< ישעה 41 >

הַחֲרִישׁוּ אֵלַי אִיִּים וּלְאֻמִּים יַחֲלִיפוּ כֹחַ יִגְּשׁוּ אָז יְדַבֵּרוּ יַחְדָּו לַמִּשְׁפָּט נִקְרָֽבָה׃ 1
''Sikilizeni mbele yangu kwa ukimya, enyi mkao pwani; wacha mataifa yapate nguvu kwa upya; waache waje karibu na kuzungumza; na tusogee karibu tujadili mgogoro.
מִי הֵעִיר מִמִּזְרָח צֶדֶק יִקְרָאֵהוּ לְרַגְלוֹ יִתֵּן לְפָנָיו גּוֹיִם וּמְלָכִים יַרְדְּ יִתֵּן כֶּֽעָפָר חַרְבּוֹ כְּקַשׁ נִדָּף קַשְׁתּֽוֹ׃ 2
Nani aliyechochea juu mmoja kutoka mashariki, anamuita katika haki yake kwenye huduma yake? Amemkabidhi mataifa juu yake ili amsaidie yeye kuwaangamiza wafalme. Aliwajeuza kuwa mavumbi kwa neno lake, kama upepo unaovuma kwenye mabua kwa upinde wake.
יִרְדְּפֵם יַעֲבוֹר שָׁלוֹם אֹרַח בְּרַגְלָיו לֹא יָבֽוֹא׃ 3
Aliwachukuwa wao na kuwapitisha salama, katika njia nyepesi ambayo miguu yake imegusa shida.
מִֽי־פָעַל וְעָשָׂה קֹרֵא הַדֹּרוֹת מֵרֹאשׁ אֲנִי יְהוָה רִאשׁוֹן וְאֶת־אַחֲרֹנִים אֲנִי־הֽוּא׃ 4
Ni nani aliyeyafanya na kukamilisha matendo haya? Ni nanialiyechagua kizazi kutoka mwanzo? Mimi, Yahwe ni mwanzo na mwisho, mimi ndiye.
רָאוּ אִיִּים וְיִירָאוּ קְצוֹת הָאָרֶץ יֶחֱרָדוּ קָרְבוּ וַיֶּאֱתָיֽוּן׃ 5
Visiwa vimeona na kuogopa; miisho ya dunia yatetemeka; walikaribia n kuja.
אִישׁ אֶת־רֵעֵהוּ יַעְזֹרוּ וּלְאָחִיו יֹאמַר חֲזָֽק׃ 6
Kila mmoja amsaidie jirani yake, na kila mmoja asemezane na mwenzake, 'Kuwa mfariji;
וַיְחַזֵּק חָרָשׁ אֶת־צֹרֵף מַחֲלִיק פַּטִּישׁ אֶת־הוֹלֶם פָּעַם אֹמֵר לַדֶּבֶק טוֹב הוּא וַיְחַזְּקֵהוּ בְמַסְמְרִים לֹא יִמּֽוֹט׃ 7
Hivyo basi seremala anamfariji mfua dhahabu, na yule anayefanya kazi kwa kutumia nyundo anamfariji anayefanya kazi kwa chuma, akisema kwa msemo wa kurehemu, ''Ni mizuri; Naye ataupigilia kwa makini misumari ili isipinduke.
וְאַתָּה יִשְׂרָאֵל עַבְדִּי יַעֲקֹב אֲשֶׁר בְּחַרְתִּיךָ זֶרַע אַבְרָהָם אֹהֲבִֽי׃ 8
Lakini wewe, Israeli mtumishi wangu, Yakobo niliyekuchagua, mtoto wa Ibrahimu rafiki yangu,
אֲשֶׁר הֶחֱזַקְתִּיךָ מִקְצוֹת הָאָרֶץ וּמֵאֲצִילֶיהָ קְרָאתִיךָ וָאֹמַר לְךָ עַבְדִּי־אַתָּה בְּחַרְתִּיךָ וְלֹא מְאַסְתִּֽיךָ׃ 9
wewe ambaye ninakurudisha kutoka miisho ya nchi, na ambaye niliyekuita kutoka sehemu ya mbali, na kwako niliyekuambia, 'Wewe ni mtumishi wangu; 'Nimekuchagua wewe na sijakukataa.
אַל־תִּירָא כִּי עִמְּךָ־אָנִי אַל־תִּשְׁתָּע כִּֽי־אֲנִי אֱלֹהֶיךָ אִמַּצְתִּיךָ אַף־עֲזַרְתִּיךָ אַף־תְּמַכְתִּיךָ בִּימִין צִדְקִֽי׃ 10
Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.
