< תהילים 93 >
יהוה מלך גאות לבש לבש יהוה עז התאזר אף-תכון תבל בל-תמוט | 1 |
Yahwe anatawala; amevikwa adhama; Yahwe amejivika na kujifunga nguvu. Ulimwengu umeimalishwa; hauwezi kusogezwa.
נכון כסאך מאז מעולם אתה | 2 |
Kiti chako cha enzi kimeimarishwa nyakati za kale; umekuwepo siku zote.
נשאו נהרות יהוה--נשאו נהרות קולם ישאו נהרות דכים | 3 |
Bahari zimeinuka, Yahwe; zimemepaza sauti zao; mawimbi ya bahari yapiga ghasia na ngurumo.
מקלות מים רבים--אדירים משברי-ים אדיר במרום יהוה | 4 |
Zaidi ya ghasia ya mawimbi mengi, mawimbi ya bahari yenye nguvu, Yahwe aliye juu ni mwenye nguvu.
עדתיך נאמנו מאד--לביתך נאוה-קדש יהוה לארך ימים | 5 |
Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.