח אליכם והשכם ושלח ולא שמעתם׃ | 5 |
kama hamsikilizi maneno ya watumishi wangu manabii ambao naendelea kuwatuma kwenu—lakini hamjasikiliza! —
ונתתי את הבית הזה כשלה ואת העיר הזאתה אתן לקללה לכל גויי הארץ׃ | 6 |
kisha nitaifanya nyumba hii kuwa kama Shilo; nitaifanya nyumba hii kuwa laana katika macho ya mataifa yote juu ya dunia.
וישמעו הכהנים והנבאים וכל העם את ירמיהו מדבר את הדברים האלה בבית יהוה׃ | 7 |
Makuhani, manabii, na watu wote wakamsikia Yeremia akitangaza maneno haya katika nyumba ya Yahwe.
ויהי ככלות ירמיהו לדבר את כל אשר צוה יהוה לדבר אל כל העם ויתפשו אתו הכהנים והנבאים וכל העם לאמר מות תמות׃ | 8 |
Kwa hiyo ikatokea kwamba Yeremia alipomaliza kutangaza aliyokuwa Yahwe alimwwamuru kuyasema kwa watu wote, makuhani, manabii, na watu wote wakamsimamisha na kusema, “Hakika utakufa!
מדוע נבית בשם יהוה לאמר כשלו יהיה הבית הזה והעיר הזאת תחרב מאין יושב ויקהל כל העם אל ירמיהו בבית יהוה׃ | 9 |
Kwa nini umetabiri katika jina la Yahwe na kusema kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa, pasipo wakaaji?” Kwa maana watu wote wameunda kundi dhidi ya nyumba ya Yeremia.
וישמעו שרי יהודה את הדברים האלה ויעלו מבית המלך בית יהוה וישבו בפתח שער יהוה החדש׃ | 10 |
Kisha wakuu wa Yuda wakasikia maneno haya na wakapanda kutoka nyumba ya mfalme kwenda kwenye nyumba ya Yahwe. Wakakaa katika njia ya lango katika Lango Jipya la nyumba ya Yahwe.
ויאמרו הכהנים והנבאים אל השרים ואל כל העם לאמר משפט מות לאיש הזה כי נבא אל העיר הזאת כאשר שמעתם באזניכם׃ | 11 |
Makuhani na manabii wakasema kwa wakuu wa Yuda na kwa watu wote. Wakasema, “Ni haki kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu!”
ויאמר ירמיהו אל כל השרים ואל כל העם לאמר יהוה שלחני להנבא אל הבית הזה ואל העיר הזאת את כל הדברים אשר שמעתם׃ | 12 |
Kwa hiyo Yeremia akasema kwa wakuu wote na watu wote, “Yeremia amenituma kutabiri juu ya nyumb hii na mji wake, kusema maneno yote ambayo mmeyasikia.
ועתה היטיבו דרכיכם ומעלליכם ושמעו בקול יהוה אלהיכם וינחם יהוה אל הרעה אשר דבר עליכם׃ | 13 |
Kwa hiyo sasa, imarisheni njia zenu na matendo yenu, na sikilizeni sauti ya Yahwe Mungu wenu kwamba ataghairi kuhusu janga ambalo ametangaza dhidi yenu.
ואני הנני בידכם עשו לי כטוב וכישר בעיניכם׃ | 14 |
Mimi mwenyewe—niangalieni! —niko mikononi mwenu. Nitendeeni yaliyo mema na sahihi katika macho yenu.
אך ידע תדעו כי אם ממתים אתם אתי כי דם נקי אתם נתנים עליכם ואל העיר הזאת ואל ישביה כי באמת שלחני יהוה עליכם לדבר באזניכם את כל הדברים האלה׃ | 15 |
Lakini kwa hakika lazima mjue kwamba kama mtaniua mimi, basi mnaiweka damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wakaaji wake, kwa maana Yahwe amenituma kweli kwenu ili nitangaze maneno yote kwa ajili ya masikio yenu.”
ויאמרו השרים וכל העם אל הכהנים ואל הנביאים אין לאיש הזה משפט מות כי בשם יהוה אלהינו דבר אלינו׃ | 16 |
Kisha wakuu na watu wote wakasema kwa makuhani na manabii, “Si vyema kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametangaza mambo haya kwetu katika jina la Yahwe Mungu wetu.”
ויקמו אנשים מזקני הארץ ויאמרו אל כל קהל העם לאמר׃ | 17 |
Kisha watu kutoka wazee wa nchi wakasimama na kusema kwa kusanyiko lote la watu.
מיכיה המורשתי היה נבא בימי חזקיהו מלך יהודה ויאמר אל כל עם יהודה לאמר כה אמר יהוה צבאות ציון שדה תחרש וירושלים עיים תהיה והר הבית לבמות יער׃ | 18 |
Wakasema, “Mikaya Mmorashi alikuwa akitabiri katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Alinena kwa watu wote wa Yuda na kusema, 'Yahwe wa majeshi anasema hivi: Sayuni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa lundo la magofu, na mlima wa hekalu utakuwa kilima kilichoota vichaka.' Hezekia mfalme wa Yuda na Yunda wote walimuua?
ההמת המתהו חזקיהו מלך יהודה וכל יהודה הלא ירא את יהוה ויחל את פני יהוה וינחם יהוה אל הרעה אשר דבר עליהם ואנחנו עשים רעה גדולה על נפשותינו׃ | 19 |
Hakumwogopa Yahwe na kuutaka radhi uso wa Yahwe ili kwamba Yahwe angeghairi kuhusu janga ambalo alilitangaza kwao? Kwa hiyo tutafanya maovu makubwa zaidi juu ya maisha yetu sisi wenyewe?”
וגם איש היה מתנבא בשם יהוה אוריהו בן שמעיהו מקרית היערים וינבא על העיר הזאת ועל הארץ הזאת ככל דברי ירמיהו׃ | 20 |
Wakati huo huo palikuwa na mtu mwingine ambaye alitabiri katika jina la Yahwe—Uria mwan wa Shemaya kutoka Kiriath Yearimu—pia alitabiri juu ya mji na nchi hii, akikubaliana na maneno yote ya Yeremia.
וישמע המלך יהויקים וכל גבוריו וכל השרים את דבריו ויבקש המלך המיתו וישמע אוריהו וירא ויברח ויבא מצרים׃ | 21 |
Lakini Mfalme Yohoyakimu na wanajeshi wake wote na watumishi wake wote waliposikia maneno yake, kisha mfalme alijaribu kumuua, lakini Uria alisikia na kuogopa, kwa hiyo alikimbia na akaenda Misiri
וישלח המלך יהויקים אנשים מצרים את אלנתן בן עכבור ואנשים אתו אל מצרים׃ | 22 |
Kisha mfalme Yehoyakimu alituma watu kwenda Misiri—Elnathani mwana wa Achbori na watu kwenda Misiri kumfuata Uria.
ויוציאו את אוריהו ממצרים ויבאהו אל המלך יהויקים ויכהו בחרב וישלך את נבלתו אל קברי בני העם׃ | 23 |
Wakamtoa Uria nje kutoka Misiri na kumleta kwa Mfalme Yehoyakimu. Kisha Yehoyakimu akamuua kwa upanga na kumpeleka nje kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
אך יד אחיקם בן שפן היתה את ירמיהו לבלתי תת אתו ביד העם להמיתו׃ | 24 |
Lakini mkno wa Ahikamu mwana wa Shapni alikuwa pamoja na Yeremia, hivyo hakutiwa mikonono mwa watu ili auawe.