< תהילים 78 >

משכיל לאסף האזינה עמי תורתי הטו אזנכם לאמרי-פי 1
Watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu.
אפתחה במשל פי אביעה חידות מני-קדם 2
Nitafungua kinywa changu katika mifano; nitaimba kuhusu mambo yaliyofichika yahusuyo yaliyopita.
אשר שמענו ונדעם ואבותינו ספרו-לנו 3
Haya ni mambo ambayo tumeyasikia na kujifunza mambo ambayo mababu zetu wametuambia sisi. Hatutawaficha uzao wao.
לא נכחד מבניהם-- לדור אחרון מספרים תהלות יהוה ועזוזו ונפלאתיו אשר עשה 4
Tutawaambia kizazi kijacho kuhusu sifa anazostahili Yahwe kwa matendo yake, nguvu zake, na maajabu ambayo ameyafanya.
ויקם עדות ביעקב ותורה שם בישראל אשר צוה את-אבותינו-- להודיעם לבניהם 5
Kwa kuwa yeye alianzisha agano la amri katika Yakobo na sheria maalumu katika Israeli. Yeye aliamuru mababu zetu kuwa walipaswa kuzifundisha kwa watoto wao.
למען ידעו דור אחרון--בנים יולדו יקמו ויספרו לבניהם 6
Aliamuru hivi ili kwamba kizazi kijacho kiweze kuzijua amri zake, ili wawafundishe wana ambao bado hawajazaliwa.
וישימו באלהים כסלם ולא ישכחו מעללי-אל ומצותיו ינצרו 7
Kisha wangeweka tumaini lao katika Mungu na kutokusahau matendo yake bali wazishike amri zake.
ולא יהיו כאבותם-- דור סורר ומרה דור לא-הכין לבו ולא-נאמנה את-אל רוחו 8
Ndipo wasingekuwa kama mababu zao, ambao walikuwa wakaidi na wenye uasi, kizazi ambacho mioyo yao haikuwa kamilifu, na ambao roho zao hazikuwa na nia thabiti na aminifu kwa Mungu.
בני-אפרים נושקי רומי-קשת הפכו ביום קרב 9
Waefraimu walikuwa na silaha na upinde, lakini walikimbia siku ya vita.
לא שמרו ברית אלהים ובתורתו מאנו ללכת 10
Hawakutunza agano na Mungu, na walikataa kutii sheria yake.
וישכחו עלילותיו ונפלאותיו אשר הראם 11
Walisahau matendo yake, mambo ya ajabu ambayo yeye amewaonesha wao.
נגד אבותם עשה פלא בארץ מצרים שדה-צען 12
Walisahau mambo ya ajabu aliyofayafanya machoni pa mababu zao katika nchi ya Misri, katika ardhi ya Soani.
בקע ים ויעבירם ויצב-מים כמו-נד 13
Aliigawa bahari na akawaongoza katikati ya bahari; aliyafanya maji yasimame kama kuta.
וינחם בענן יומם וכל-הלילה באור אש 14
Wakati wa mchana aliwaongoza kwa wingu na usiku wote kwa nuru ya moto.
יבקע צרים במדבר וישק כתהמות רבה 15
Alipasua miamba jangwani, na aliwapa maji mengi, ya kutosha kujaza vina virefu vya bahari.
ויוצא נוזלים מסלע ויורד כנהרות מים 16
Alifanya maporomoko ya maji kutiririka tokea mwambani na aliyafanya maji yatiririke kama mito.
ויוסיפו עוד לחטא-לו-- למרות עליון בציה 17
Lakini bado waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi dhidi ya Aliye Juu katika jangwa.
וינסו-אל בלבבם-- לשאל-אכל לנפשם 18
Walimjaribu Mungu mioyoni mwao kwa kuomba chakula cha kuwatosheleza hamu zao.
וידברו באלהים אמרו היוכל אל--לערך שלחן במדבר 19
Waliongea dhidi ya Mungu; walisema, “Kweli Mungu anaweza kuweka meza ya chakula kwa ajili yetu jangwani?
הן הכה-צור ויזובו מים-- ונחלים ישטפו הגם-לחם יוכל תת אם-יכין שאר לעמו 20
Tazama, wakati alipoupiga mwamba, maji yalibubujika, mito ikafurika. Lakini anaweza kutoa mkate tena? Ataweza kuleta nyama kwa watu wake?”
לכן שמע יהוה-- ויתעבר ואש נשקה ביעקב וגם-אף עלה בישראל 21
Yahwe aliposikia haya, alikasirika; moto wake uliwaka dhidi ya Yakobo, hasira yake ikamshambulia Israeli,
כי לא האמינו באלהים ולא בטחו בישועתו 22
kwa sababu hawakumwamini Mungu na hawakuamini katika wokovu wake.
