< תהילים 115 >

לא לנו יהוה לא-לנו כי-לשמך תן כבוד--על-חסדך על-אמתך 1
Sio kwetu, Yahwe, sio kwetu, bali kwa jina lako ulete heshima, kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na uaminifu wako.
למה יאמרו הגוים איה-נא אלהיהם 2
Kwa nini mataifa yalazimike kusema, “Yuko wapi Mungu wako?”
ואלהינו בשמים-- כל אשר-חפץ עשה 3
Mungu wetu aliye mbinguni; hufanya chochote apendacho.
עצביהם כסף וזהב מעשה ידי אדם 4
Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
פה-להם ולא ידברו עינים להם ולא יראו 5
Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
אזנים להם ולא ישמעו אף להם ולא יריחון 6
zina masikio, lakini hazisikii; zina pua lakini hazinusi.
ידיהם ולא ימישון--רגליהם ולא יהלכו לא-יהגו בגרונם 7
Sanamu hizo zina mikono, lakini hazishiki; zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala haziongei kutoka viywani mwao.
כמוהם יהיו עשיהם-- כל אשר-בטח בהם 8
Wale wanao zitengeneza wanafanana nazo, vile vile yeyote anaye amini katika hizo.
ישראל בטח ביהוה עזרם ומגנם הוא 9
Israeli, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
בית אהרן בטחו ביהוה עזרם ומגנם הוא 10
Nyumba ya Haruni, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
יראי יהוה בטחו ביהוה עזרם ומגנם הוא 11
Ninyi mnao mheshumu Yahwe, mwamini yeye; yeye ni msaada wenu na ngao yenu.
יהוה זכרנו יברך יברך את-בית ישראל יברך את-בית אהרן 12
Yahwe hutukumbuka sisi na atatubariki; ataibariki familia ya Israeli; atabariki familia ya Haruni.
יברך יראי יהוה-- הקטנים עם-הגדלים 13
Atawabariki wale wanao muheshimu yeye, wote vijana na wazee.
יסף יהוה עליכם עליכם ועל בניכם 14
Yahwe na awaongeze ninyi zaidi na zaidi, ninyi pamoja na watoto wenu.
ברוכים אתם ליהוה-- עשה שמים וארץ 15
Yahwe na awabariki, aliyeziumba mbingu na nchi.
השמים שמים ליהוה והארץ נתן לבני-אדם 16
Mbingu ni za Yahwe; lakini nchi amewapa wanadamu.
לא המתים יהללו-יה ולא כל-ירדי דומה 17
Wafu hawamsifu Yahwe, wala wote washukao chini kwenye ukimya;
ואנחנו נברך יה-- מעתה ועד-עולם הללו-יה 18
bali tutamtukuza Yahwe sasa na hata milele. Msifuni Yahwe.

< תהילים 115 >