< תהילים 138 >
לדוד אודך בכל-לבי נגד אלהים אזמרך | 1 |
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote; mbele ya miungu nitakuimbia sifa.
אשתחוה אל-היכל קדשך ואודה את-שמך-- על-חסדך ועל-אמתך כי-הגדלת על-כל-שמך אמרתך | 2 |
Nitasujundu mbele ya hekalu lako takatifu na kulishukuru jina lako kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na kwa uaminifu wako. Umelifanya muhimu zaidi neno lako na jina lako kuliko kitu chochote.
ביום קראתי ותענני תרהבני בנפשי עז | 3 |
Siku ile niliyo kuita, ulinijibu; ulinitia moyo na kuitia nguvu nafsi yangu.
יודוך יהוה כל-מלכי-ארץ כי שמעו אמרי-פיך | 4 |
Wafalme wote wa nchi watakushukuru wewe, Yahwe, maana watasikia maneno kutoka kinywani mwako.
וישירו בדרכי יהוה כי-גדול כבוד יהוה | 5 |
Hakika, wataimba kuhusu matendo ya Yahwe, kwa kuwa utukufu wa Yahwe ni mkuu.
כי-רם יהוה ושפל יראה וגבה ממרחק יידע | 6 |
Maana ingawa Yahwe yuko juu, lakini anawajali wanyenyekevu, lakini hawatambui wenye majivuno.
אם-אלך בקרב צרה-- תחיני על אף איבי תשלח ידך ותושיעני ימינך | 7 |
Nijapopita katikati ya hatari, wewe utauhifadhi uhai wangu; utanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa.
יהוה יגמר בעדי יהוה חסדך לעולם מעשי ידיך אל-תרף | 8 |
Yahwe yuko pamoja nami hadi mwisho; uaminifu wa agano lako, Yahwe, wadumu milele. Usiwaache wale ambao mikono yako imewaumba.