< שמואל א 20 >

ויברח דוד מנוית ברמה ויבא ויאמר לפני יהונתן מה עשיתי מה עוני ומה חטאתי לפני אביך כי מבקש את נפשי׃ 1
Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akaenda na kumwambia Yonathani, “Nimefanya nini? Uovu wangu ni upi? Dhambi yangu ni ipi kwa baba yako, inayofanya atafute kuutoa uhai wangu.”
ויאמר לו חלילה לא תמות הנה לו עשה אבי דבר גדול או דבר קטן ולא יגלה את אזני ומדוע יסתיר אבי ממני את הדבר הזה אין זאת׃ 2
Yonathani akamwambia Daudi, “La hasha; hautakufa. Baba yangu hafanyi jambo kubwa wala dogo bila kunijulisha. Kwa nini inamlazimu baba yangu anifiche jambo hili? La, siyo hivyo?”
וישבע עוד דוד ויאמר ידע ידע אביך כי מצאתי חן בעיניך ויאמר אל ידע זאת יהונתן פן יעצב ואולם חי יהוה וחי נפשך כי כפשע ביני ובין המות׃ 3
Bado Daudi aliapa tena na akasema, “Baba yako anajua wazi kwamba nimepata kibali machoni pako. Pengine anasema, 'Asije Yonathani akajua jambo hili, labda atahuzunika.' Lakini kweli kama BWANA aishivyo, kama wewe uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti.”
ויאמר יהונתן אל דוד מה תאמר נפשך ואעשה לך׃ 4
Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Lolote utakalosema, nitakufanyia.”
ויאמר דוד אל יהונתן הנה חדש מחר ואנכי ישב אשב עם המלך לאכול ושלחתני ונסתרתי בשדה עד הערב השלשית׃ 5
Daudi akamwambia Yonathani, “Kesho ni siku ya mwezi mpya, na inanibidi kukaa na kula pamoja na mfalme. Lakini acha niende, ili niweze kujificha katika shamba hadi siku ya tatu jioni.
אם פקד יפקדני אביך ואמרת נשאל נשאל ממני דוד לרוץ בית לחם עירו כי זבח הימים שם לכל המשפחה׃ 6
Baba yako akinikosa kabisa, ndipo utasema, 'Daudi aliniomba kwa msisitizo ruhusa aondoke kwenda mjini kwake Bethlehemu; kwa sababu huko ni kipindi cha utoaji wa dhabihu ya mwaka kwa familia yao yote.'
אם כה יאמר טוב שלום לעבדך ואם חרה יחרה לו דע כי כלתה הרעה מעמו׃ 7
Kama atasema kuwa ni vyema, 'basi mtumishi wako atakuwa na amani. Lakini kama atakasirika sana, ndipo utajua kwamba ameamua kunitendea uovu.
ועשית חסד על עבדך כי בברית יהוה הבאת את עבדך עמך ואם יש בי עון המיתני אתה ועד אביך למה זה תביאני׃ 8
Kwa hiyo, umtendee wema mtumishi wako. Kwa maana umemweka mtumishi katika agano la BWANA pamoja na wewe. Lakini kama kuna dhambi ndani yangu, wewe mwenyewe uniuwe; maana kwa nini basi unipeleke kwa baba yako?”
ויאמר יהונתן חלילה לך כי אם ידע אדע כי כלתה הרעה מעם אבי לבוא עליך ולא אתה אגיד לך׃ 9
Yonathani akasema, “La hasha! Ikiwa ninajua kwamba baba ameamua baya likupate, siwezi kukuambia?”
ויאמר דוד אל יהונתן מי יגיד לי או מה יענך אביך קשה׃ 10
Ndipo Daudi akamwambia Yonathani, “Ni nani ataniambia ikiwa imetokea, baba yako akakujibu kwa ukali?”
ויאמר יהונתן אל דוד לכה ונצא השדה ויצאו שניהם השדה׃ 11
Yonathani akamwambia Daudi, “Njoo, hebu twende huko shambani.” Ndipo wote wakaondoka kwenda shambani.
ויאמר יהונתן אל דוד יהוה אלהי ישראל כי אחקר את אבי כעת מחר השלשית והנה טוב אל דוד ולא אז אשלח אליך וגליתי את אזנך׃ 12
Yonathani akamwambia Daudi, “Na BWANA, Mungu wa Israeli, awe shahidi. Kesho muda kama huu, nitakuwa nimemuuliza baba yangu, au siku ya tatu, tazama, ikiwa kutakuwa na jambo zuri upande wa Daudi; je, nisikutumie taarifa na kulidhihirisha kwako?
כה יעשה יהוה ליהונתן וכה יסיף כי ייטב אל אבי את הרעה עליך וגליתי את אזנך ושלחתיך והלכת לשלום ויהי יהוה עמך כאשר היה עם אבי׃ 13
Na kama ikimpendeza baba yangu akufanyie madhara, Basi BWANA ayafanye hayo kwa Yonathani na kuzidi ikiwa sitakujulisha jambo na kukupeleka mbali, ili kwamba uende kwa amani. Na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa na baba yangu.
ולא אם עודני חי ולא תעשה עמדי חסד יהוה ולא אמות׃ 14
Kama bado nikiwa hai, hautanionesha uaminifu wa agano la BWANA, kwamba siwezi kufa?
ולא תכרת את חסדך מעם ביתי עד עולם ולא בהכרת יהוה את איבי דוד איש מעל פני האדמה׃ 15
Na usivunje kabisa uaminifu wako wa agano kati yako na nyumba yangu, hata wakati BWANA atakapowaodoa kila mmoja wa adui za Daudi kutoka uso wa dunia.”
ויכרת יהונתן עם בית דוד ובקש יהוה מיד איבי דוד׃ 16
Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi na kusema, “Naye BWANA atawaondoa maadui wa Daudi.”
ויוסף יהונתן להשביע את דוד באהבתו אתו כי אהבת נפשו אהבו׃ 17
Yonathani akamtaka Daudi aape tena kwa sababu ya upendo aliokuwa nao juu yake, kwa sababu alimpenda kama alivyopenda roho yake mwenyewe.
ויאמר לו יהונתן מחר חדש ונפקדת כי יפקד מושבך׃ 18
Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni siku ya mwezi mpya. Hautakuwapo, kwa sababu kiti chako kitakuwa wazi.
ושלשת תרד מאד ובאת אל המקום אשר נסתרת שם ביום המעשה וישבת אצל האבן האזל׃ 19
Utakapokuwa umekaa huko siku tatu, uende upesi hadi mahala ulipojificha mara ya kwanza, wakati shughuli ikifanyika, na ukaye karibu jiwe Ezeli.
ואני שלשת החצים צדה אורה לשלח לי למטרה׃ 20
Nitatupa mishale mitatu pembeni mwa jiwe, kama vile ninalenga kitu fulani.
והנה אשלח את הנער לך מצא את החצים אם אמר אמר לנער הנה החצים ממך והנה קחנו ובאה כי שלום לך ואין דבר חי יהוה׃ 21
Kisha nitamtuma kijana wangu na kumwambia, 'Nenda utafute hiyo mishale.' Kama nitamwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko upande huu wa kwako; kaichukue,” ndipo uje; maana hapo kutakuwa na usalama kwako na siyo madhara, kama BWANA aishivyo.
ואם כה אמר לעלם הנה החצים ממך והלאה לך כי שלחך יהוה׃ 22
“Lakini kama nikimwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko mbele yako,' ndipo utakapokwenda zako, maana BWANA ametaka uende zako.
והדבר אשר דברנו אני ואתה הנה יהוה ביני ובינך עד עולם׃ 23
Kulingana na makubaliano ambayo mimi na wewe tumeongea, angalia, BWANA yupo kati yangu na wewe milele.'”
ויסתר דוד בשדה ויהי החדש וישב המלך על הלחם לאכול׃ 24
Kwa hiyo Daudi akajificha mle shambani. Pindi mwezi ulipoandama, mfalme aliketi chini ale chakula.
וישב המלך על מושבו כפעם בפעם אל מושב הקיר ויקם יהונתן וישב אבנר מצד שאול ויפקד מקום דוד׃ 25
Mfalme alikaa juu ya kiti chake, kama kawaida kwenye kiti karibu na ukuta. Yonathani alisimama wima, na Abneri alikaa ubavuni mwa Sauli. Lakini nafasi ya Daudi ilikuwa wazi.
ולא דבר שאול מאומה ביום ההוא כי אמר מקרה הוא בלתי טהור הוא כי לא טהור׃ 26
Hata hivyo Sauli hakusema kitu siku hiyo, kwa sababu alifikiri, “Kuna jambo limempata Daudi. Hayuko safi; hakika hayuko safi.”
ויהי ממחרת החדש השני ויפקד מקום דוד ויאמר שאול אל יהונתן בנו מדוע לא בא בן ישי גם תמול גם היום אל הלחם׃ 27
Lakini siku ya pili, siku moja baada ya mwandamo wa mwezi, bado nafasi ya Daudi ilikuwa tupu. Ndipo Sauli akamuuliza Yonathani mwanaye, “Kwa nini mwana wa Yese hakuja kwenye chakula, jana na hata leo?”
ויען יהונתן את שאול נשאל נשאל דוד מעמדי עד בית לחם׃ 28
Yonathani akamjibu Sauli, “Daudi aliomba kwangu ruhusa kwa dhati ili aende Bethlehemu.
