< צפניה 3 >
הוֹי מֹרְאָה וְנִגְאָלָה הָעִיר הַיּוֹנָֽה׃ | 1 |
Ole kwa mji ulioasi! Mji wenye vurugu umenajisiwa.
לֹא שָֽׁמְעָה בְּקוֹל לֹא לָקְחָה מוּסָר בַּֽיהֹוָה לֹא בָטָחָה אֶל־אֱלֹהֶיהָ לֹא קָרֵֽבָה׃ | 2 |
Haukuisikiliza sauti ya Mungu, wala haukupokea masahihisho kutoka kwa Yahwe. Hakumtumaini Yahwe na hatamkaribia Mungu wake.
שָׂרֶיהָ בְקִרְבָּהּ אֲרָיוֹת שֹׁאֲגִים שֹׁפְטֶיהָ זְאֵבֵי עֶרֶב לֹא גָרְמוּ לַבֹּֽקֶר׃ | 3 |
Wafalme wao ni simba wanaounguruma miongoni mwao. Waamuzi wao ni mbwa mwitu wa jioni wasiobakiza kitu ambacho kitakuwa kimemung'unywa asubuhi yake.
נְבִיאֶיהָ פֹּֽחֲזִים אַנְשֵׁי בֹּֽגְדוֹת כֹּהֲנֶיהָ חִלְּלוּ־קֹדֶשׁ חָמְסוּ תּוֹרָֽה׃ | 4 |
Manabii wake wanakiburi na wanaume wasaliti. Makuhani wake wamepanajisi mahali patakatifu na wameifanyia vurugu sheria.
יְהֹוָה צַדִּיק בְּקִרְבָּהּ לֹא יַעֲשֶׂה עַוְלָה בַּבֹּקֶר בַּבֹּקֶר מִשְׁפָּטוֹ יִתֵּן לָאוֹר לֹא נֶעְדָּר וְלֹא־יוֹדֵעַ עַוָּל בֹּֽשֶׁת׃ | 5 |
Yahwe ni mwenye haki miongoni mwao. Hawezi kufanya makosa. Kila asubuhi husimamia haki yake! Haitafichika nuruni, hata hivyo watu wasio wenye haki hawajui kuona aibu.
הִכְרַתִּי גוֹיִם נָשַׁמּוּ פִּנּוֹתָם הֶחֱרַבְתִּי חוּצוֹתָם מִבְּלִי עוֹבֵר נִצְדּוּ עָרֵיהֶם מִבְּלִי־אִישׁ מֵאֵין יוֹשֵֽׁב׃ | 6 |
Nimeyaharibu mataifa; ngome zao zimeharibiwa. Nimeifanya mitaa yao magofu, hivyo hakuna hata mmoja anayepitia kwake. Miji yao imeharibiwa kwa hiyo hakuna mtu anayeikaa.
אָמַרְתִּי אַךְ־תִּֽירְאִי אוֹתִי תִּקְחִי מוּסָר וְלֹֽא־יִכָּרֵת מְעוֹנָהּ כֹּל אֲשֶׁר־פָּקַדְתִּי עָלֶיהָ אָכֵן הִשְׁכִּימוּ הִשְׁחִיתוּ כֹּל עֲלִילוֹתָֽם׃ | 7 |
Nikasema, 'Hakika mtaniogopa mimi. Pokeeni masahihisho na msikatiliwe mbali kutoka kwenye miji yenu kwa yote yale niliyokuwa nimeyapanga kuyafanya kwenu.' Lakini walikuwa na shauku kuanza kila siku kwa kuharibu matendo yao yote.
לָכֵן חַכּוּ־לִי נְאֻם־יְהֹוָה לְיוֹם קוּמִי לְעַד כִּי מִשְׁפָּטִי לֶאֱסֹף גּוֹיִם לְקׇבְצִי מַמְלָכוֹת לִשְׁפֹּךְ עֲלֵיהֶם זַעְמִי כֹּל חֲרוֹן אַפִּי כִּי בְּאֵשׁ קִנְאָתִי תֵּאָכֵל כׇּל־הָאָֽרֶץ׃ | 8 |
Kwa hiyo ningojeni - hili ni tamko la Yahwe - mpaka siku ambayo nitainuka kwa ajili ya waathirika. Uaamuzi wangu nikuwakusanya mataifa, kuzikusanya falme, na kumwaga juu yao hasira yangu, uchungu wangu wote mkali, hivyo nchi yote itamezwa kwa moto wa hasira yangu.
כִּֽי־אָז אֶהְפֹּךְ אֶל־עַמִּים שָׂפָה בְרוּרָה לִקְרֹא כֻלָּם בְּשֵׁם יְהֹוָה לְעׇבְדוֹ שְׁכֶם אֶחָֽד׃ | 9 |
Ndipo nitawapa midomo safi watu, kuwaita wote kwa jina la Bwana kunitumikia wakisimama bega kwa bega.
מֵעֵבֶר לְנַהֲרֵי־כוּשׁ עֲתָרַי בַּת־פּוּצַי יוֹבִלוּן מִנְחָתִֽי׃ | 10 |
Kutoka ng'ambo ya mto Ethiopia waniabuduo - watu wangu waliotawanyika - wataleta dhabihu kwa sababu yangu.
