< דברים 17 >
לא תזבח ליהוה אלהיך שור ושה אשר יהיה בו מום כל דבר רע כי תועבת יהוה אלהיך הוא׃ | 1 |
Haupaswi kumtolea dhabihu Yahwe Mungu wako ng'ombe au kondoo aliye na kasoro au kitu chochote kibaya, kwa kuwa hiyo itakuwa chukizo kwa Yahwe Mungu wako.
כי ימצא בקרבך באחד שעריך אשר יהוה אלהיך נתן לך איש או אשה אשר יעשה את הרע בעיני יהוה אלהיך לעבר בריתו׃ | 2 |
Kama kunapatikana miongoni mwenu, ndani ya malango ya mji wowote ambao Yahwe Mungu wenu anawapatia, mwanaume yoyote au mwanamke ambaye anafanya uovu mbele ya Yahwe Mungu wenu kuiharibu agano lake -
וילך ויעבד אלהים אחרים וישתחו להם ולשמש או לירח או לכל צבא השמים אשר לא צויתי׃ | 3 |
yoyote ambaye ameenda na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, wala jua, mwezi, au kati ya jeshi la mbinguni- hakuna chochote nimekuamuru,
והגד לך ושמעת ודרשת היטב והנה אמת נכון הדבר נעשתה התועבה הזאת בישראל׃ | 4 |
na kama ungeambiwa kuhusu hiki, au kama una mifugo- basi unapaswa kufanya uchunguzi wa makini. Kama ni kweli na hakika kwamba chukizo kama hilo limefanyika Israeli-
והוצאת את האיש ההוא או את האשה ההוא אשר עשו את הדבר הרע הזה אל שעריך את האיש או את האשה וסקלתם באבנים ומתו׃ | 5 |
-basi utamleta huyo mwanaume au mwanamke, aliyefanya uovu huu, katika malango ya mji, kwamba mwanaume kabisa au mwanamke, na umponde huyo mtu mpaka kufa.
על פי שנים עדים או שלשה עדים יומת המת לא יומת על פי עד אחד׃ | 6 |
Kwa kinywa cha mashahidi wawili, au mashahidi watatu, itakuwa yeye anayepaswa kuuwawa; lakini kwa kinywa cha shahidi mmoja peke hatauwawa.
יד העדים תהיה בו בראשנה להמיתו ויד כל העם באחרנה ובערת הרע מקרבך׃ | 7 |
Mkono wa mashahidi unapaswa kuwa wa kwanza kumuuwa, na badae mkono wa watu wote; na mtamuondoa muovu miongoni mwenu.
כי יפלא ממך דבר למשפט בין דם לדם בין דין לדין ובין נגע לנגע דברי ריבת בשעריך וקמת ועלית אל המקום אשר יבחר יהוה אלהיך בו׃ | 8 |
Kama jambo linatokea ambalo ni gumu kwenu kufanya maamuzi- pengine swali la mauaji au kifo cha ajali, haki ya mtu mmoja na haki ya mtu mwingine, au swali moja la aina ya kuzulu kufanyika, au aina nyingine ya jambo-mambo ya utata ndani ya malango yenu, basi utapaswa kwenda kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kama patakatifu pake.
ובאת אל הכהנים הלוים ואל השפט אשר יהיה בימים ההם ודרשת והגידו לך את דבר המשפט׃ | 9 |
Utapaswa kwenda kwa makuhani, wazao wa Lawi, na kwa mwamuzi atakayetumika kwa wakati huo; mtatafuta ushauri wao, na watawapa ninyi maamuzi.
ועשית על פי הדבר אשר יגידו לך מן המקום ההוא אשר יבחר יהוה ושמרת לעשות ככל אשר יורוך׃ | 10 |
Mnapaswa kufuata sheria mliyopewa, katika eneo Yahwe atachagua kama patakatifu pake. Mtakuwa makini kufanya kila kitu ambacho wanawaelekeza kufanya.
