< מלכים ב 6 >

ויאמרו בני הנביאים אל אלישע הנה נא המקום אשר אנחנו ישבים שם לפניך צר ממנו׃ 1
Wana wa manabii wakamwambia Elisha, “Sehemu ambayo tunayoishi na wewe ni ndogo sana kwa ajili ya wote.
נלכה נא עד הירדן ונקחה משם איש קורה אחת ונעשה לנו שם מקום לשבת שם ויאמר לכו׃ 2
Tafadhali, tuache tuende Yordani, na umwache kila mtu akate mti hapo ambako tunaweza kuishi.” Elisha akajibu, “unaweza kwenda mbele.”
ויאמר האחד הואל נא ולך את עבדיך ויאמר אני אלך׃ 3
Mmoja wao akasema, “Nenda na watumishi wako tafadhali.” Elisha akajibu, “Nitaenda.”
וילך אתם ויבאו הירדנה ויגזרו העצים׃ 4
Kwa hiyo akaenda pamoja nao, na wakati walipokuja Yordani, wakaanza kukata miti.
ויהי האחד מפיל הקורה ואת הברזל נפל אל המים ויצעק ויאמר אהה אדני והוא שאול׃ 5
Lakini mmoja wao alipokuwa akikata, kichwa cha shoka kikaangukia kwenye maji; akalia kwa sauti na kusema, “la hasha, bwana wangu, kilikuwa kimeazimwa!”
ויאמר איש האלהים אנה נפל ויראהו את המקום ויקצב עץ וישלך שמה ויצף הברזל׃ 6
Basi mtu wa Mungu akasema, “kiliangukia wapi?” Yule mtu akamwonyesha Elisha ile sehemu. akakata fimbo, akarusha kwenye maji, na kufanya chuma kuelea.
ויאמר הרם לך וישלח ידו ויקחהו׃ 7
Elisha akasema, “Kichukue.” Basi yule mtu akafikisha mkono wake na kukinyakua.
ומלך ארם היה נלחם בישראל ויועץ אל עבדיו לאמר אל מקום פלני אלמני תחנתי׃ 8
Basi mfalme wa Shamu alikuwa akipigana vita dhidi ya Israel. Akafanya shauri na watumishi wake, akisema, “kambi yangu itakuwa sehemu flani na flani.”
וישלח איש האלהים אל מלך ישראל לאמר השמר מעבר המקום הזה כי שם ארם נחתים׃ 9
Basi huyo mtu wa Mungu akamtuma kwa mfalme wa Israeli, akisema, “Kuwa makini usipite ile sehemu, kwa kuwa ndipo Washamu wanakoshukia hapo.”
וישלח מלך ישראל אל המקום אשר אמר לו איש האלהים והזהירה ונשמר שם לא אחת ולא שתים׃ 10
Mfalme wa Israeli akatuma mjumbe kwenda pale sehemu ambayo mtu wa Mungu alipaongelea na kumtahadharisha. Zaidi ya mara moja au mbili, wakati mfalme alipoenda pale, alikuwa kwenye ulinzi wake.
ויסער לב מלך ארם על הדבר הזה ויקרא אל עבדיו ויאמר אליהם הלוא תגידו לי מי משלנו אל מלך ישראל׃ 11
Huyo mfalme wa Shamu alikasirishwa kuhusu haya maonyo, na akawaita watumishi wake na kuwaambia, “Je hamtaniambia ni nani miongoni mwetu aliye upande wa Israeli?”
ויאמר אחד מעבדיו לוא אדני המלך כי אלישע הנביא אשר בישראל יגיד למלך ישראל את הדברים אשר תדבר בחדר משכבך׃ 12
Hivyo mmoja wa watumishi wake akasema, “Hapana, bwana wangu, mfalme, kwa ajili ya Elisha yule nabii katika Israeli humwambia yule mfalme wa Israeli maneno ambayo uyaongeayo kwenye kitanda chako cha kulala!”