ויאמר שלחני נא כי זבח משפחה לנו בעיר והוא צוה לי אחי ועתה אם מצאתי חן בעיניך אמלטה נא ואראה את אחי על כן לא בא אל שלחן המלך׃ 29
Alisema, 'Tafadhali niruhusu niende. Maana familia yetu wanayo dhabihu huko mjini, na kaka yangu ameniagiza niwe huko. Basi kama nimepata kibali machoni pako, tafadhali niruhusu niende nikawaone kaka zangu.' Hakuja kwenye meza ya mfalme kwa sababu hii.”
ויחר אף שאול ביהונתן ויאמר לו בן נעות המרדות הלוא ידעתי כי בחר אתה לבן ישי לבשתך ולבשת ערות אמך׃ 30
Ndipo hasira ya Sauli iliwaka juu ya Yonathani, na akamwambia, “Wee mwana wa mwanamke mkaidi na muasi! Wadhani kwamba sijui kuwa umemchagua Mwana wa Yese kwa ajili ya aibu yako, na kwa aibu ya uchi wa mama yako?
כי כל הימים אשר בן ישי חי על האדמה לא תכון אתה ומלכותך ועתה שלח וקח אתו אלי כי בן מות הוא׃ 31
Kwa kuwa mwana wa Yese anaishi duniani, siyo wewe wala ufalme wako utakaoimarika. Sasa basi, tuma watu wamlete kwangu, kwa sababu inampasa kufa.”
ויען יהונתן את שאול אביו ויאמר אליו למה יומת מה עשה׃ 32
Yonathani akamjibu Sauli baba yake, “Kwa sababu gani inampasa kuuwawa? Amefanya nini?”
ויטל שאול את החנית עליו להכתו וידע יהונתן כי כלה היא מעם אביו להמית את דוד׃ 33
Ndipo Sauli akamtupia mkuki apate kumuua. Kwa hiyo Yonatani akatambua kwamba baba yake alinuia kumuua Daudi.
ויקם יהונתן מעם השלחן בחרי אף ולא אכל ביום החדש השני לחם כי נעצב אל דוד כי הכלמו אביו׃ 34
Yonathani alitoka mezani akiwa na hasira kali bila kula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
ויהי בבקר ויצא יהונתן השדה למועד דוד ונער קטן עמו׃ 35
Ikawa asubuhi, Yonathani akaenda huko shambani kama walivyoahidiana na Daudi, akiwa pamoja na kijana wake.
ויאמר לנערו רץ מצא נא את החצים אשר אנכי מורה הנער רץ והוא ירה החצי להעברו׃ 36
Akamwambia yule kijana wake, “Kimbia utafute ile mishale niliyoitupa.” Na kijana alikimbia, akatupa mshale mwingine mbele yake.
ויבא הנער עד מקום החצי אשר ירה יהונתן ויקרא יהונתן אחרי הנער ויאמר הלוא החצי ממך והלאה׃ 37
Kijana alipofika katika eneo ambapo mshale ulitua, ule alioutuma Yonathani, akamwita tena kijana, na kusema, “Huo mshale hauko mbele yako?”
ויקרא יהונתן אחרי הנער מהרה חושה אל תעמד וילקט נער יהונתן את החצי ויבא אל אדניו׃ 38
Kisha Yonathani akamwita yule kijana, “Upesi, harakisha, usikawie!” Hivyo kijana wa Yonathani akaikusanya mishale na kurudi kwa bwana wake.
והנער לא ידע מאומה אך יהונתן ודוד ידעו את הדבר׃ 39
Lakini huyo kijana hakujua lolote. Ni Yonathani na Daudi tu ndio walijua habari yenyewe.
ויתן יהונתן את כליו אל הנער אשר לו ויאמר לו לך הביא העיר׃ 40
Yonathani akampa kijana wake silaha na kumwambia, “Nenda, uzipeleke mjini.”
הנער בא ודוד קם מאצל הנגב ויפל לאפיו ארצה וישתחו שלש פעמים וישקו איש את רעהו ויבכו איש את רעהו עד דוד הגדיל׃ 41
Punde tu kijana alipoondoka, Daudi akasimama kutokea upande wa kusini, akiwa amelala kifudifudi, akainama mara tatu. Walibusiana wao kwa wao na wote wakalia kwa pamoja, Daudi akilia zaidi.
ויאמר יהונתן לדוד לך לשלום אשר נשבענו שנינו אנחנו בשם יהוה לאמר יהוה יהיה ביני ובינך ובין זרעי ובין זרעך עד עולם ויקם וילך ויהונתן בא העיר׃ 42
Yonathani akamwambia Daudi, “Nenda kwa amani, kwa sababu wote tumeapa kwa jina la BWANA na tulisema, 'BWANA awe kati yangu na wewe, na awe kati ya uzao wangu na uzao wako, milele.'” Kisha Daudi alisimama na akaondoka, na Yonathani akarudi mjini.

< שמואל א 20 >