על פי התורה אשר יורוך ועל המשפט אשר יאמרו לך תעשה לא תסור מן הדבר אשר יגידו לך ימין ושמאל׃ | 11 |
Fuata sheria wanayowafundisha, na kufanya kulingana na maamuzi wanawapa. Msigeuke kutoka kwa kile wanawambia, kwa kulia au kushoto.
והאיש אשר יעשה בזדון לבלתי שמע אל הכהן העמד לשרת שם את יהוה אלהיך או אל השפט ומת האיש ההוא ובערת הרע מישראל׃ | 12 |
Yeyote anayefanya kwa kiburi, kwa kutomsikiliza kuhani anayesimama kutumika mbele ya Yahwe Mungu wako, au kwa kutomsikiliza mwamuzi- huyu mtu atakufa; mtaweka mbali uovu kutoka Israeli.
וכל העם ישמעו ויראו ולא יזידון עוד׃ | 13 |
Watu wote wanapaswa kusikia na kuogopa, na kutofanya kwa kiburi tena.
כי תבא אל הארץ אשר יהוה אלהיך נתן לך וירשתה וישבתה בה ואמרת אשימה עלי מלך ככל הגוים אשר סביבתי׃ | 14 |
Wakati mlipokuja kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu anawapa, na wakati mnamiliki na kuanza kuishi ndani yake, na halafu unasema, 'Nitajiwekea mfalme juu yangu, kama mataifa yote yanayonizunguka mimi,'
שום תשים עליך מלך אשר יבחר יהוה אלהיך בו מקרב אחיך תשים עליך מלך לא תוכל לתת עליך איש נכרי אשר לא אחיך הוא׃ | 15 |
basi unapaswa kwa hakika kujiwekea mfalme juu yako mtu yeyote ambaye Yahwe atachagua. Unapaswa kujiweka kama mfalme juu yako mtu yeyote kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Haupaswi kuweka mgeni, ambaye si ndugu yenu, juu yenu.
רק לא ירבה לו סוסים ולא ישיב את העם מצרימה למען הרבות סוס ויהוה אמר לכם לא תספון לשוב בדרך הזה עוד׃ | 16 |
Lakini hapaswi kuzidisha farasi kwa ajili yake, wala kusababisha watu kurudi Misri ili kwamba aweze kuzidisha farasi, kwa kuwa Yahwe alikwisha sema kwako, 'Unapaswa kuanzia sasa usirudi njia hiyo tena.'
ולא ירבה לו נשים ולא יסור לבבו וכסף וזהב לא ירבה לו מאד׃ | 17 |
Na hapaswi kuzidisha wake kwa ajili yake, ili kwamba moyo wake usigeuke kotoka kwa Yahwe; wala hapaswi sana kuzidisha kwa ajili yake fedha au dhahabu.
והיה כשבתו על כסא ממלכתו וכתב לו את משנה התורה הזאת על ספר מלפני הכהנים הלוים׃ | 18 |
Wakati aketipo kwenye kiti cha enzi cha ufalme wake, anapaswa kuandika kwenye kitabu kwa ajili yake nakala ya sheria hii, kutoka kwenye sheria ambayo iko mbele ya makuhani, ambao ni Walawi.
והיתה עמו וקרא בו כל ימי חייו למען ילמד ליראה את יהוה אלהיו לשמר את כל דברי התורה הזאת ואת החקים האלה לעשתם׃ | 19 |
Kitabu kinapaswa kuwa na yeye, na anapaswa kusoma ndani yake kwa siku zake zote, ili kwamba aweze kujifunza kumheshimu Yahwe Mungu wako, ili kwamba ashike maneno yote ya sheria hii na amri hizi, kuzishika.
לבלתי רום לבבו מאחיו ולבלתי סור מן המצוה ימין ושמאול למען יאריך ימים על ממלכתו הוא ובניו בקרב ישראל׃ | 20 |
Anapaswa kufanya hivi ili kwamba moyo wake usiinuliwe zaidi ya ndugu zake, na ili kwamba asigeuke mbali na amri, kwa kulia au kwa kushoto' kwa kusudi kwamba aweze kuzidisha siku zake katika ufalme wake, yeye na watoto wake, miongoni mwa Israel.