< תהילים 11 >

למנצח לדוד ביהוה חסיתי--איך תאמרו לנפשי נודו (נודי) הרכם צפור 1
Ni kwako Yahweh ninapata usalama; ni kwa namna gani utasema na mimi, “Ruka kama ndege hadi mlimani”?
כי הנה הרשעים ידרכון קשת כוננו חצם על-יתר-- לירות במו-אפל לישרי-לב 2
Tazama! Waovu wana andaa pinde zao. Wana tayarisha gizani mishale yao kwenye kamba ili kufyatua mioyo ya wenye haki.
כי השתות יהרסון-- צדיק מה-פעל 3
Ikiwa misingi imeharibiwa, mwenye haki atafanya nini?
יהוה בהיכל קדשו-- יהוה בשמים כסאו עיניו יחזו-- עפעפיו יבחנו בני אדם 4
Yahweh yuko katika hekalu takatifu; macho yake yanatazama, yakiuchunguza ubinadamu.
יהוה צדיק יבחן ורשע ואהב חמס--שנאה נפשו 5
Yahweh huwachunguza wote wenye haki na waovu, bali huwachukia wapendao kuwaumiza wengine.
ימטר על-רשעים פחים אש וגפרית ורוח זלעפות--מנת כוסם 6
Yeye huwanyeshea waovu makaa ya mawe na moto wa jehanamu; upepo uunguzao utakuwa ni sehemu yao kutoka katika kikombe chake!
כי-צדיק יהוה צדקות אהב ישר יחזו פנימו 7
Kwa kuwa Yahweh ni mwenye haki, Naye hupenda haki; wenye haki watauona uso wake.

< תהילים 11 >