< תהילים 44 >
למנצח לבני-קרח משכיל ב אלהים באזנינו שמענו-- אבותינו ספרו-לנו פעל פעלת בימיהם בימי קדם | 1 |
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametueleza yale uliyotenda katika siku zao, siku za kale.
אתה ידך גוים הורשת-- ותטעם תרע לאמים ותשלחם | 2 |
Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu.
כי לא בחרבם ירשו ארץ וזרועם לא-הושיעה-למו כי-ימינך וזרועך ואור פניך-- כי רציתם | 3 |
Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.
אתה-הוא מלכי אלהים צוה ישועות יעקב | 4 |
Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo.
בך צרינו ננגח בשמך נבוס קמינו | 5 |
Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.
כי לא בקשתי אבטח וחרבי לא תושיעני | 6 |
Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi;
כי הושעתנו מצרינו ומשנאינו הבישות | 7 |
bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, unawaaibisha watesi wetu.
באלהים הללנו כל-היום ושמך לעולם נודה סלה | 8 |
Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, nasi tutalisifu jina lako milele.
אף-זנחת ותכלימנו ולא-תצא בצבאותינו | 9 |
Lakini sasa umetukataa na kutudhili, wala huendi tena na jeshi letu.
תשיבנו אחור מני-צר ומשנאינו שסו למו | 10 |
Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui, nao watesi wetu wametuteka nyara.
תתננו כצאן מאכל ובגוים זריתנו | 11 |
Umetuacha tutafunwe kama kondoo na umetutawanya katika mataifa.
תמכר-עמך בלא-הון ולא-רבית במחיריהם | 12 |
Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.
תשימנו חרפה לשכנינו לעג וקלס לסביבותינו | 13 |
Umetufanya lawama kwa jirani zetu, dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka.
תשימנו משל בגוים מנוד-ראש בלאמים | 14 |
Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa, mataifa hutikisa vichwa vyao.
כל-היום כלמתי נגדי ובשת פני כסתני | 15 |
Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, na uso wangu umejaa aibu tele,
מקול מחרף ומגדף מפני אויב ומתנקם | 16 |
kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.
כל-זאת באתנו ולא שכחנוך ולא-שקרנו בבריתך | 17 |
Hayo yote yametutokea, ingawa tulikuwa hatujakusahau wala hatujaenda kinyume na agano lako.
לא-נסוג אחור לבנו ותט אשרינו מני ארחך | 18 |
Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako.
כי דכיתנו במקום תנים ותכס עלינו בצלמות | 19 |
Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, na ukatufunika kwa giza nene.
אם-שכחנו שם אלהינו ונפרש כפינו לאל זר | 20 |
Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni,
הלא אלהים יחקר-זאת כי-הוא ידע תעלמות לב | 21 |
je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo?
כי-עליך הרגנו כל-היום נחשבנו כצאן טבחה | 22 |
Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.
עורה למה תישן אדני הקיצה אל-תזנח לנצח | 23 |
Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? Zinduka! Usitukatae milele.
למה-פניך תסתיר תשכח ענינו ולחצנו | 24 |
Kwa nini unauficha uso wako na kusahau taabu na mateso yetu?
כי שחה לעפר נפשנו דבקה לארץ בטננו | 25 |
Tumeshushwa hadi mavumbini, miili yetu imegandamana na ardhi.
קומה עזרתה לנו ופדנו למען חסדך | 26 |
Inuka na utusaidie, utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho.