< תהילים 60 >

למנצח על-שושן עדות מכתם לדוד ללמד ב בהצותו את ארם נהרים-- ואת-ארם צובה וישב יואב ויך את-אדום בגיא-מלח-- שנים עשר אלף ג אלהים זנחתנו פרצתנו אנפת תשובב לנו 1
Mungu, wewe umetutupa; umeuvunja ulinzi wetu; wewe umekuwa hasirani; utuwezeshe tena.
הרעשתה ארץ פצמתה רפה שבריה כי-מטה 2
Wewe umeifanya nchi kutetemeka; umeipasua pasua; uiponye nyufa zake, maana zinatikisika.
הראית עמך קשה השקיתנו יין תרעלה 3
Wewe umewafanya watu wako kuona mambo magumu; umetufanya tunywe mvinyo wenye kutufanya kupepesuka.
נתתה ליראיך נס להתנוסס-- מפני קשט סלה 4
Kwa wale wanao kuheshimu wewe, wewe umeweka bandera ionekane dhidi ya wale wabebao upinde. (Selah)
למען יחלצון ידידיך הושיעה ימינך ועננו (וענני) 5
Ili kwamba wale uwapendao waweze kuokolewa, utuokoe sisi kwa mkono wako wa kuume na unijibu.
אלהים דבר בקדשו--אעלזה אחלקה שכם ועמק סכות אמדד 6
Mungu ameongea katika utakatifu wake, “Nitashangilia; nitaigawanya Shekemu na kuligawa bonde la Sukothi.
לי גלעד ולי מנשה ואפרים מעוז ראשי יהודה מחקקי 7
Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu na Ephraimu pia ni kofia yangu ya chuma; Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.
מואב סיר רחצי--על-אדום אשליך נעלי עלי פלשת התרועעי 8
Moabu ni bakuli langu la kunawia; juu ya Edomu nitatupa kiatu changu; nitapiga kelele za ushindi kwa sababu ya Filisti.”
מי יבלני עיר מצור מי נחני עד-אדום 9
Ni nani atakaye nileta kwenye mji imara? Ni nani ataniongoza kwenda Edomu?
הלא-אתה אלהים זנחתנו ולא-תצא אלהים בצבאותינו 10
Lakini wewe, Mungu, je, haukutukataa? Wewe hauendi vitani pamoja na jeshi letu.
הבה-לנו עזרת מצר ושוא תשועת אדם 11
Utusaidie dhidi ya adui yetu, maana msaada wa mwanadamu ni bure.
באלהים נעשה-חיל והוא יבוס צרינו 12
Kwa msaada wa Mungu tutashinda; yeye atawakanyaga chini adui zetu.

< תהילים 60 >