< תהילים 119 >

אשרי תמימי-דרך-- ההלכים בתורת יהוה 1
Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana.
אשרי נצרי עדתיו בכל-לב ידרשוהו 2
Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.
אף לא-פעלו עולה בדרכיו הלכו 3
Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake.
אתה צויתה פקדיך-- לשמר מאד 4
Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu.
אחלי יכנו דרכי-- לשמר חקיך 5
Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako!
אז לא-אבוש-- בהביטי אל-כל-מצותיך 6
Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote.
אודך בישר לבב-- בלמדי משפטי צדקך 7
Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki.
את-חקיך אשמר אל-תעזבני עד-מאד 8
Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa.
במה יזכה-נער את-ארחו-- לשמר כדברך 9
Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
בכל-לבי דרשתיך אל-תשגני ממצותיך 10
Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.
בלבי צפנתי אמרתך-- למען לא אחטא-לך 11
Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.
ברוך אתה יהוה-- למדני חקיך 12
Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako.
בשפתי ספרתי-- כל משפטי-פיך 13
Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako.
בדרך עדותיך ששתי-- כעל כל-הון 14
Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi.
בפקודיך אשיחה ואביטה ארחתיך 15
Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.
בחקתיך אשתעשע לא אשכח דברך 16
Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.
גמל על-עבדך אחיה ואשמרה דברך 17
Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako.
גל-עיני ואביטה-- נפלאות מתורתך 18
Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.
גר אנכי בארץ אל-תסתר ממני מצותיך 19
Mimi ni mgeni duniani, usinifiche amri zako.
גרסה נפשי לתאבה-- אל-משפטיך בכל-עת 20
Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa juu ya sheria zako wakati wote.
גערת זדים ארורים-- השגים ממצותיך 21
Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako.
גל מעלי חרפה ובוז כי עדתיך נצרתי 22
Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika sheria zako.
גם ישבו שרים בי נדברו-- עבדך ישיח בחקיך 23
Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako.
גם-עדתיך שעשעי-- אנשי עצתי 24
Sheria zako ni furaha yangu, nazo ni washauri wangu.
דבקה לעפר נפשי חיני כדברך 25
Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.
דרכי ספרתי ותענני למדני חקיך 26
Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako.
דרך-פקודיך הבינני ואשיחה בנפלאותיך 27
Nijulishe mafundisho ya mausia yako, nami nitatafakari maajabu yako.
דלפה נפשי מתוגה קימני כדברך 28
Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako.
דרך-שקר הסר ממני ותורתך חנני 29
Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako.
דרך-אמונה בחרתי משפטיך שויתי 30
Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako.
דבקתי בעדותיך יהוה אל-תבישני 31
Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, usiniache niaibishwe.
דרך-מצותיך ארוץ כי תרחיב לבי 32
Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.
הורני יהוה דרך חקיך ואצרנה עקב 33
Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho.
הבינני ואצרה תורתך ואשמרנה בכל-לב 34
Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote.
הדריכני בנתיב מצותיך כי-בו חפצתי 35
Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha.
הט-לבי אל-עדותיך ואל אל-בצע 36
Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.
העבר עיני מראות שוא בדרכך חיני 37
Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.
הקם לעבדך אמרתך-- אשר ליראתך 38
Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa.
העבר חרפתי אשר יגרתי כי משפטיך טובים 39
Niondolee aibu ninayoiogopa, kwa kuwa sheria zako ni njema.
הנה תאבתי לפקדיך בצדקתך חיני 40
Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako.
ויבאני חסדך יהוה תשועתך כאמרתך 41
Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako,
ואענה חרפי דבר כי-בטחתי בדברך 42
ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako.
ואל-תצל מפי דבר-אמת עד-מאד כי למשפטך יחלתי 43
Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.
ואשמרה תורתך תמיד-- לעולם ועד 44
Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele.
ואתהלכה ברחבה כי פקדיך דרשתי 45
Nitatembea nikiwa huru, kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
ואדברה בעדתיך נגד מלכים ולא אבוש 46
Nitasema sheria zako mbele za wafalme wala sitaaibishwa,
ואשתעשע במצותיך אשר אהבתי 47
kwa kuwa ninazifurahia amri zako kwa sababu ninazipenda.
