< שמות 22 >
כִּי יִגְנֹֽב־אִישׁ שׁוֹר אוֹ־שֶׂה וּטְבָחוֹ אוֹ מְכָרוֹ חֲמִשָּׁה בָקָר יְשַׁלֵּם תַּחַת הַשּׁוֹר וְאַרְבַּע־צֹאן תַּחַת הַשֶּֽׂה׃ | 1 |
Kama mwanaume akiiba ng'ombe aua kondoo na kumuua au kumuuza, kisha lazima alipe ng'ombe watano au ng'ombe mmoja, na kondoo wanne kwa mmoja.
אִם־בַּמַּחְתֶּרֶת יִמָּצֵא הַגַּנָּב וְהֻכָּה וָמֵת אֵין לוֹ דָּמִֽים׃ | 2 |
Kama mwizi akikutwa anavunja ndani, na kama akipigwa na kufa, hakutakuwa na hatia ya mauaji hayatakuwa juu ya mtu yeyote.
אִם־זָרְחָה הַשֶּׁמֶשׁ עָלָיו דָּמִים לוֹ שַׁלֵּם יְשַׁלֵּם אִם־אֵין לוֹ וְנִמְכַּר בִּגְנֵבָתֽוֹ׃ | 3 |
Lakini kama jua limechomoza kabla ya yeye kuvunja ndani, hatia ya mauaji itakuwa juu ya aliyemuua. Mwizi lazima afanya alipe alichoiba. Kama hana chochote, kisha lazima auzwe kwa uwizi wake.
אִֽם־הִמָּצֵא תִמָּצֵא בְיָדוֹ הַגְּנֵבָה מִשּׁוֹר עַד־חֲמוֹר עַד־שֶׂה חַיִּים שְׁנַיִם יְשַׁלֵּֽם׃ | 4 |
Kama mnyama amekutwa hai eneo lake, kama ni ng'ombe, punda, au kondoo, lazima alipe mara mbili.
כִּי יַבְעֶר־אִישׁ שָׂדֶה אוֹ־כֶרֶם וְשִׁלַּח אֶת־בְּעִירֹה וּבִעֵר בִּשְׂדֵה אַחֵר מֵיטַב שָׂדֵהוּ וּמֵיטַב כַּרְמוֹ יְשַׁלֵּֽם׃ | 5 |
Kama mwanaume akiwapeleka malishoni mifugo yake au shamba la mizabibu na akawaachia wanyama wake, na kawa wanakula shambani mwa mwanaume mwengine, lazima afanye malipo bora kutoka shambani mwake na shamba lake la mizabibu.
כִּֽי־תֵצֵא אֵשׁ וּמָצְאָה קֹצִים וְנֶאֱכַל גָּדִישׁ אוֹ הַקָּמָה אוֹ הַשָּׂדֶה שַׁלֵּם יְשַׁלֵּם הַמַּבְעִר אֶת־הַבְּעֵרָֽה׃ | 6 |
Kama moto ukitokea na kusambaa kwenye miba hadi mbegu, au mimea, au shamba kuteketezwa, yeye aliye anzisha moto lazima afanye malipo.
כִּֽי־יִתֵּן אִישׁ אֶל־רֵעֵהוּ כֶּסֶף אֽוֹ־כֵלִים לִשְׁמֹר וְגֻנַּב מִבֵּית הָאִישׁ אִם־יִמָּצֵא הַגַּנָּב יְשַׁלֵּם שְׁנָֽיִם׃ | 7 |
Kama mwanaume akitoa pesa au mali kwa jirani yake amtunzie, na kama itaibiwa nyumbani mwa huyo mwanaume, kama mwizi akipatikana, huyo mwizi lazima alipe mara mbili.
אִם־לֹא יִמָּצֵא הַגַּנָּב וְנִקְרַב בַּֽעַל־הַבַּיִת אֶל־הָֽאֱלֹהִים אִם־לֹא שָׁלַח יָדוֹ בִּמְלֶאכֶת רֵעֵֽהוּ׃ | 8 |
Lakini kama mwizi asipo patikana, kisha mmiliki wa nyumba ata kuja mbele za waamuzi kuona kama ameeka mkono wake kwenye mali za jirani yake.