הֵן יֵבֹשׁוּ וְיִכָּלְמוּ כֹּל הַנֶּחֱרִים בָּךְ יִֽהְיוּ כְאַיִן וְיֹאבְדוּ אַנְשֵׁי רִיבֶֽךָ׃ 11
Tazama, watakuwa na aibu na hawataheshimiwa, wale wote waliokuwa na hasira na wewe; watakuwa si kitu na watatokomea, wale watakao kupinga wewe.
תְּבַקְשֵׁם וְלֹא תִמְצָאֵם אַנְשֵׁי מַצֻּתֶךָ יִהְיוּ כְאַיִן וּכְאֶפֶס אַנְשֵׁי מִלְחַמְתֶּֽךָ׃ 12
Utawatafuta na wala hautawapata wale wanaopingana na wewe; wale wafanyao vita dhidi yako watakuwa kama si kitu, si kitu kabisa.
כִּי אֲנִי יְהוָה אֱלֹהֶיךָ מַחֲזִיק יְמִינֶךָ הָאֹמֵר לְךָ אַל־תִּירָא אֲנִי עֲזַרְתִּֽיךָ׃ 13
Maana mimi Yahwe Mungu wako, nitawashika mkono wako wa kiume, nikikuambia wewe, 'Usiogope; Nitakusaidia wewe.
אַל־תִּֽירְאִי תּוֹלַעַת יַֽעֲקֹב מְתֵי יִשְׂרָאֵל אֲנִי עֲזַרְתִּיךְ נְאֻם־יְהוָה וְגֹאֲלֵךְ קְדוֹשׁ יִשְׂרָאֵֽל׃ 14
Usiogope, Yakobo wewe mdudu, na enyi watu wa Israeli; Nitawasaidia''- hili ni tamko la Yahwe, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli.
הִנֵּה שַׂמְתִּיךְ לְמוֹרַג חָרוּץ חָדָשׁ בַּעַל פִּֽיפִיּוֹת תָּדוּשׁ הָרִים וְתָדֹק וּגְבָעוֹת כַּמֹּץ תָּשִֽׂים׃ 15
Tazama, ninakufanya wewe kuwa chombo kikali cha kuparulia chenye makali pande mbili; utaparua milima na kuiponda; utafanya vilima kama makapi.
תִּזְרֵם וְרוּחַ תִּשָּׂאֵם וּסְעָרָה תָּפִיץ אוֹתָם וְאַתָּה תָּגִיל בַּֽיהוָה בִּקְדוֹשׁ יִשְׂרָאֵל תִּתְהַלָּֽל׃ 16
Utawatawanya wao, na upepo utawabeba na kuwapeka mbali; upepo utawatanya wao. Utashanglia katika Yahwe, utashangiliakatika mtakatifu wa Israeli
הָעֲנִיִּים וְהָאֶבְיוֹנִים מְבַקְשִׁים מַיִם וָאַיִן לְשׁוֹנָם בַּצָּמָא נָשָׁתָּה אֲנִי יְהוָה אֶעֱנֵם אֱלֹהֵי יִשְׂרָאֵל לֹא אֶעֶזְבֵֽם׃ 17
Waliodhulumiwa na masikini wanatafuta maji, lakini hakuna kitu, ndimi zao zimekauka kwa kiu; Mimi Yahwe, nitajibu maombi yao; Mimi Mungu wa Israeli, sitawacha wao.
אֶפְתַּח עַל־שְׁפָיִים נְהָרוֹת וּבְתוֹךְ בְּקָעוֹת מַעְיָנוֹת אָשִׂים מִדְבָּר לַאֲגַם־מַיִם וְאֶרֶץ צִיָּה לְמוֹצָאֵי מָֽיִם׃ 18
Nitatengeneza mikondo ya maji kushusha chini, na chemichem katikati ya mabonde; nitalifanya jangwa kuwa kisima cha maji, na aridhi kavu kuwa chemichem ya maji.
אֶתֵּן בַּמִּדְבָּר אֶרֶז שִׁטָּה וַהֲדַס וְעֵץ שָׁמֶן אָשִׂים בָּעֲרָבָה בְּרוֹשׁ תִּדְהָר וּתְאַשּׁוּר יַחְדָּֽו׃ 19
Katika jangwa nitapanda mierezi, mshita, mhadisi, na mti wa mizeituni. Nitaotesha mberoshi katika uwazi wa jangwa, pamoja na mbono nitapanda mberoshi kitika jangwa lililowazi.
