< תהילים 57 >
למנצח אל-תשחת לדוד מכתם-- בברחו מפני-שאול במערה ב חנני אלהים חנני-- כי בך חסיה נפשי ובצל-כנפיך אחסה-- עד יעבר הוות | 1 |
Unihurumie, Mungu, unihurumie mimi, kwa maana ninakukimbilia wewe mpaka matatizo haya yaishe. Ninakaa chini ya mbawa za zako kwa ajili ya ulinzi mpaka huu uharibifu utakapoisha.
אקרא לאלהים עליון לאל גמר עלי | 2 |
Nitakulilia Mungu uliye hai, kwa Mungu, afanyaye mambo yote kwa ajili yangu.
ישלח משמים ויושיעני-- חרף שאפי סלה ישלח אלהים חסדו ואמתו | 3 |
Yeye atatuma msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, ana hasira na wale wanaonishambulia. (Selah) Mungu atanitumia upendo wake mwema na uaminifu wake.
נפשי בתוך לבאם-- אשכבה להטים בני-אדם--שניהם חנית וחצים ולשונם חרב חדה | 4 |
Uhai wangu uko katikati ya simba; niko katikati ya wale walio tayari kunila. Niko katikati ya watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, na ambao ndimi zao ni kali kama upanga.
רומה על-השמים אלהים על כל-הארץ כבודך | 5 |
Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu, utukufu wako uwe juu ya nchi yote.
רשת הכינו לפעמי-- כפף נפשי כרו לפני שיחה נפלו בתוכה סלה | 6 |
Wao walisambaza nje wavu kwa ajili ya miguu yangu; nilikuwa na shida sana. Walichimba shimo mbele yangu. Wao wenyewe wameangukia katikati ya shimo! (Selah)
נכון לבי אלהים נכון לבי אשירה ואזמרה | 7 |
Moyo wangu umeponywa, Mungu, moyo wangu umeponywa, nitaimba, ndiyo, nitaimba sifa.
עורה כבודי--עורה הנבל וכנור אעירה שחר | 8 |
Inuka, moyo wa thamani; inuka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri.
אודך בעמים אדני אזמרך בלאמים | 9 |
Nitakushukuru wewe, Bwana, kati ya watu; Kati ya mataifa nitakuimbia sifa.
כי-גדל עד-שמים חסדך ועד-שחקים אמתך | 10 |
Maana upendo wako usiokwisha, huzifikia mbingu; na uaminifu wako mawinguni.
רומה על-שמים אלהים על כל-הארץ כבודך | 11 |
Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu; na utukufu wako uinuliwe juu ya nchi yote.