ויאמר לכו וראו איכה הוא ואשלח ואקחהו ויגד לו לאמר הנה בדתן׃ 13
Yule mfalme akajibu, “Nenda na uone Elisha alipo hivyo naweza kutuma watu na kumkamata.” Akaambiwa, “Tazama yuko Dothani.”
וישלח שמה סוסים ורכב וחיל כבד ויבאו לילה ויקפו על העיר׃ 14
Kwa hiyo yule mfalme akatuma farasi kwenda Donathi, magari ya farasi, na jeshi kubwa. Wakaja usiku na kuzunguka ule mji.
וישכם משרת איש האלהים לקום ויצא והנה חיל סובב את העיר וסוס ורכב ויאמר נערו אליו אהה אדני איכה נעשה׃ 15
Wakati yule mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka mapema na kutoka nje, kumbe, jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya farasi yameuzunguka mji. Mtumishi wake akamwabia, “Kumbe, bwana wangu! Tutafanya nini?”
ויאמר אל תירא כי רבים אשר אתנו מאשר אותם׃ 16
Elisha akajibu, “usiogope, wale walio na sisi ni zaidi kuliko wale walio nao.”
ויתפלל אלישע ויאמר יהוה פקח נא את עיניו ויראה ויפקח יהוה את עיני הנער וירא והנה ההר מלא סוסים ורכב אש סביבת אלישע׃ 17
Elisha akajibu na kusema, “Yahwe, nakuomba kwamba utamfungua macho yake ili kwamba aweze kuona.” Ndipo Yahwe alipofungua macho ya mtumishi, na akaona. Kumbe, ule mlima ulikuwa umejaa farasi na magari ya farasi ya moto yamemzunguka Elisha!
וירדו אליו ויתפלל אלישע אל יהוה ויאמר הך נא את הגוי הזה בסנורים ויכם בסנורים כדבר אלישע׃ 18
Wakati hao Washami walipomshukia chini, Elisha aliomba kwa Yahwe na kusema, “Uwapige hawa watu kwa upofu, nakuomba.” Hivyo Yahwe akawafanya vipofu, kama Elisha alivyoomba.
ויאמר אלהם אלישע לא זה הדרך ולא זה העיר לכו אחרי ואוליכה אתכם אל האיש אשר תבקשון וילך אותם שמרונה׃ 19
Kisha Elisha akawaambia Washami, “Hii njia sio, pia mji huu sio. Nifuateni mimi, na nitawaleta kwa yule mtu ambaye mnayemtafuta.” Ndipo akawaongoza kweda Samaria.
ויהי כבאם שמרון ויאמר אלישע יהוה פקח את עיני אלה ויראו ויפקח יהוה את עיניהם ויראו והנה בתוך שמרון׃ 20
Hata walipokwisha kufika Samaria, Elisha akasema, “Yahwe, fungua macho ya hawa watu ili waweze kuona.” Yahwe akawafungua macho yao na wakaona, na kumbe, walikuwa katikati ya mji wa Samaria.
ויאמר מלך ישראל אל אלישע כראתו אותם האכה אכה אבי׃ 21
Yule mfalme wa Israeli akamwambia Elisha, wakati alipowaona, “Baba yangu, niwaue? Niwaue?”
ויאמר לא תכה האשר שבית בחרבך ובקשתך אתה מכה שים לחם ומים לפניהם ויאכלו וישתו וילכו אל אדניהם׃ 22
Elisha akajibu, “Usiwaue. Ungeweza kuwaua wale ambao uliokuwa umewachukua mateka kwa upanga na upinde wako? Weka mkate na maji mbele yao, ili kwamba waweze kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.”
ויכרה להם כרה גדולה ויאכלו וישתו וישלחם וילכו אל אדניהם ולא יספו עוד גדודי ארם לבוא בארץ ישראל׃ 23
Ndipo mfalme akaandaa chakula kingi kwa ajili yao, na wakati walipokula na kunywa, akawapeleka mbali, na walirudi kwa bwana wao. Lile kundi la jeshi la Wasahami halikurudi kwa mda mrefu katika nchi ya Israeli.
ויהי אחרי כן ויקבץ בן הדד מלך ארם את כל מחנהו ויעל ויצר על שמרון׃ 24
Baadaye baada ya huyu Ben Hadadi mfalme wa Shamu kukusanya majeshi yake yote na kuiteka Samaria na kuizingira.
ויהי רעב גדול בשמרון והנה צרים עליה עד היות ראש חמור בשמנים כסף ורבע הקב חרייונים בחמשה כסף׃ 25
Hivyo kulikuwa na njaa kubwa katika Samaria. Kumbe, wakauzingira hadi kichwa cha punda kilipouzwa kwa vipande themanini vya fedha, na sehemu ya nne ya sehemu ya kibaba cha kinyesi cha njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
ויהי מלך ישראל עבר על החמה ואשה צעקה אליו לאמר הושיעה אדני המלך׃ 26
Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa akipita karibu na ukuta, mwanamke mmoka akamlilia akisema, “Nisaidie, bwana wangu, mfalme.”
ויאמר אל יושעך יהוה מאין אושיעך המן הגרן או מן היקב׃ 27
Akasema, “Kama Yahwe hawezi kukusaidia, je nitakusaidiaje? je kuna kitu chochote kinakuja kutoka sehemu ya kupuria nafaka au shinikizoni?”
ויאמר לה המלך מה לך ותאמר האשה הזאת אמרה אלי תני את בנך ונאכלנו היום ואת בני נאכל מחר׃ 28
Mfalme akaendelea, “Nini kinakusumbua?” Akajibu, “Huyu mwanamke ameniambia, 'Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla leo, na tutamla wakwangu kesho.”
ונבשל את בני ונאכלהו ואמר אליה ביום האחר תני את בנך ונאכלנו ותחבא את בנה׃ 29
Hivyo tulimchemsha mtoto wangu na kumla, na siku ya pili yake nikamwambia, “Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla, lakini alikuwa amemficha mtoto wake.”
ויהי כשמע המלך את דברי האשה ויקרע את בגדיו והוא עבר על החמה וירא העם והנה השק על בשרו מבית׃ 30
Basi mfalme aliposikia yale maneno ya yule mwanamke, akayachana mavazi yake (sasa alikuwa akitembelea kwenye ukuta), na watu wakatazama na kuona kwamba alikuwa amevaa nguo ya gunia chini, dhidi ya ngozi yake.
ויאמר כה יעשה לי אלהים וכה יוסף אם יעמד ראש אלישע בן שפט עליו היום׃ 31
Kisha akasema, “Mungu afanye hivyo kwangu, na zaidi pia, kama kichwa cha Elisha mwana wa Shafati kitabaki juu yake leo.”
ואלישע ישב בביתו והזקנים ישבים אתו וישלח איש מלפניו בטרם יבא המלאך אליו והוא אמר אל הזקנים הראיתם כי שלח בן המרצח הזה להסיר את ראשי ראו כבא המלאך סגרו הדלת ולחצתם אתו בדלת הלוא קול רגלי אדניו אחריו׃ 32
Basi Elisha alikuwa ameketi kwenye nyumba yake, na wazee walikuwa wamekaa pamoja naye. Yule mfalme akamtuma mtu wa mbele yake, lakini wakati mjumbe alipokuja kwa Elisha, akawaambia wazee, “Ona jinsi huyu mwana wa muuaji alivytumwa kuchukua kichwa changu? Tazama, wakati yule mjumbe atakapokuja, funga mlango, na uushikilie huo mlango funga dhidi yake asiingie. Je sio sauti ya bwana wake nyuma mguuni pake?”
עודנו מדבר עמם והנה המלאך ירד אליו ויאמר הנה זאת הרעה מאת יהוה מה אוחיל ליהוה עוד׃ 33
Wakati alipokuwa bado akiongea pamoja nao, kumbe, yule mjumbe alishuka kwake. Mfalme akasema, “Kumbe, masumbuko haya yatoka kwa Yahwe. Kwa nini nimsubiri Yahwe tena?”

< מלכים ב 6 >