ואשא-כפי--אל-מצותיך אשר אהבתי ואשיחה בחקיך 48
Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, nami ninatafakari juu ya maagizo yako.
זכר-דבר לעבדך-- על אשר יחלתני 49
Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini.
זאת נחמתי בעניי כי אמרתך חיתני 50
Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
זדים הליצני עד-מאד מתורתך לא נטיתי 51
Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, hata hivyo sitaiacha sheria yako.
זכרתי משפטיך מעולם יהוה ואתנחם 52
Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani, nazo zinanifariji.
זלעפה אחזתני מרשעים-- עזבי תורתך 53
Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako.
זמרות היו-לי חקיך-- בבית מגורי 54
Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi.
זכרתי בלילה שמך יהוה ואשמרה תורתך 55
Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako.
זאת היתה-לי כי פקדיך נצרתי 56
Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako.
חלקי יהוה אמרתי-- לשמר דבריך 57
Ee Bwana, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako.
חליתי פניך בכל-לב חנני כאמרתך 58
Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako.
חשבתי דרכי ואשיבה רגלי אל-עדתיך 59
Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.
חשתי ולא התמהמהתי-- לשמר מצותיך 60
Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako.
חבלי רשעים עודני תורתך לא שכחתי 61
Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako.
חצות-לילה--אקום להודות לך על משפטי צדקך 62
Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.
חבר אני לכל-אשר יראוך ולשמרי פקודיך 63
Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao, kwa wote wanaofuata mausia yako.
חסדך יהוה מלאה הארץ חקיך למדני 64
Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako.
טוב עשית עם-עבדך-- יהוה כדברך 65
Mtendee wema mtumishi wako Ee Bwana, sawasawa na neno lako.
טוב טעם ודעת למדני כי במצותיך האמנתי 66
Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako.
טרם אענה אני שגג ועתה אמרתך שמרתי 67
Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.
טוב-אתה ומטיב למדני חקיך 68
Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako.
טפלו עלי שקר זדים אני בכל-לב אצר פקודיך 69
Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.
טפש כחלב לבם אני תורתך שעשעתי 70
Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako.
טוב-לי כי-עניתי-- למען אלמד חקיך 71
Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.
טוב-לי תורת-פיך-- מאלפי זהב וכסף 72
Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.
ידיך עשוני ויכוננוני הבינני ואלמדה מצותיך 73
Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.
יראיך יראוני וישמחו כי לדברך יחלתי 74
Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.
ידעתי יהוה כי-צדק משפטיך ואמונה עניתני 75
Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.
יהי-נא חסדך לנחמני-- כאמרתך לעבדך 76
Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
יבאוני רחמיך ואחיה כי-תורתך שעשעי 77
Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.
יבשו זדים כי-שקר עותוני אני אשיח בפקודיך 78
Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.
ישובו לי יראיך וידעו (וידעי) עדתיך 79
Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako.
יהי-לבי תמים בחקיך-- למען לא אבוש 80
Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe.
כלתה לתשועתך נפשי לדברך יחלתי 81
Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.
כלו עיני לאמרתך-- לאמר מתי תנחמני 82
Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?”
כי-הייתי כנאד בקיטור-- חקיך לא שכחתי 83
Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako.
כמה ימי-עבדך מתי תעשה ברדפי משפט 84
Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?
כרו-לי זדים שיחות-- אשר לא כתורתך 85
Wenye majivuno wananichimbia mashimo, kinyume na sheria yako.
כל-מצותיך אמונה שקר רדפוני עזרני 86
Amri zako zote ni za kuaminika; unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu.
כמעט כלוני בארץ ואני לא-עזבתי פקדיך 87
Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako.
כחסדך חיני ואשמרה עדות פיך 88
Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako.
לעולם יהוה-- דברך נצב בשמים 89
Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.
לדר ודר אמונתך כוננת ארץ ותעמד 90
Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu.
למשפטיך עמדו היום כי הכל עבדיך 91
Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.
לולי תורתך שעשעי-- אז אבדתי בעניי 92
Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu.