ויצו שחקים ממעל ודלתי שמים פתח 23
Lakini yeye bado aliziamuru mbingu juu na kufungua milango ya mbingu.
וימטר עליהם מן לאכל ודגן-שמים נתן למו 24
Aliwanyeshea mana ili wale, na aliwapa nafaka kutoka mbinguni.
לחם אבירים אכל איש צידה שלח להם לשבע 25
Watu walikula mikate ya malaika. Aliwatumia chakula kingi.
יסע קדים בשמים וינהג בעזו תימן 26
Alisababisha upepo wa mashariki kupiga mawinguni, na kwa uweza wake aliuongoza upepo wa kusini.
וימטר עליהם כעפר שאר וכחול ימים עוף כנף 27
Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, na ndege kama wingi wa mchanga wa baharini.
ויפל בקרב מחנהו סביב למשכנתיו 28
Walianguka katikati ya kambi yao, na maeneo yote karibu na hema zao.
ויאכלו וישבעו מאד ותאותם יבא להם 29
Hivyo walikula na walishiba. Maana aliwapa kile walichokitamani sana.
לא-זרו מתאותם עוד אכלם בפיהם 30
Lakini walikuwa bado hawajatosheka; chakula chao kilikuwa bado kinywani mwao.
ואף אלהים עלה בהם ויהרג במשמניהם ובחורי ישראל הכריע 31
Ndipo hasira ya Mungu iliwashambulia na kuwaua wenye nguvu kati yao. Aliwaangusha chini vijana wa Israeli.
בכל-זאת חטאו-עוד ולא-האמינו בנפלאותיו 32
Licha ya hili, waliendelea kutenda dhambi na hawakuyaamini matendo yake ya ajabu.
ויכל-בהבל ימיהם ושנותם בבהלה 33
Hivyo Mungu alizikatisha siku zao; miaka yao ilijawa na hofu.
אם-הרגם ודרשוהו ושבו ושחרו-אל 34
Wakati wowote Mungu alipowataabisha, nao waligeuka na kumtafuta yeye kwa bidii.
ויזכרו כי-אלהים צורם ואל עליון גאלם 35
Walikumbuka kuwa Mungu alikuwa mwamba wao na kuwa Mungu Aliye Juu Sana alikuwa mwokozi wao.
ויפתוהו בפיהם ובלשונם יכזבו-לו 36
Lakini walimsifia tu kwa vinywa vyao na kumdanganya kwa maneno yao.
ולבם לא-נכון עמו ולא נאמנו בבריתו 37
Maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake, na hawakuwa waaminifu kwa agano lake.
והוא רחום יכפר עון-- ולא-ישחית והרבה להשיב אפו ולא-יעיר כל-חמתו 38
Lakini yeye, kwa kuwa alikuwa alikuwa na huruma, aliwasamehe uovu wao na hakuwaangamiza. Ndiyo, wakati mwingi aliizuia hasira yake na hakuionesha ghadhabu yake yote.
ויזכר כי-בשר המה רוח הולך ולא ישוב 39
Alikumbuka kuwa waliumbwa kwa mwili, upepo ambao hupita nao haurudi.
כמה ימרוהו במדבר יעציבוהו בישימון 40
Mara ngapi wameasi dhidi yake jangwani na kumuhuzunisha nyikani!
וישובו וינסו אל וקדוש ישראל התוו 41
Tena na tena walimjaribu Mungu na wakamtilia mashaka Mtakatifu wa Israeli.
לא-זכרו את-ידו יום אשר-פדם מני-צר 42
Hawakufikiria kuhusu uweza wake, jinsi alivyo waokoa dhidi ya adui
אשר-שם במצרים אתותיו ומופתיו בשדה-צען 43
alipofanya ishara za kutisha katika Misri na maajabu yake katika konde la Soani.
ויהפך לדם יאריהם ונזליהם בל-ישתיון 44
Aligeuza mito ya Wamisri kuwa damu ili wasipate kunywa kutoka katika vijito vyao.
ישלח בהם ערב ויאכלם וצפרדע ותשחיתם 45
Alituma makundi ya inzi yaliyowavamia na vyura ambao walisambaa katika nchi yao.
ויתן לחסיל יבולם ויגיעם לארבה 46
Aliwapa mazao yao panzi na kazi yao nzige.
יהרג בברד גפנם ושקמותם בחנמל 47
Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na miti ya mikuyu kwa mvua ya mawe zaidi.