לְמַעַן יִרְאוּ וְיֵדְעוּ וְיָשִׂימוּ וְיַשְׂכִּילוּ יַחְדָּו כִּי יַד־יְהוָה עָשְׂתָה זֹּאת וּקְדוֹשׁ יִשְׂרָאֵל בְּרָאָֽהּ׃ 20
Nitayafanya haya ili waweze kuona, kutambua na kuelewa kwa pamoja, kwamba mkono wa Yahwe umetenda haya, kama Mtakatifu wa Israeli aliyeliumba.
קָרְבוּ רִֽיבְכֶם יֹאמַר יְהוָה הַגִּישׁוּ עֲצֻמוֹתֵיכֶם יֹאמַר מֶלֶךְ יַעֲקֹֽב׃ 21
Wakilisha keshi yako, '' asema Yahwe; ''wakilisha hoja zenu nzuri kwa sanamu yenu,'' asema Mfalme wa Yakobo.
יַגִּישׁוּ וְיַגִּידוּ לָנוּ אֵת אֲשֶׁר תִּקְרֶינָה הָרִאשֹׁנוֹת ׀ מָה הֵנָּה הַגִּידוּ וְנָשִׂימָה לִבֵּנוּ וְנֵדְעָה אַחֲרִיתָן אוֹ הַבָּאוֹת הַשְׁמִיעֻֽנוּ׃ 22
Waache walete hoja zao wenyewe; waache waje mbele na watutangazie sisi nini kitakachotokea, ili tuweze kuelewa haya mambo vizuri. Tuawaache watupe tamko mapema, ili tuweze kulitafakari na tuweze kujua n kwa jinsi gani litatimia.
הַגִּידוּ הָאֹתִיּוֹת לְאָחוֹר וְנֵדְעָה כִּי אֱלֹהִים אַתֶּם אַף־תֵּיטִיבוּ וְתָרֵעוּ וְנִשְׁתָּעָה ונרא וְנִרְאֶה יַחְדָּֽו׃ 23
Wajulishe kitu kuhusu baadaye, ili tujue kuwa ninyi ni miungu; fanya kitu kizuri au kibaya, ambacho kitatutisha na kutushangaza.
הֵן־אַתֶּם מֵאַיִן וּפָעָלְכֶם מֵאָפַע תּוֹעֵבָה יִבְחַר בָּכֶֽם׃ 24
Tazama sanamu zenu si kitu na matendo yenu si kitu; aliyewachagua ni machukizo.
הַעִירוֹתִי מִצָּפוֹן וַיַּאת מִמִּזְרַח־שֶׁמֶשׁ יִקְרָא בִשְׁמִי וְיָבֹא סְגָנִים כְּמוֹ־חֹמֶר וּכְמוֹ יוֹצֵר יִרְמָס־טִֽיט׃ 25
Nimemnyanyua mmoja kutoka kaskazini, naye amekuja kutoka mawio ya jua nimemchagua yeye alitajae jina langu, na atawakanyaga viongozi kama matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo.
מִֽי־הִגִּיד מֵרֹאשׁ וְנֵדָעָה וּמִלְּפָנִים וְנֹאמַר צַדִּיק אַף אֵין־מַגִּיד אַף אֵין מַשְׁמִיעַ אַף אֵין־שֹׁמֵעַ אִמְרֵיכֶֽם׃ 26
Ni nani aliyetangaza hili tangu mwanzo, ili tuweze kujua? na kabla ya mda, ili tuseme, ''Yuko sawasawa''? Kweli hakuna hata mmoja aliyekiri hili, ndio hakuna hata mmoja aliyekusikia ukisema chochote.
רִאשׁוֹן לְצִיּוֹן הִנֵּה הִנָּם וְלִירוּשָׁלַ͏ִם מְבַשֵּׂר אֶתֵּֽן׃ 27
Kwanza nilizungumza na Sayuni, ''Tazama hapo walipo;'' Nimemtuma mhubiri Yerusalemu.
וְאֵרֶא וְאֵין אִישׁ וּמֵאֵלֶּה וְאֵין יוֹעֵץ וְאֶשְׁאָלֵם וְיָשִׁיבוּ דָבָֽר׃ 28
Nilipoangalia, hakuna hata mmoja, hakuna hata miongoni mwao ambaye anaweza kutoa ushauri mzuri, nani, lini nimulize, awezaye kunijibu neno.
הֵן כֻּלָּם אָוֶן אֶפֶס מַעֲשֵׂיהֶם רוּחַ וָתֹהוּ נִסְכֵּיהֶֽם׃ 29
Tazama, matendo yao si kitu; sanamu zao za chuma zilizotupwa ni upepo na utupu.

< ישעה 41 >