לעולם לא-אשכח פקודיך כי בם חייתני 93
Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.
לך-אני הושיעני כי פקודיך דרשתי 94
Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako.
לי קוו רשעים לאבדני עדתיך אתבונן 95
Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako.
לכל-תכלה ראיתי קץ רחבה מצותך מאד 96
Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka.
מה-אהבתי תורתך כל-היום היא שיחתי 97
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.
מאיבי תחכמני מצותך כי לעולם היא-לי 98
Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima.
מכל-מלמדי השכלתי כי עדותיך שיחה לי 99
Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.
מזקנים אתבונן כי פקודיך נצרתי 100
Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako.
מכל-ארח רע כלאתי רגלי-- למען אשמר דברך 101
Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako.
ממשפטיך לא-סרתי כי-אתה הורתני 102
Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.
מה-נמלצו לחכי אמרתך-- מדבש לפי 103
Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!
מפקודיך אתבונן על כן שנאתי כל-ארח שקר 104
Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.
נר-לרגלי דברך ואור לנתיבתי 105
Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
נשבעתי ואקימה-- לשמר משפטי צדקך 106
Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki.
נעניתי עד-מאד יהוה חיני כדברך 107
Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana, sawasawa na neno lako.
נדבות פי רצה-נא יהוה ומשפטיך למדני 108
Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.
נפשי בכפי תמיד ותורתך לא שכחתי 109
Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako.
נתנו רשעים פח לי ומפקודיך לא תעיתי 110
Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako.
נחלתי עדותיך לעולם כי-ששון לבי המה 111
Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu.
נטיתי לבי לעשות חקיך-- לעולם עקב 112
Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.
סעפים שנאתי ותורתך אהבתי 113
Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.
סתרי ומגני אתה לדברך יחלתי 114
Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako.
סורו-ממני מרעים ואצרה מצות אלהי 115
Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!
סמכני כאמרתך ואחיה ואל-תבישני משברי 116
Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa.
סעדני ואושעה ואשעה בחקיך תמיד 117
Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako.
סלית כל-שוגים מחקיך כי-שקר תרמיתם 118
Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure.
סגים--השבת כל-רשעי-ארץ לכן אהבתי עדתיך 119
Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako.
סמר מפחדך בשרי וממשפטיך יראתי 120
Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako.
עשיתי משפט וצדק בל-תניחני לעשקי 121
Nimetenda yaliyo haki na sawa, usiniache mikononi mwa watesi wangu.
ערב עבדך לטוב אל-יעשקני זדים 122
Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee.
עיני כלו לישועתך ולאמרת צדקך 123
Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli.
עשה עם-עבדך כחסדך וחקיך למדני 124
Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako.
עבדך-אני הבינני ואדעה עדתיך 125
Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu ili niweze kuelewa sheria zako.
עת לעשות ליהוה-- הפרו תורתך 126
Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa.
על-כן אהבתי מצותיך-- מזהב ומפז 127
Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi,
על-כן כל-פקודי כל ישרתי כל-ארח שקר שנאתי 128
na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, nachukia kila njia potovu.
פלאות עדותיך על-כן נצרתם נפשי 129
Sheria zako ni za ajabu, hivyo ninazitii.
פתח דבריך יאיר מבין פתיים 130
Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.
פי-פערתי ואשאפה כי למצותיך יאבתי 131
Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako.
פנה-אלי וחנני-- כמשפט לאהבי שמך 132
Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.
פעמי הכן באמרתך ואל-תשלט-בי כל-און 133
Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale.
פדני מעשק אדם ואשמרה פקודיך 134
Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako.
פניך האר בעבדך ולמדני את-חקיך 135
Mwangazie mtumishi wako uso wako na unifundishe amri zako.
פלגי-מים ירדו עיני-- על לא-שמרו תורתך 136
Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi.
צדיק אתה יהוה וישר משפטיך 137
Ee Bwana, wewe ni mwenye haki, sheria zako ni sahihi.
צוית צדק עדתיך ואמונה מאד 138
Sheria ulizoziweka ni za haki, ni za kuaminika kikamilifu.
צמתתני קנאתי כי-שכחו דבריך צרי 139
Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu wanayapuuza maneno yako.
