< בראשית 39 >

ויוסף הורד מצרימה ויקנהו פוטיפר סריס פרעה שר הטבחים איש מצרי מיד הישמעאלים אשר הורדהו שמה׃ 1
Yusufu akaletwa Misri. Potifa, aliyekuwa afisa wa Farao mkuu wa walinzi na Mmisri, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli, waliokuwa wamempeleka pale.
ויהי יהוה את יוסף ויהי איש מצליח ויהי בבית אדניו המצרי׃ 2
Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na akawa mtu aliyefanikiwa. Aliishi katika nyumba ya Mmisri bwana wake.
וירא אדניו כי יהוה אתו וכל אשר הוא עשה יהוה מצליח בידו׃ 3
Bwana wake akaona kwamba Yahwe alikuwa pamoja naye na kwamba Yahwe alifanikisha kila kitu alichokifanya.
וימצא יוסף חן בעיניו וישרת אתו ויפקדהו על ביתו וכל יש לו נתן בידו׃ 4
Yusufu akapata kibali mbele zake. Akamtumikia Potifa. Potifa akamfanya msimamizi juu ya nyumba yake, na kila alichokimiliki, akakiweka chini ya uangalizi wake.
ויהי מאז הפקיד אתו בביתו ועל כל אשר יש לו ויברך יהוה את בית המצרי בגלל יוסף ויהי ברכת יהוה בכל אשר יש לו בבית ובשדה׃ 5
Ikawa alipomfanya msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki, Yahwe akaibariki nyumba ya Mmisri kwa sababu ya Yusufu. Baraka za Yahwe zilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa nyumbani na shambani.
ויעזב כל אשר לו ביד יוסף ולא ידע אתו מאומה כי אם הלחם אשר הוא אוכל ויהי יוסף יפה תאר ויפה מראה׃ 6
Potifa akaweka kila alichokuwa nacho chini ya uangalizi wa Yusufu. Hakuwa na haja ya kufikiri juu ya lolote isipokuwa chakula alichokula tu. Basi Yusufu alikuwa kijana mzuri na wa kuvutia.
ויהי אחר הדברים האלה ותשא אשת אדניו את עיניה אל יוסף ותאמר שכבה עמי׃ 7
Ikawa baada ya hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu. Akamwambia, “Lala nami.”
וימאן ויאמר אל אשת אדניו הן אדני לא ידע אתי מה בבית וכל אשר יש לו נתן בידי׃ 8
Lakini yeye alikataa na kumwambia mke wa bwana wake, “Tazama, bwana wangu haangalii chochote nikifanyacho nyumbani, na ameweka kila kitu anachokimiliki chini ya uangalizi wangu.
איננו גדול בבית הזה ממני ולא חשך ממני מאומה כי אם אותך באשר את אשתו ואיך אעשה הרעה הגדלה הזאת וחטאתי לאלהים׃ 9
Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi. Hajanidhuiria chochote isipokuwa wewe, kwa sababu wewe ni mkewe. Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu?
ויהי כדברה אל יוסף יום יום ולא שמע אליה לשכב אצלה להיות עמה׃ 10
Akamwambia Yusufu siku baada ya siku, lakini yeye akakataa kulala naye wala kuwa naye.
ויהי כהיום הזה ויבא הביתה לעשות מלאכתו ואין איש מאנשי הבית שם בבית׃ 11
Ikawa siku moja aliingia ndani kufanya kazi yake. Hakuna mtu yeyote wa nyumbani aliyekuwepo pale ndani.
ותתפשהו בבגדו לאמר שכבה עמי ויעזב בגדו בידה וינס ויצא החוצה׃ 12
Akashika nguo zake na kusema, “Lala nami.” Akaacha nguo zake mikononi mwake, akakimbia, na kutoka nje.
ויהי כראותה כי עזב בגדו בידה וינס החוצה׃ 13
Ikawa, alipoona kwamba ameziacha nguo zake mikononi mwake na kwamba amekimbia nje,
ותקרא לאנשי ביתה ותאמר להם לאמר ראו הביא לנו איש עברי לצחק בנו בא אלי לשכב עמי ואקרא בקול גדול׃ 14
akawaita watu wa nyumbani mwake na kuwambia, “Tazama, Potifa ameleta Mwebrania huyu kutudhihaki. Aliingia kulala nami, na nikapiga kelele.
ויהי כשמעו כי הרימתי קולי ואקרא ויעזב בגדו אצלי וינס ויצא החוצה׃ 15
Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha na nguo yake, akakimbia, na kutoka nje.”
ותנח בגדו אצלה עד בוא אדניו אל ביתו׃ 16
Akaweka nguo zake karibu naye hata bwana yake alipokuja nyumbani.
ותדבר אליו כדברים האלה לאמר בא אלי העבד העברי אשר הבאת לנו לצחק בי׃ 17
Akamwambia maelelezo haya, “Yule mtumishi Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kunidhihaki.
ויהי כהרימי קולי ואקרא ויעזב בגדו אצלי וינס החוצה׃ 18
Ikawa nilipopiga kelele, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje.”
ויהי כשמע אדניו את דברי אשתו אשר דברה אליו לאמר כדברים האלה עשה לי עבדך ויחר אפו׃ 19
Ikawa, bwana wake aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe, “Hivi ndivyo mtumishi wako alivyonitenda,” alikasirika sana.
ויקח אדני יוסף אתו ויתנהו אל בית הסהר מקום אשר אסורי המלך אסורים ויהי שם בבית הסהר׃ 20
Bwana wa Yusufu akamchukua na kumweka gerezani, mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme. Akawa pale kifungoni.
ויהי יהוה את יוסף ויט אליו חסד ויתן חנו בעיני שר בית הסהר׃ 21
Lakini Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na kumwonyesha uaminifu wa agano. Akampa kibali mbele ya mlinzi wa gereza.
ויתן שר בית הסהר ביד יוסף את כל האסירם אשר בבית הסהר ואת כל אשר עשים שם הוא היה עשה׃ 22
Mlinzi wa gereza akawaweka mikononi mwa Yusufu wafungwa wote waliokuwa gerezani. Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu.
אין שר בית הסהר ראה את כל מאומה בידו באשר יהוה אתו ואשר הוא עשה יהוה מצליח׃ 23
Mlinzi wa gereza hakuwa na wasiwasi juu ya chochote kilichokuwa mkononi mwake, kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye. Yahwe akafanikisha kila alichokifanya.

< בראשית 39 >