< אֶל־הָעִבְרִים 1 >
האלהים אשר דבר מקדם פעמים רבות ובפנים שנים אל אבתינו ביד הנביאים דבר אלינו באחרית הימים האלה ביד בנו׃ | 1 |
Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali,
אשר נתנו ליורש כל וגם עשה בידו את העולמות׃ (aiōn ) | 2 |
lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu. (aiōn )
והוא זהר כבודו וצלם ישותו ונושא כל בדבר גבורתו ואחרי עשתו בנפשו טהרת חטאתינו ישב לימין הגדלה במרומים׃ | 3 |
Mwana ni mngʼao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni.
ויגדל מאד מן המלאכים כאשר השם אשר נחלו יקר הוא משלהם׃ | 4 |
Kwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao.
כי אל מי מן המלאכים אמר מעולם בני אתה אני היום ילדתיך ועוד אני אהיה לו לאב והוא יהיה לי לבן׃ | 5 |
Kwa maana ni malaika yupi ambaye wakati wowote Mungu alipata kumwambia, “Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa?” Au tena, “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu?”
ובהביאו את הבכור שנית לעולם אמר והשתחוו לו כל מלאכים אלהים׃ | 6 |
Tena, Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, anasema, “Malaika wote wa Mungu na wamsujudu.”
הן על המלאכים הוא אמר עשה מלאכיו רוחות משרתיו אש להט׃ | 7 |
Anenapo kuhusu malaika asema, “Huwafanya malaika wake kuwa pepo, watumishi wake kuwa miali ya moto.”
אך על הבן אמר כסאך אלהים עולם ועד שבט מישר שבט מלכותך׃ (aiōn ) | 8 |
Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako. (aiōn )
אהבת צדק ותשנא רשע על כן משחך אלהים אלהיך שמן ששון מחבריך׃ | 9 |
Umependa haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako kwa kukupaka mafuta ya furaha.”
ועוד אתה אדני לפנים הארץ יסדת ומעשה ידיך שמים׃ | 10 |
Pia asema, “Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.
המה יאבדו ואתה תעמד וכלם כבגד יבלו׃ | 11 |
Hizo zitatoweka, lakini wewe utadumu; zote zitachakaa kama vazi.
כלבוש תחליפם ויחלפו ואתה הוא ושנותיך לא יתמו׃ | 12 |
Utazikungʼutakungʼuta kama joho, nazo zitachakaa kama vazi. Lakini wewe hubadiliki, nayo miaka yako haikomi kamwe.”
ואל מי מן המלאכים אמר מעולם שב לימיני עד אשית איביך הדם לרגליך׃ | 13 |
Je, ni kwa malaika yupi ambaye Mungu amepata kumwambia wakati wowote, “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako”?
הלא הם כלם רוחות השרת שלוחים לעזרה בעד העתידים לרשת את הישועה׃ | 14 |
Je, malaika wote si roho watumikao, waliotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?