עַֽל־כׇּל־דְּבַר־פֶּשַׁע עַל־שׁוֹר עַל־חֲמוֹר עַל־שֶׂה עַל־שַׂלְמָה עַל־כׇּל־אֲבֵדָה אֲשֶׁר יֹאמַר כִּי־הוּא זֶה עַד הָֽאֱלֹהִים יָבֹא דְּבַר־שְׁנֵיהֶם אֲשֶׁר יַרְשִׁיעֻן אֱלֹהִים יְשַׁלֵּם שְׁנַיִם לְרֵעֵֽהוּ׃ | 9 |
Kwa kila lumbano kuhusu jambo, kama ni ng'ombe, punda, kondoo, nguo, au chochote kilichopotea mtu anacho sema, “Hichi ni changu,” malalamiko ya pande zote lazima zije kwa waamuzi. Mwanaume ambaye waamuzi wanamkuta na hatia ata lipa mara mbili kwa jirani yake.
כִּֽי־יִתֵּן אִישׁ אֶל־רֵעֵהוּ חֲמוֹר אוֹ־שׁוֹר אוֹ־שֶׂה וְכׇל־בְּהֵמָה לִשְׁמֹר וּמֵת אוֹ־נִשְׁבַּר אוֹ־נִשְׁבָּה אֵין רֹאֶֽה׃ | 10 |
Kama mwanaume akimpa jirani yake punda, ng'ombe, kondoo, au mnyama yeyote kumuhifadhia, na kama akifa au kuumia au akibebwa pasipo mtu kumuona,
שְׁבֻעַת יְהֹוָה תִּהְיֶה בֵּין שְׁנֵיהֶם אִם־לֹא שָׁלַח יָדוֹ בִּמְלֶאכֶת רֵעֵהוּ וְלָקַח בְּעָלָיו וְלֹא יְשַׁלֵּֽם׃ | 11 |
kiapo kwa Yahweh lazima wafanye wote wawili, kama ndio au hapana mtu ameeka mkono wake kwenye mali ya jirani yake. Mmiliki lazima akubali hili, na mwengine hatafanya malipo.
וְאִם־גָּנֹב יִגָּנֵב מֵעִמּוֹ יְשַׁלֵּם לִבְעָלָֽיו׃ | 12 |
Lakini kama iliibwa kwake, mwengine lazima afanye malipo kwa mmiliki kwa ajili yake.
אִם־טָרֹף יִטָּרֵף יְבִאֵהוּ עֵד הַטְּרֵפָה לֹא יְשַׁלֵּֽם׃ | 13 |
Kama mnyama alikatwa vipande, acha mwanaume mwengine alete huyo mnyama kama ushahidi. Hatalipa kwa ajili ya vile vipande.
וְכִֽי־יִשְׁאַל אִישׁ מֵעִם רֵעֵהוּ וְנִשְׁבַּר אוֹ־מֵת בְּעָלָיו אֵין־עִמּוֹ שַׁלֵּם יְשַׁלֵּֽם׃ | 14 |
Kama mwanaume akiazima mnyama kutoka kwa jirani yake na mnyama akajeruhia au akafa pasipo mmiliki kuwa naye, mwanaume mwengine lazima afanya malipo.
אִם־בְּעָלָיו עִמּוֹ לֹא יְשַׁלֵּם אִם־שָׂכִיר הוּא בָּא בִּשְׂכָרֽוֹ׃ | 15 |
Lakini kama mmiliki alikuwa nae, mwanaume mwengine haitaji kulipa; kama mnyama aliazimwa, atalipwa kwa gharama ya kuazima.
וְכִֽי־יְפַתֶּה אִישׁ בְּתוּלָה אֲשֶׁר לֹא־אֹרָשָׂה וְשָׁכַב עִמָּהּ מָהֹר יִמְהָרֶנָּה לּוֹ לְאִשָּֽׁה׃ | 16 |
Kama mwanaume akimtongoza bikra ambaye hana mchumba, na kama akilala naye, lazima amfanye kuwa mke wake kwa kulipa gharama za bibi arusi zinazo stahili.
אִם־מָאֵן יְמָאֵן אָבִיהָ לְתִתָּהּ לוֹ כֶּסֶף יִשְׁקֹל כְּמֹהַר הַבְּתוּלֹֽת׃ | 17 |
Kama baba yake akikataa kabisa kumpatia, lazima alipe hela inayo lingana na gharama za bibi arusi bikra.
מְכַשֵּׁפָה לֹא תְחַיֶּֽה׃ | 18 |
Hautamwacha mchawi kuishi.
כׇּל־שֹׁכֵב עִם־בְּהֵמָה מוֹת יוּמָֽת׃ | 19 |
Yeyote atakaye lala na mnyama lazima auawe.
