< תהילים 136 >
הודו ליהוה כי-טוב כי לעולם חסדו | 1 |
Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
הודו לאלהי האלהים כי לעולם חסדו | 2 |
Oh, Mshukuruni Mungu wa miungu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
הודו לאדני האדנים כי לעולם חסדו | 3 |
Oh, mshukuruni Bwana wa mabwana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
לעשה נפלאות גדלות לבדו כי לעולם חסדו | 4 |
Mshukuruni yeye ambaye peke yake hufanya maajabu makuu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
לעשה השמים בתבונה כי לעולם חסדו | 5 |
Yeye aliyezifanya mbingu kwa hekima zake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
לרקע הארץ על-המים כי לעולם חסדו | 6 |
Mshukuruni yeye alitetandaza nchi juu ya maji, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
לעשה אורים גדלים כי לעולם חסדו | 7 |
Yeye aliyefanya mianga mikubwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
את-השמש לממשלת ביום כי לעולם חסדו | 8 |
Mshukuruni yeye alipaye jua kutawala mchana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
את-הירח וכוכבים לממשלות בלילה כי לעולם חסדו | 9 |
Mwezi na nyota vitawale usiku, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
למכה מצרים בבכוריהם כי לעולם חסדו | 10 |
Mshukuruni yeye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
ויוצא ישראל מתוכם כי לעולם חסדו | 11 |
Akawatoa Waisraeli kati yao, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
ביד חזקה ובזרוע נטויה כי לעולם חסדו | 12 |
Kwa mkono hodari na mkono ulio nyooshwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
לגזר ים-סוף לגזרים כי לעולם חסדו | 13 |
Mshukuruni yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
והעביר ישראל בתוכו כי לעולם חסדו | 14 |
Na kuwapitisha Waisraeli katikati yake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
ונער פרעה וחילו בים-סוף כי לעולם חסדו | 15 |
Lakini akamtupa Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
למוליך עמו במדבר כי לעולם חסדו | 16 |
Mshukuruni yeye aliye waongoza watu wake jangwani, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wa milele.
למכה מלכים גדלים כי לעולם חסדו | 17 |
Yeye aliyewaua wafalme wakuu, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wadumu milele.
ויהרג מלכים אדירים כי לעולם חסדו | 18 |
Mshukuruni yeye aliyewaua wafalme maarufu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
לסיחון מלך האמרי כי לעולם חסדו | 19 |
Sihoni mfalme wa Waamori, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
ולעוג מלך הבשן כי לעולם חסדו | 20 |
Na Ogu, mfalme wa Bashani, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
ונתן ארצם לנחלה כי לעולם חסדו | 21 |
Mshukuruni yeye aliyewapa nchi yao kama urithi, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
נחלה לישראל עבדו כי לעולם חסדו | 22 |
Urithi wa Israel mtumishi wake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
שבשפלנו זכר לנו כי לעולם חסדו | 23 |
Yeye aliyetukumbuka na kutusaidia katika unyonge wetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
ויפרקנו מצרינו כי לעולם חסדו | 24 |
Mshukuruni yeye ambaye ametupa ushindi juu ya aui zetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
נתן לחם לכל-בשר כי לעולם חסדו | 25 |
Yeye awapaye chakula viumbe hai wote, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
הודו לאל השמים כי לעולם חסדו | 26 |
Oh, mshukuruni Mungu wa mbinguni, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.