< תהילים 83 >

שיר מזמור לאסף ב אלהים אל-דמי-לך אל-תחרש ואל-תשקט אל 1
Ee Mungu, usikae kimya! usitupuuze na kustarehe, Ee Mungu.
כי-הנה אויביך יהמיון ומשנאיך נשאו ראש 2
Tazama, adui zako wanafanya vurugu, na wale wakuchukiao wameinua vichwa vyao.
על-עמך יערימו סוד ויתיעצו על-צפוניך 3
Wanafanya hila juu ya watu wako na kwa pamoja kupanga njama dhidi ya wale uwalindao. Wamesema,
אמרו--לכו ונכחידם מגוי ולא-יזכר שם-ישראל עוד 4
“Njoni na tuwaangamize wao kama taifa. Kisha jina la Israeli halitakumbukwa.”
כי נועצו לב יחדו עליך ברית יכרתו 5
Wamepanga njama pamoja wakiwa na mkakati mmoja; wamefanya muungano dhidi yako.
אהלי אדום וישמעאלים מואב והגרים 6
Hii inajumuisha hema za Edomu na Waishmaeli, na watu wa Moabu na Wahagari, ambao wamepanga njama pamoja nao
גבל ועמון ועמלק פלשת עם-ישבי צור 7
Gebal, Amoni, Amaleki; pia inajumuisha Filisti na wenyeji wa Tiro.
גם-אשור נלוה עמם היו זרוע לבני-לוט סלה 8
Ashuri pia ameshirikina nao; wanawasaidia wana wa Lutu. Serah
עשה-להם כמדין כסיסרא כיבין בנחל קישון 9
Ufanye kwao kama ulivyofanya kwa Midiani, kama ulivyofanya kwa Sisera na kwa Yabini kwenye Mto Kishoni.
נשמדו בעין-דאר היו דמן לאדמה 10
Waliangamizwa kule Endori na wakawa kama mbolea juu ya chi.
שיתמו נדיבימו כערב וכזאב וכזבח וכצלמנע כל-נסיכימו 11
Uvifanye vyeo vyao kama Oreb na Zeeb, na wakuu wao wote kama Zeba na Zalmuna.
אשר אמרו נירשה לנו-- את נאות אלהים 12
Wao walisema, natujimilikishe malisho ya Mungu.”
אלהי שיתמו כגלגל כקש לפני-רוח 13
Ee Mungu wangu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi mbele ya upepo,
כאש תבער-יער וכלהבה תלהט הרים 14
Kama moto uteketezao msitu, na kama miali ya moto iwakayo milimani.
כן תרדפם בסערך ובסופתך תבהלם 15
Uwafuatie kwa tufani yako, na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
מלא פניהם קלון ויבקשו שמך יהוה 16
Uwajaze nyuso zao kwa aibu ili kwamba waweze kulitafuta jina lako, Yahwe.
יבשו ויבהלו עדי-עד ויחפרו ויאבדו 17
Nao waaibishwe na kufadhaishwa milele; waangamizwe katika aibu.
וידעו-- כי-אתה שמך יהוה לבדך עליון על-כל-הארץ 18
Kisha watajua kwamba ni wewe pekee, Yahwe, Uliye Juu ya nchi yote.

< תהילים 83 >