זֹבֵחַ לָאֱלֹהִים יׇֽחֳרָם בִּלְתִּי לַיהֹוָה לְבַדּֽוֹ׃ | 20 |
Yeyote atakaye toa dhabihu kwa mungu mwengine isipo kuwa Yahweh lazima auawe.
וְגֵר לֹא־תוֹנֶה וְלֹא תִלְחָצֶנּוּ כִּֽי־גֵרִים הֱיִיתֶם בְּאֶרֶץ מִצְרָֽיִם׃ | 21 |
Hauta mkosea mgeni au kumnyanyasa, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
כׇּל־אַלְמָנָה וְיָתוֹם לֹא תְעַנּֽוּן׃ | 22 |
Hauruhusiwi kumtendea vibaya mjane au mtoto asiye kuwa na baba.
אִם־עַנֵּה תְעַנֶּה אֹתוֹ כִּי אִם־צָעֹק יִצְעַק אֵלַי שָׁמֹעַ אֶשְׁמַע צַעֲקָתֽוֹ׃ | 23 |
Ukiwadhuru ata kidogo, na kama wakiniita mimi, hakika nitasikia sauti yao.
וְחָרָה אַפִּי וְהָרַגְתִּי אֶתְכֶם בֶּחָרֶב וְהָיוּ נְשֵׁיכֶם אַלְמָנוֹת וּבְנֵיכֶם יְתֹמִֽים׃ | 24 |
Hasira yangu itawaka, na nitakuua kwa upanga; wake zenu watakuwa wajane, na watoto wenu pasipo baba.
אִם־כֶּסֶף ׀ תַּלְוֶה אֶת־עַמִּי אֶת־הֶֽעָנִי עִמָּךְ לֹא־תִהְיֶה לוֹ כְּנֹשֶׁה לֹֽא־תְשִׂימוּן עָלָיו נֶֽשֶׁךְ׃ | 25 |
Ukiazima hela kwa watu wangu walio maskini, haupaswi kuwa kama anaye kopesha hela kwake au kutoza faida.
אִם־חָבֹל תַּחְבֹּל שַׂלְמַת רֵעֶךָ עַד־בֹּא הַשֶּׁמֶשׁ תְּשִׁיבֶנּוּ לֽוֹ׃ | 26 |
Ukichukuwa vazi la jirani yako kwa deni, lazima umrudishie kabla jua kuzama,
כִּי הִוא כְסוּתֹה לְבַדָּהּ הִוא שִׂמְלָתוֹ לְעֹרוֹ בַּמֶּה יִשְׁכָּב וְהָיָה כִּֽי־יִצְעַק אֵלַי וְשָׁמַעְתִּי כִּֽי־חַנּוּן אָֽנִי׃ | 27 |
kwa kuwa hilo ndilo funiko lake, ni vazi la mwili wake. Nini tena ambacho anaweza kulalia? Atakapo niita mimi, nitasikia, kwa kuwa mimi ni mwenye huruma.
אֱלֹהִים לֹא תְקַלֵּל וְנָשִׂיא בְעַמְּךָ לֹא תָאֹֽר׃ | 28 |
Usinikufuru mimi, Mungu, wala kumtukana mtawala wa watu wako.
מְלֵאָתְךָ וְדִמְעֲךָ לֹא תְאַחֵר בְּכוֹר בָּנֶיךָ תִּתֶּן־לִֽי׃ | 29 |
Husizuie sadaka kutoka kwenye mavuno yako au kwenye hifadhi ya mvinyo wako. Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako.
כֵּֽן־תַּעֲשֶׂה לְשֹׁרְךָ לְצֹאנֶךָ שִׁבְעַת יָמִים יִהְיֶה עִם־אִמּוֹ בַּיּוֹם הַשְּׁמִינִי תִּתְּנוֹ־לִֽי׃ | 30 |
Lazima ufanye hivyo hivyo kwa ng'ombe na kondoo wako. Kwa siku saba lazima wabaki na mama zao, lakini siku ya nane lazima unipe mimi.
וְאַנְשֵׁי־קֹדֶשׁ תִּהְיוּן לִי וּבָשָׂר בַּשָּׂדֶה טְרֵפָה לֹא תֹאכֵלוּ לַכֶּלֶב תַּשְׁלִכוּן אֹתֽוֹ׃ | 31 |
Mtakuwa watu walio tengwa kwa ajili yangu. Hivyo hamtakula nyama iliyo uliwa na wanyama porini. Badala yake, uwatupie mbwa.