< תהילים 62 >

למנצח על-ידותון-- מזמור לדוד ב אך אל-אלהים דומיה נפשי ממנו ישועתי 1
Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; wokovu wangu watoka kwake.
אך-הוא צורי וישועתי משגבי לא-אמוט רבה 2
Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu mrefu; sitasogezwa kamwe.
עד-אנה תהותתו על-איש-- תרצחו כלכם כקיר נטוי גדר הדחויה 3
Mpaka lini, ninyi nyote, mtamshambulia mtu, ili kwamba mumpindue yeye kama ukuta ulio inama au kama fensi isiyo imara?
אך משאתו יעצו להדיח-- ירצו כזב בפיו יברכו ובקרבם יקללו-סלה 4
Wanashauliana naye ili tu kumshusha chini kutoka kwenye nafasi yake heshimiwa; wao wanapenda kuongea uongo; wanambariki yeye kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wana mlaani yeye. (Selah)
אך לאלהים דומי נפשי כי-ממנו תקותי 5
Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; kwa maana matumaini yangu yako kwake.
אך-הוא צורי וישועתי משגבי לא אמוט 6
Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu mrefu; sitasogezwa.
על-אלהים ישעי וכבודי צור-עזי מחסי באלהים 7
Na Mungu ni wokovu wangu na utukufu wangu; mwamba wa nguvu yangu na kimbilio langu salama liko katika Mungu.
בטחו בו בכל-עת עם-- שפכו-לפניו לבבכם אלהים מחסה-לנו סלה 8
Mwaminini Mungu wakati wote, ninyi watu; mimina moyo wako mbele zake; Mungu ni kimbilio salama kwa ajili yetu. (Selah)
אך הבל בני-אדם-- כזב בני-איש במאזנים לעלות המה מהבל יחד 9
Hakika watu wenye msimamo mdogo ni ubatili, na watu wenye msimamo mkubwa ni waongo; wao watakuwa wepesi kwenye mzani; uzito wao pamoja ni wepesi kuliko kitu chochote.
אל-תבטחו בעשק ובגזל אל-תהבלו חיל כי-ינוב-- אל-תשיתו לב 10
Usiamini katika ukandamizaji au wizi; usitumainie utajiri, maana hawatazaa matunda; usiuweke moyo wako kwenye hivyo.
אחת דבר אלהים--שתים-זו שמעתי כי עז לאלהים 11
Mungu ameongea mara moja, mara mbili nimesikia hili: nguvu ni za Mungu.
ולך-אדני חסד כי-אתה תשלם לאיש כמעשהו 12
Pia kwako, Bwana, ni uaminifu wa agano, maana humlipa kila mtu kwa kile alichokifanya.

< תהילים 62 >