ויסגר לברד בעירם ומקניהם לרשפים 48
Aliinyeshea mifugo yao mvua ya mawe na alirusha radi ya umeme ikapiga mifugo yao. Ukali wa hasira yake ulielekea dhidi yao.
ישלח-בם חרון אפו--עברה וזעם וצרה משלחת מלאכי רעים 49
Alituma gadhabu, uchungu na taabu kama wakala aletaye maafa.
יפלס נתיב לאפו לא-חשך ממות נפשם וחיתם לדבר הסגיר 50
Aliifanyia njia hasira yake; hakuwakinga dhidi ya kifo bali aliwakabidhi kwa pigo.
ויך כל-בכור במצרים ראשית אונים באהלי-חם 51
Aliwaua wazaliwa wote wa kwanza katika Misri, wazaliwa wa kwanza wa nguvu zao katika mahema ya Hamu.
ויסע כצאן עמו וינהגם כעדר במדבר 52
Aliwaongoza nje watu wake mwenyewe kama kondoo na aliwaelekeza kupitia jangwani kama kundi.
וינחם לבטח ולא פחדו ואת-אויביהם כסה הים 53
Aliwaongoza salama na pasipo na woga, lakini bahari iliwaelemea adui zao.
ויביאם אל-גבול קדשו הר-זה קנתה ימינו 54
Kisha aliwaleta mpaka wa nchi yake takatifu, kwenye mlima huu ambao aliutwaa kwa mkono wake wa kuume.
ויגרש מפניהם גוים-- ויפילם בחבל נחלה וישכן באהליהם שבטי ישראל 55
Aliwafukuza mataifa mbele yao na akawapa urithi wao. Aliwakalisha makabila ya Israeli katika mahema yao.
וינסו וימרו את-אלהים עליון ועדותיו לא שמרו 56
Lakini bado walimjaribu na walimkaidi Mungu Aliye Juu na hawakushika amri zake takatifu.
ויסגו ויבגדו כאבותם נהפכו כקשת רמיה 57
Hawakuwa waaminifu na walienenda katika hila kama baba zao; walikuwa sio wa kutegemewa kama upinde mbovu.
ויכעיסוהו בבמותם ובפסיליהם יקניאוהו 58
Kwa maana walimkasirisha kwa mahali pao pa juu na walimgadhabisha hata akawa na hasira ya wivu kwa miungu yao.
שמע אלהים ויתעבר וימאס מאד בישראל 59
Mungu aliposikia hili, alikasirika na alimkataa kabisa Israeli.
ויטש משכן שלו אהל שכן באדם 60
Alipaacha patakatifu pa Shilo, na hema alikoishi kati ya watu.
ויתן לשבי עזו ותפארתו ביד-צר 61
Aliruhusu nguvu zake kutekwa na kuutoa utukufu wake mkononi mwa adui.
ויסגר לחרב עמו ובנחלתו התעבר 62
Aliukabidhi upanga watu wake, na aliukasirikia urithi wake.
בחוריו אכלה-אש ובתולתיו לא הוללו 63
Moto uliwavamia vijana wao wa kiume, na vijana wao wa kike hawakuwa na nyimbo za harusi.
כהניו בחרב נפלו ואלמנתיו לא תבכינה 64
Makuhani wao waliangushwa kwa upanga, na wajane wao hawakulia.
ויקץ כישן אדני כגבור מתרונן מיין 65
Kisha Bwana aliamshwa kama aliyetoka usingizini, kama shujaa apigaye kelele kwa sababu ya mvinyo.
ויך-צריו אחור חרפת עולם נתן למו 66
Aliwarudisha adui zake nyuma; aliwaweka kwenye aibu ya milele.
וימאס באהל יוסף ובשבט אפרים לא בחר 67
Aliikataa hema ya Yusufu, na hakulichagua kabila la Efraimu.
ויבחר את-שבט יהודה את-הר ציון אשר אהב 68
Alilichagua kabila la Yuda na Mlima Sayuni aliyoupenda.
ויבן כמו-רמים מקדשו כארץ יסדה לעולם 69
Alipajenga patakatifu pake kama mbinguni, na kama nchi aliyoiimarisha milele.
ויבחר בדוד עבדו ויקחהו ממכלאת צאן 70
Alimchagua Daudi, mtumishi wake, alimchukua kutoka zizi la kondoo.
מאחר עלות הביאו לרעות ביעקב עמו ובישראל נחלתו 71
Alimtoa kutoka katika kufuata kondoo pamoja na wana wao, na kumweka kuwa mchungaji wa Yakobo, watu wake, na Israeli, urithi wake.
וירעם כתם לבבו ובתבונות כפיו ינחם 72
Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo wake, naye aliwaongoza kwa ujuzi wa mikono yake.

< תהילים 78 >