< שיר השירים 6 >

אָנָה הָלַךְ דּוֹדֵךְ הַיָּפָה בַּנָּשִׁים אָנָה פָּנָה דוֹדֵךְ וּנְבַקְשֶׁנּוּ עִמָּֽךְ׃ 1
Mpenzi wako ameenda wapi, ulio mzuri miongoni mwa wanawake? Kwa njia gani mpenzi wako ameenda? ilitumtafute nawe? Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
דּוֹדִי יָרַד לְגַנּוֹ לַעֲרֻגוֹת הַבֹּשֶׂם לִרְעוֹת בַּגַּנִּים וְלִלְקֹט שֽׁוֹשַׁנִּֽים׃ 2
Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro.
אֲנִי לְדוֹדִי וְדוֹדִי לִי הָרֹעֶה בַּשּׁוֹשַׁנִּֽים׃ 3
Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; na kula katika nyinyoro kwa raha. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
יָפָה אַתְּ רַעְיָתִי כְּתִרְצָה נָאוָה כִּירוּשָׁלָ͏ִם אֲיֻמָּה כַּנִּדְגָּלֽוֹת׃ 4
Wewe ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu, waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele.
הָסֵבִּי עֵינַיִךְ מִנֶּגְדִּי שֶׁהֵם הִרְהִיבֻנִי שַׂעְרֵךְ כְּעֵדֶר הָֽעִזִּים שֶׁגָּלְשׁוּ מִן־הַגִּלְעָֽד׃ 5
Geuza macho yako mbali na mimi, kwa kuwa yana nizidi ukali. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka miteremko ya Mlima Gileadi.
שִׁנַּיִךְ כְּעֵדֶר הָֽרְחֵלִים שֶׁעָלוּ מִן־הָרַחְצָה שֶׁכֻּלָּם מַתְאִימוֹת וְשַׁכֻּלָה אֵין בָּהֶֽם׃ 6
Meno yako ni kama kundi la kondoo likishuka kutoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja anapacha, na hamna ata mmoja aliyefiwa.
כְּפֶלַח הָרִמּוֹן רַקָּתֵךְ מִבַּעַד לְצַמָּתֵֽךְ׃ 7
Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso. Mpenzi wa mwanamke akizungumza peke yake
שִׁשִּׁים הֵמָּה מְלָכוֹת וּשְׁמֹנִים פִּֽילַגְשִׁים וַעֲלָמוֹת אֵין מִסְפָּֽר׃ 8
Kuna malikia sitini, masuria themanini, na wanawake wadogo bila idadi.
אַחַת הִיא יוֹנָתִי תַמָּתִי אַחַת הִיא לְאִמָּהּ בָּרָה הִיא לְיֽוֹלַדְתָּהּ רָאוּהָ בָנוֹת וַֽיְאַשְּׁרוּהָ מְלָכוֹת וּפִֽילַגְשִׁים וַֽיְהַלְלֽוּהָ׃ 9
Hua wangu, asiye na doa wangu, ni yeye pekee; ni binti muhimu wa mama yake; ndiye kipenzi cha mwanamke aliye mzaa. Mabinti wa wenzengu wamemuona na kumuita mbarikiwa; wamalikia na masuria walimuona pia, na wakamsifu: Kile walicho sema wamalikia na masuria
מִי־זֹאת הַנִּשְׁקָפָה כְּמוֹ־שָׁחַר יָפָה כַלְּבָנָה בָּרָה כַּֽחַמָּה אֲיֻמָּה כַּנִּדְגָּלֽוֹת׃ 10
“Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha, mzuri kama mwezi, ana ng'aa kama jua, uamasisha kama bendera ya jeshi?” Mpenzi wa mwanamke akizungumza mwenyewe
אֶל־גִּנַּת אֱגוֹז יָרַדְתִּי לִרְאוֹת בְּאִבֵּי הַנָּחַל לִרְאוֹת הֲפָֽרְחָה הַגֶּפֶן הֵנֵצוּ הָרִמֹּנִֽים׃ 11
Nimeenda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona mimea midogo ikikua bondeni, kuona kama mizabibu imechipua, na kama mikomamanga imestawi.
לֹא יָדַעְתִּי נַפְשִׁי שָׂמַתְנִי מַרְכְּבוֹת עַמִּי נָדִֽיב׃ 12
Nilikuwa nina furaha nikahisi kama nimepakia gari ya farasi la mtoto wa mfalme. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
שׁוּבִי שׁוּבִי הַשּׁוּלַמִּית שׁוּבִי שׁוּבִי וְנֶחֱזֶה־בָּךְ מַֽה־תֶּחֱזוּ בַּשּׁוּלַמִּית כִּמְחֹלַת הַֽמַּחֲנָֽיִם׃ 13
Geuka nyuma, geuka nyuma, wewe mwanamke mkamilifu; geuka nyuma, geuka nyuma iliniweze kukushangaa. Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake Kwanini wanishangaa, mwanamke mkamilifu, kana kwamba nina cheza katika ya mistari miwili ya wachezaji?

< שיר השירים 6 >