< תהילים 118 >

הודו ליהוה כי-טוב כי לעולם חסדו 1
Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
יאמר-נא ישראל כי לעולם חסדו 2
Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
יאמרו-נא בית-אהרן כי לעולם חסדו 3
Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
יאמרו-נא יראי יהוה כי לעולם חסדו 4
Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
מן-המצר קראתי יה ענני במרחב יה 5
Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana, naye akanijibu kwa kuniweka huru.
יהוה לי לא אירא מה-יעשה לי אדם 6
Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?
יהוה לי בעזרי ואני אראה בשנאי 7
Bwana yuko pamoja nami, yeye ni msaidizi wangu. Nitawatazama adui zangu wakiwa wameshindwa.
טוב לחסות ביהוה-- מבטח באדם 8
Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kumtumainia mwanadamu.
טוב לחסות ביהוה-- מבטח בנדיבים 9
Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wakuu.
כל-גוים סבבוני בשם יהוה כי אמילם 10
Mataifa yote yalinizunguka, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
סבוני גם-סבבוני בשם יהוה כי אמילם 11
Walinizunguka pande zote, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
סבוני כדבורים-- דעכו כאש קוצים בשם יהוה כי אמילם 12
Walinizunguka kama kundi la nyuki, lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
דחה דחיתני לנפל ויהוה עזרני 13
Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka, lakini Bwana alinisaidia.
עזי וזמרת יה ויהי-לי לישועה 14
Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu.
קול רנה וישועה--באהלי צדיקים ימין יהוה עשה חיל 15
Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!
ימין יהוה רוממה ימין יהוה עשה חיל 16
Mkono wa kuume wa Bwana umeinuliwa juu, mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!”
לא-אמות כי-אחיה ואספר מעשי יה 17
Sitakufa, bali nitaishi, nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda.
יסר יסרני יה ולמות לא נתנני 18
Bwana ameniadhibu vikali, lakini hakuniacha nife.
פתחו-לי שערי-צדק אבא-בם אודה יה 19
Nifungulie malango ya haki, nami nitaingia na kumshukuru Bwana.
זה-השער ליהוה צדיקים יבאו בו 20
Hili ni lango la Bwana ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.
אודך כי עניתני ותהי-לי לישועה 21
Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu.
אבן מאסו הבונים-- היתה לראש פנה 22
Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni.
מאת יהוה היתה זאת היא נפלאת בעינינו 23
Bwana ametenda hili, nalo ni la kushangaza machoni petu.
זה-היום עשה יהוה נגילה ונשמחה בו 24
Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya, tushangilie na kufurahi ndani yake.
אנא יהוה הושיעה נא אנא יהוה הצליחה נא 25
Ee Bwana, tuokoe, Ee Bwana, utujalie mafanikio.
ברוך הבא בשם יהוה ברכנוכם מבית יהוה 26
Heri yule ajaye kwa jina la Bwana. Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki.
אל יהוה--ויאר-לנו אסרו-חג בעבתים--עד קרנות המזבח 27
Bwana ndiye Mungu, naye ametuangazia nuru yake. Mkiwa na matawi mkononi, unganeni kwenye maandamano ya sikukuu hadi kwenye pembe za madhabahu.
אלי אתה ואודך אלהי ארוממך 28
Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.
הודו ליהוה כי-טוב כי לעולם חסדו 29
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

< תהילים 118 >