צרופה אמרתך מאד ועבדך אהבה 140
Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, mtumishi wako anazipenda.
צעיר אנכי ונבזה פקדיך לא שכחתי 141
Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, sisahau mausia yako.
צדקתך צדק לעולם ותורתך אמת 142
Haki yako ni ya milele, na sheria yako ni kweli.
צר-ומצוק מצאוני מצותיך שעשעי 143
Shida na dhiki zimenipata, lakini amri zako ni furaha yangu.
צדק עדותיך לעולם הבינני ואחיה 144
Sheria zako ni sahihi milele, hunipa ufahamu ili nipate kuishi.
קראתי בכל-לב ענני יהוה חקיך אצרה 145
Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote, nami nitayatii maagizo yako.
קראתיך הושיעני ואשמרה עדתיך 146
Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako.
קדמתי בנשף ואשועה לדבריך (לדברך) יחלתי 147
Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako.
קדמו עיני אשמרות-- לשיח באמרתך 148
Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.
קולי שמעה כחסדך יהוה כמשפטך חיני 149
Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.
קרבו רדפי זמה מתורתך רחקו 150
Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, lakini wako mbali na sheria yako.
קרוב אתה יהוה וכל-מצותיך אמת 151
Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu, na amri zako zote ni za kweli.
קדם ידעתי מעדתיך כי לעולם יסדתם 152
Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.
ראה-עניי וחלצני כי-תורתך לא שכחתי 153
Yaangalie mateso yangu, uniokoe, kwa kuwa sijasahau sheria yako.
ריבה ריבי וגאלני לאמרתך חיני 154
Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.
רחוק מרשעים ישועה כי חקיך לא דרשו 155
Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.
רחמיך רבים יהוה כמשפטיך חיני 156
Ee Bwana, huruma zako ni kuu, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.
רבים רדפי וצרי מעדותיך לא נטיתי 157
Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako.
ראיתי בגדים ואתקוטטה-- אשר אמרתך לא שמרו 158
Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako.
ראה כי-פקודיך אהבתי יהוה כחסדך חיני 159
Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.
ראש-דברך אמת ולעולם כל-משפט צדקך 160
Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.
שרים רדפוני חנם ומדבריך (ומדברך) פחד לבי 161
Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.
שש אנכי על-אמרתך-- כמוצא שלל רב 162
Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi.
שקר שנאתי ואתעבה תורתך אהבתי 163
Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo, lakini napenda sheria yako.
שבע ביום הללתיך-- על משפטי צדקך 164
Ninakusifu mara saba kwa siku, kwa ajili ya sheria zako za haki.
שלום רב לאהבי תורתך ואין-למו מכשול 165
Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.
שברתי לישועתך יהוה ומצותיך עשיתי 166
Ee Bwana, ninangojea wokovu wako, nami ninafuata amri zako,
שמרה נפשי עדתיך ואהבם מאד 167
Ninazitii sheria zako, kwa sababu ninazipenda mno.
שמרתי פקודיך ועדתיך כי כל-דרכי נגדך 168
Nimetii mausia yako na sheria zako, kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako.
תקרב רנתי לפניך יהוה כדברך הבינני 169
Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako, nipe ufahamu sawasawa na neno lako.
תבוא תחנתי לפניך כאמרתך הצילני 170
Maombi yangu na yafike mbele zako, niokoe sawasawa na ahadi yako.
תבענה שפתי תהלה כי תלמדני חקיך 171
Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.
תען לשוני אמרתך כי כל-מצותיך צדק 172
Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki.
תהי-ידך לעזרני כי פקודיך בחרתי 173
Mkono wako uwe tayari kunisaidia, kwa kuwa nimechagua mausia yako.
תאבתי לישועתך יהוה ותורתך שעשעי 174
Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.
תחי-נפשי ותהללך ומשפטך יעזרני 175
Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, na sheria zako zinitegemeze.
תעיתי-- כשה אבד בקש עבדך כי מצותיך לא שכחתי 176
Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. Mtafute mtumishi wako, kwa kuwa sijasahau amri zako.

< תהילים 119 >