בַּיּוֹם הַהוּא לֹא תֵבוֹשִׁי מִכֹּל עֲלִילֹתַיִךְ אֲשֶׁר פָּשַׁעַתְּ בִּי כִּי־אָז ׀ אָסִיר מִקִּרְבֵּךְ עַלִּיזֵי גַּאֲוָתֵךְ וְלֹא־תוֹסִפִי לְגׇבְהָה עוֹד בְּהַר קׇדְשִֽׁי׃ | 11 |
Katika siku hiyo hamtawekwa kwenye woga kwa matendo yenu yote ambayo mmeyafanya dhidi yangu, tangu wakati ule nitaondoa kutoka kwenu wale waliosherehekea fahari yenu, na kwa sababu hamtakuwa na muda mrefu kufanya majivuno juu ya mlima wangu mtakatifu.
וְהִשְׁאַרְתִּי בְקִרְבֵּךְ עַם עָנִי וָדָל וְחָסוּ בְּשֵׁם יְהֹוָֽה׃ | 12 |
Lakini nitawaacha kama wa chini zaidi na watu masikini, na mtapata kimbilio katika jina la Yahwe.
שְׁאֵרִית יִשְׂרָאֵל לֹֽא־יַעֲשׂוּ עַוְלָה וְלֹֽא־יְדַבְּרוּ כָזָב וְלֹֽא־יִמָּצֵא בְּפִיהֶם לְשׁוֹן תַּרְמִית כִּֽי־הֵמָּה יִרְעוּ וְרָבְצוּ וְאֵין מַחֲרִֽיד׃ | 13 |
Mkazi wa Israeli si muda mrefu hatafanya udhalimu au kusema uongo, na hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao; hivyo watalisha na kulala chini, na hakuna hata mmoja atakayewafanya kuogopa.”
רׇנִּי בַּת־צִיּוֹן הָרִיעוּ יִשְׂרָאֵל שִׂמְחִי וְעׇלְזִי בְּכׇל־לֵב בַּת יְרוּשָׁלָֽ͏ִם׃ | 14 |
Imba, binti Sayuni! Piga kelele, Israeli. Ufurahi na kushangilia kwa moyo wako wote, binti wa Yerusalemu.
הֵסִיר יְהֹוָה מִשְׁפָּטַיִךְ פִּנָּה אֹֽיְבֵךְ מֶלֶךְ יִשְׂרָאֵל ׀ יְהֹוָה בְּקִרְבֵּךְ לֹא־תִֽירְאִי רָע עֽוֹד׃ | 15 |
Yahwe ameiondoa hukumu yako; amewafukuzia mbali adui zako! Yahwe ni mfalme wa Israeli miongoni mwenu. Kamwe hamtamwogopa tena mwovu!
בַּיּוֹם הַהוּא יֵאָמֵר לִירֽוּשָׁלַ͏ִם אַל־תִּירָאִי צִיּוֹן אַל־יִרְפּוּ יָדָֽיִךְ׃ | 16 |
Katika siku hizo watasema kwa Yerusalemi, “Usiogope, Sayuni. Usiiache mikono yako ilegee.
יְהֹוָה אֱלֹהַיִךְ בְּקִרְבֵּךְ גִּבּוֹר יוֹשִׁיעַ יָשִׂישׂ עָלַיִךְ בְּשִׂמְחָה יַֽחֲרִישׁ בְּאַהֲבָתוֹ יָגִיל עָלַיִךְ בְּרִנָּֽה׃ | 17 |
Yahwe Mungu wako yuko katikati yenu, mwenye nguvu wa kuwaokoa. Atasherehekea juu yenu na kwa furaha atakuwa kimya juu yenu kwa upendo wake. Atakuwa na furaha juu yenu na atashangilia kwa furaha,
נוּגֵי מִמּוֹעֵד אָסַפְתִּי מִמֵּךְ הָיוּ מַשְׂאֵת עָלֶיהָ חֶרְפָּֽה׃ | 18 |
katika siku maalumu ya sherehe. Nitaondoa maafa kutoka kwenu; si muda mrefu hamtabeba aibu kwa ajili yake.
הִנְנִי עֹשֶׂה אֶת־כׇּל־מְעַנַּיִךְ בָּעֵת הַהִיא וְהוֹשַׁעְתִּי אֶת־הַצֹּלֵעָה וְהַנִּדָּחָה אֲקַבֵּץ וְשַׂמְתִּים לִתְהִלָּה וּלְשֵׁם בְּכׇל־הָאָרֶץ בׇּשְׁתָּֽם׃ | 19 |
Tazama, Niko tayari kuwashughulikia watesi wenu wote. Katika wakati ule, Nitawaokoa waliolemaa na kuwakusanya waliotupiliwa mbali. Nitawafanya kuwa sifa, na nitaibadilisha aibu yao iwe sifa katika dunia yote.
בָּעֵת הַהִיא אָבִיא אֶתְכֶם וּבָעֵת קַבְּצִי אֶתְכֶם כִּֽי־אֶתֵּן אֶתְכֶם לְשֵׁם וְלִתְהִלָּה בְּכֹל עַמֵּי הָאָרֶץ בְּשׁוּבִי אֶת־שְׁבוּתֵיכֶם לְעֵינֵיכֶם אָמַר יְהֹוָֽה׃ | 20 |
Katika wakati ule nitawaongoza; katika wakati ule nitawakusanya pamoja. Nitawafanya mataifa yote ya dunia kuwaheshimu na kuwasifu, wakati mtakapoona hivyo, Nitakuwa nimewarudisha”, asema Yahwe.